Shadow7
JF-Expert Member
- Sep 28, 2020
- 13,777
- 20,172
Kabisa mkuuChanzo: Hotuba ya Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto ya Mwaka 2020/2021.sorry to say this but sometimes hizi report hazina uhalisia
Kabisa mkuuChanzo: Hotuba ya Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia wazee na watoto ya Mwaka 2020/2021.sorry to say this but sometimes hizi report hazina uhalisia
Mungu atusaidieVilivyoandikwa 'weka mbali na watoto'
viwekwe mbali nao kweli.
Leo kuna mmoja wa miaka 3 kabugia super glue
Yeah inaitwa nimonia ya jotoahsante sana, kumbe ndiyo maana watoto dar wanapata hako kaugonjwa!
Wengi wetu humu tunalea ama watoto wetu ama watoto wa ndugu jamaa na marafiki.
Tumekuwa na mada maalum nyingi za mambo tofauti kama urembo magari simu n.k. lakini hatujawahi kuwa na mada hii maalum ya watoto.
Kumlea mtoto tangu kutungwa kwa mimba mpaka kuzaliwa na hatimaye kulelewa mpaka kuvuka kile kipindi cha hatari si jambo dogo.
Changamoto ni nyingi hasa na zingine hatujui jinsi ya kuzitatua lakini tukiwa na hii mada hapa jukwaani tutashirikishana na kujuzana mengi kwa haraka na uhakika zaidi.
Kuna vitu vidogo vidogo ambavyo havihitaji daktari au ufumbuzi wake ni kama huduma ya kwanza kabla hujapata usaidizi mwingine. HII NI TOFAUTI NA JF DOCTOR.
Kwa mfano, ufanyeje;
- Mtoto anapolialia
- Mtoto anapopata gesi tumboni
- Mtoto anapopaliwa kila akila chochote
- Mtoto anaposhtuka shtuka usiku na kulia sana nk k
Hatari zimnyemeleazo mtoto;
- Umeme
- Maji
- Moto
- Mwanga wa Tv
- Simu, mawimbi yake
- Vyombo na vitu mbalimbali
- Madawa na vipodozi nk nk
Hii ni mada pana yenye mambo mengi mno.
Kwa mfano kitunguu saumu ni tiba kwa mtoto anayelia na kushtuka usiku, Kijiko cha asali ni tiba kwa mtoto anayekohoa mfululizo (ukiacha kifua na mafua), Vitu kama mahirizi ya kiunoni na mkononi havimsaidii mtoto, Muda mwingi kumvalisha mtoto nguo nyingi humsababishia nimonia n.k.
Mambo ni mengi...
IKIWAPENDEZA ITAKUWA NI MADA MAALUMU YA WATOTO..
Mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha..!
SanaMungu atusaidie
Sidhani kama hili ni tatizo lakini naomba nimualike Dr Faustine Ndugulile na Dr. WansegamilaMwanangu mpaka sasa miaka 2 na mwezi mmoja utosi bado unadunda vp Kuna tatizo?
Prim K njoo utoe msaada hapaMwanangu mpaka sasa miaka 2 na mwezi mmoja utosi bado unadunda vp Kuna tatizo?
Halafu ukimpima hospital hana tatizo loloteHuku Tanga Kuna kitu kinaitwa Zongo, mtoto anapigwa yeye ni kulia tu na kuharisha, na tumbo kuuma, unaweza kumpa kila aina ya dawa lakini wapi, ila ukienda kwa hao wataalam wenyewe wa kutegua mabomu, unakuta mtoto anapona kwa Tsh 5000 tu, mimi nilikua mbishi ila mwisho wa siku nuliamsha mkono, unakuta mtoto anadhoofika mpaka unamuonea huruma,
Yaani hospital wanakwambia ni joto tu wanakupa madawa kibao ila unayatumia yote ila mtoto anazidi kunyongea,Halafu ukimpima hospital hana tatizo lolote