jajcom
Senior Member
- Jan 4, 2013
- 125
- 191
Mheshimiwa asante sana kwa ushauri wako. Naona kuna vitu unavijua pasipo shaka sasa pls nimashine zipi ambazo ni nzuri especially zisizosumbua.
UPDATED!..
Kwa kipndi kirefu tumekuwa tukijadili swala zima la kutibu maji kwa njia ya nadhalia, hivyo nimeona vyema leo kuwaletea michoro husika, machine, gharama na kazi zake ili iwe fursa kwa watu wanaohitaji kuingia katika biashara ya kutibu maji ya kunywa na kuyapaki kwenye chupa.
Hapa nitatoa gharama ya kiwandani ya vifaa ambayo inaambatana na warrant ya mwaka mmoja, sitaweka gharama za kusafirisha, kodi etc.
Gharama hizi zinatoka katika kampuni kubwa na ya kwanza nchini India kwa kusambaza mashine za kutibu maji ndani na nje ya nchi.
HATUA YA KWANZA
Vifaa vinavyotumika katika mfumo mzima wa kutibu maji (Reverse Osmosis (RO) system)
Jinsi mfumo unavyofungwa kupokea maji, kutibu na kutoa maji safi na salama
HATUA YA PILI
Uwezo wa mtambo kutibu maji kulingana na jinsi ulivyobuniwa, Mtambo una uwezo wa kutoa parameters zifuatazo baada ya kutibu maji.
HATUA YA TATU
Vitu vya msingi kwa mteja ili kuwezesha mtambo kufanya kazi kulingana design basis. Chumba cha kutibu maji kinatakiwa kiwe na feed water, power-electricity, na chemicals kwa ajili ya kusafisha membrane (tumia Antiscalant chemical).
HATUA YA NNE
Technical specification ya kila mashine kwa kuzingatia uwezo wake, kazi inayofanya na idadi.
HATUA YA TANO
Hapa nimependekeza automatic machine katika chumba cha packaging, machine hii inafanya zake zote automatically. Miongoni mwa kazi za hii machine ni kujaza maji kwenye chupa, kuosha chupa & vifuniko, kufunga vifuniko kwenye chupa, kutengeneza chupa (blowing), n.k
Lakini pia Digital batch coding machine kwa ajili ya kutoa code kwenye chupa za maji na kuprint expire date kwenye chupa
HATUA YA SITA
Hii ni mashine inaitwa semi Automatic Pet blow Molding Machine, kazi yake kubwa ni kutengeneza shape za chupa kwa kufanya molding. Inafanya kazi kwa haraka zaidi kwani ina uwezo wa kutengeneza chupa ya lita 1 ndani ya sekunde 10 tu.
HATUA YA SABA
Hii machine inaitwa Bottle Group Shrink Packing Machine, inafanya kazi ya kupack maji kwenye carton kwa ajili ya kuanza kusambaza.
HATUA YA NANE
Gharama ya machine zote, kumbuka hii ni bei ya kiwandani kabla ya kusafirisha, kodi n.k Lakini kufungiwa machine (installation) na manufacturer ni 100USD/siku.
Jumla ya gharama za machine ni USD 53,269/- = Milioni 116
HATUA YA TISA
Huu ndio mfumo mzima wa kiwanda kuanzia kutibu maji mpaka mpaka kupack katika carton.
MWISHO
Mbali na hizo machine, pipe zitakuwa chini ya mteja na mambo mengine yanayohusiana na kiwanda. Jambo la msingi katika kiwanda cha maji, ni kweli biashara ya maji inalipa sio lazima usafirishe nchi nzima badala yake unaweza kujikita katika mkoa mmoja tu, ukahakikisha unakuwa na uwezo wa kusambaza maji maeneo yote ya mji ikiwezekana mpaka wilaya za jirani.
Kuwa huru kuuliza chochote. Naomba kuwasilisha,