Kwa wazazi na walezi: Mada maalum ya watoto

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
280,865
730,440
Wengi wetu humu tunalea ama watoto wetu ama watoto wa ndugu jamaa na marafiki.

Tumekuwa na mada maalum nyingi za mambo tofauti kama urembo magari simu n.k. lakini hatujawahi kuwa na mada hii maalum ya watoto.

Kumlea mtoto tangu kutungwa kwa mimba mpaka kuzaliwa na hatimaye kulelewa mpaka kuvuka kile kipindi cha hatari si jambo dogo.

Changamoto ni nyingi hasa na zingine hatujui jinsi ya kuzitatua lakini tukiwa na hii mada hapa jukwaani tutashirikishana na kujuzana mengi kwa haraka na uhakika zaidi.

Kuna vitu vidogo vidogo ambavyo havihitaji daktari au ufumbuzi wake ni kama huduma ya kwanza kabla hujapata usaidizi mwingine. HII NI TOFAUTI NA JF DOCTOR.

Kwa mfano, ufanyeje;

  • Mtoto anapolialia
  • Mtoto anapopata gesi tumboni
  • Mtoto anapopaliwa kila akila chochote
  • Mtoto anaposhtuka shtuka usiku na kulia sana nk k

Hatari zimnyemeleazo mtoto;
  • Umeme
  • Maji
  • Moto
  • Mwanga wa Tv
  • Simu, mawimbi yake
  • Vyombo na vitu mbalimbali
  • Madawa na vipodozi nk nk

Hii ni mada pana yenye mambo mengi mno.

Kwa mfano kitunguu saumu ni tiba kwa mtoto anayelia na kushtuka usiku, Kijiko cha asali ni tiba kwa mtoto anayekohoa mfululizo (ukiacha kifua na mafua), Vitu kama mahirizi ya kiunoni na mkononi havimsaidii mtoto, Muda mwingi kumvalisha mtoto nguo nyingi humsababishia nimonia n.k.

Mambo ni mengi...

IKIWAPENDEZA ITAKUWA NI MADA MAALUMU YA WATOTO..

Mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha..!
 
1453558063331.jpg
1453558080528.jpg
1453558090857.jpg
1453558101556.jpg
1453558109770.jpg
 
Wazazi wengi siku hizi hatuna muda na watoto wetu... Watoto wamekuwa ni wa wadada wa kazi na walimu, makuzi ya mtoto kiakili na kimaadili yanahitaji uwepo na ukaribu wa mtoto kuliko mtu mwingine yeyote yule.

Pamoja na harakati za kimaisha lakini ni vema ni muhimu na kuna wakati kutenga muda wa kukaa na familia yako ili kile ukitafutacho kiwe na manufaa na baraka mbeleni.

Dada wa kazi ana sehemu yake na majukumu yake ambayo ni 1/4
Mwalimu ana sehemu yake na majukumu yake ambayo ni 1/4 pia
Mzazi ana majukumu yake ambayo ni 1/2

Kwahiyo kama mzazi usibweteke nusu nzima ya malezi ya mtoto inakuhusu wewe.
 
Kati ya mambo yanayonikosesha raha ni jinsi hawa madriver wa hizi school bus walivyokosa umakini waendeshapo watoto wetu.

Nilshuhudia ajali ya bus la shule iliopelekea kupoteza uhai wa watoto watatu hapo hapo...niliumia mno na siwezi sahau tukio lile.

Toka siku hiyo huwa najitahidi sana asubuh kuhakikisha na wadrop watoto wangu shuleni kwao mwenyewe nimeshindwa tu kuwachukua jioni.

Kweli kuna changa moto sana kumlea mtoto hadi akue
 
Kati ya mambo yanayonikosesha raha ni jinsi hawa madriver wa hizi school bus walivyokosa umakini waendeshapo watoto wetu...Nilshuhudia ajali ya bus la shule iliopelekea kupoteza uhai wa watoto watatu hapo hapo...niliumia mno na siwezi sahau tukio lile...Toka siku hiyo huwa najitahidi sana asubuh kuhakikisha na wadrop watoto wangu shuleni kwao mwenyewe nimeshindwa tu kuwachukua jioni..Kweli kuna changa moto sana kumlea mtoto hadi akue.
Japo tunadhani kuwa changamoto za malezi ya mimba ni nyingi lakini kiuhalisia changamoto kubwa na za muda mrefu ni baada ya mtoto kuzaliwa mpaka atoke kwenye kile kipindi cha 'danger zone'
 
ahsante sana, kumbe ndiyo maana watoto dar wanapata hako kaugonjwa!
Kuna baadhi ya matatizo ya watoto husababishwa na wazazi au walezi
  • Kumpa mtoto chakula kingi kupita kiasi hapo unatafuta obesity
  • Kumlazimisha mtoto chakula asichopenda au kumpa chakula cha aina moja kila siku hii humpotezea mtoto hamu ya kula
  • Kutomvisha mtoto nguo sahihi kwa wakati sahihi
 
Inategemea na mazingira. .kwa mfano mazingira ya joto ni mbaya kwakuwa mtoto hutoa jasho kwa ndani na kuleta unyevunyevu ambao huumiza mapafu ya mtoto

Hili jambo nimekuwa najaribu kusema lakini wazazi wetu yani wakwe na mama zetu huchangia sana kuumiza watoto ktk eneo hili kwa kisingizio mtoto anahitaji joto mtoto huwa hasikii joto wanashindwa kuelewa dar ni tofauti pengine na mkoani ulipozaliwa wewe au bibi huyo alipokuzia watoto wake wengine unaenda clinic daktari anakushangaa jinsi ulivyomjaza mtoto nguo nyingi kabaki macho tu.wazazi tuwe makini hawa ni wakubwa zetu ila panapobidi kuwaelewesha tufanye hivyo vinginevyo ni sisi ndio tunakuja kupata shida na watoto wetu badae.
 
Back
Top Bottom