Kwa wazazi na walezi: Mada maalum ya watoto

Wengi wetu humu tunalea ama watoto wetu ama watoto wa ndugu jamaa na marafiki
Tumekuwa na mada maalum nyingi za mambo tofauti kama urembo magari simu nk ..lakini hatujawahi kuwa na mada hii maalum ya watoto
Kumlea mtoto tangu kutungwa kwa mimba mpaka kuzaliwa na hatimaye kulelewa mpaka kuvuka kile kipindi cha hatari si jambo dogo. Changamoto ni nyingi hasa na zingine hatujui jinsi ya kuzitatua lakini tukiwa na hii mada hapa jukwaani tutashirikishana na kujuzana mengi kwa haraka na uhakika zaidi
Kuna vitu vidogo vidogo ambavyo havihitaji daktari au ufumbuzi wake ni kama huduma ya kwanza kabla hujapata usaidizi mwingine. .HII NI TOFAUTI NA JF DOCTOR
kwa mfano ufanyeje
-mtoto anapolialia
-mtoto anapopata gesi tumboni
-mtoto anapopaliwa kila akila chochote
-mtoto anaposhtuka shtuka usiku na kulia sana nk k

Hatari zimnyemeleazo mtoto
-umeme
-maji
-Moto
-mwanga wa tv
-Simu , mawimbi yake
-vyombo na vitu mbalimbali
-madawa na vipodozi nk nk
Hii ni mada pana yenye mambo mengi mno
Kwa mfano kitunguu saumu ni tiba kwa mtoto anayelia na kushtuka usiku
Kijiko cha asali ni tiba kwa mtoto anayekohoa mfululizo (ukiacha kifua na mafua
Vitu kama mahirizi ya kiunoni na mkononi havimsaidii mtoto
Muda mwingi kumvalisha mtoto nguo nyingi humsababishia nimonia nk nk
Mambo ni mengi...
IKIWAPENDEZA ITAKUWA NI MADA MAALUM YA WATOTO
Mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha. ....!
Hii itasaidia na watu ambao hatuna watoto na mungu akipenda soon tutaitwa mababa
 
Mshana ungefafanua vizuri kuhusu Asali, nijuavyo ni hatari sana kumpa mtoto mdogo Asali mbichi. At least akishazidi miaka mi5.

Kuhusu Pneumonia inasababishwa zaidi na baridi. Ukimwona mtoto anatetemeka sanaaa wakati wa baridi usitumie dawa yoyote zaidi ya chai ya rangi yenye tangawizi kidogo then mfunike alale. Akiamka yupo shwariii.

Shukran mshana jr kwa ubunifu wa mada hii.
 
Mshana ungefafanua vizuri kuhusu Asali, nijuavyo ni hatari sana kumpa mtoto mdogo Asali mbichi. At least akishazidi miaka mi5.

Kuhusu Pneumonia inasababishwa zaidi na baridi. Ukimwona mtoto anatetemeka sanaaa wakati wa baridi usitumie dawa yoyote zaidi ya chai ya rangi yenye tangawizi kidogo then mfunike alale. Akiamka yupo shwariii.

Shukran mshana jr kwa ubunifu wa mada hii.
Kuna vikohozi vikavu visivyokoma hapa dawa yake ni Kijiko kidogo cha asali na kama una maziwa fresh unaweza kumchanganyia humo...hii haina madhara kabisa na kama ni mdogo zaidi humpi kwenye Kijiko bali unamlambisha
 
147 Reactions
Reply
Back
Top Bottom