BADILI TABIA
JF-Expert Member
- Jun 13, 2011
- 32,772
- 23,164
Mada muhimu hii
Nitarudi
Nitarudi
Hii itasaidia na watu ambao hatuna watoto na mungu akipenda soon tutaitwa mababaWengi wetu humu tunalea ama watoto wetu ama watoto wa ndugu jamaa na marafiki
Tumekuwa na mada maalum nyingi za mambo tofauti kama urembo magari simu nk ..lakini hatujawahi kuwa na mada hii maalum ya watoto
Kumlea mtoto tangu kutungwa kwa mimba mpaka kuzaliwa na hatimaye kulelewa mpaka kuvuka kile kipindi cha hatari si jambo dogo. Changamoto ni nyingi hasa na zingine hatujui jinsi ya kuzitatua lakini tukiwa na hii mada hapa jukwaani tutashirikishana na kujuzana mengi kwa haraka na uhakika zaidi
Kuna vitu vidogo vidogo ambavyo havihitaji daktari au ufumbuzi wake ni kama huduma ya kwanza kabla hujapata usaidizi mwingine. .HII NI TOFAUTI NA JF DOCTOR
kwa mfano ufanyeje
-mtoto anapolialia
-mtoto anapopata gesi tumboni
-mtoto anapopaliwa kila akila chochote
-mtoto anaposhtuka shtuka usiku na kulia sana nk k
Hatari zimnyemeleazo mtoto
-umeme
-maji
-Moto
-mwanga wa tv
-Simu , mawimbi yake
-vyombo na vitu mbalimbali
-madawa na vipodozi nk nk
Hii ni mada pana yenye mambo mengi mno
Kwa mfano kitunguu saumu ni tiba kwa mtoto anayelia na kushtuka usiku
Kijiko cha asali ni tiba kwa mtoto anayekohoa mfululizo (ukiacha kifua na mafua
Vitu kama mahirizi ya kiunoni na mkononi havimsaidii mtoto
Muda mwingi kumvalisha mtoto nguo nyingi humsababishia nimonia nk nk
Mambo ni mengi...
IKIWAPENDEZA ITAKUWA NI MADA MAALUM YA WATOTO
Mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha. ....!
Ukirudi na kukuta wameanza kuongelea wa kuanzia miaka 9 ni-mention BADILI TABIAMada muhimu hii
Nitarudi
Ndo akuje hapa...
Hili la chakula aina moja teh ni shida utadhani kuna ratiba ya kupewa uji, watoto tunawaonea kuwapa uji kila siku kila siku ndo maana hata wanakua wanasumbua kuunywa-kumlazimisha mtoto chakula asichopenda au kumpa chakula cha aina moja kila siku hii humpotezea mtoto hamu ya kula
Naufatiria kwa makini sana huu uzi...
Kuna wazazi underground ndo muda wa kufahamiana!!!
Hahha umeona enh... nasubir experience yako na weweAhahahahah ukisikia ngo ngo ngo ujue kuna mtu anagonga
Hahha umeona enh... nasubir experience yako na wewe
Mtoto anatakiwa ajaribiwe vyakula tofauti tofauti ajue ladha..Hili la chakula aina moja teh ni shida utadhani kuna ratiba ya kupewa uji, watoto tunawaonea kuwapa uji kila siku kila siku ndo maana hata wanakua wanasumbua kuunywa
Hata sio umasikini kiivo mazoea pia afu uji ni kitu cha fasta ndo maanaMtoto anatakiwa ajaribiwe vyakula tofauti tofauti ajue ladha..
asubuhi uji
Mchana mpondee maboga
Mpondee karoti
Nk
Nk
Sema tatizo ni umasikini tu
Unajua kuna wengine wanawapa hadi viporo vya ujiHata sio umasikini kiivo mazoea pia afu uji ni kitu cha fasta ndo maana
Kuna vikohozi vikavu visivyokoma hapa dawa yake ni Kijiko kidogo cha asali na kama una maziwa fresh unaweza kumchanganyia humo...hii haina madhara kabisa na kama ni mdogo zaidi humpi kwenye Kijiko bali unamlambishaMshana ungefafanua vizuri kuhusu Asali, nijuavyo ni hatari sana kumpa mtoto mdogo Asali mbichi. At least akishazidi miaka mi5.
Kuhusu Pneumonia inasababishwa zaidi na baridi. Ukimwona mtoto anatetemeka sanaaa wakati wa baridi usitumie dawa yoyote zaidi ya chai ya rangi yenye tangawizi kidogo then mfunike alale. Akiamka yupo shwariii.
Shukran mshana jr kwa ubunifu wa mada hii.