Nimezitumia card za Benki zote 2.
Equity wanabana kwenye refund hadi msumbuane
BANCABC wao shida ipo kwenye makato ya hapa na pale yaani ukiuliza salio kwa mobile banking wanakata,kila online transaction wanakata kiwango fulani pia ukijaribu kununua kitu wakati salio lako halitoshi wanakupiga penalt 1200 kila unavyojaribu.
Wakati mwingine unaweza kuhamisha salio toka kwenye tigo/mpesa ukapata ujumbe muamala umekamilika ila zikachelewa kuingia kwenye system yao nawe ukajaribu nunua vitu unapata ujumbe hela haitoshi na zikija kuingia unakuta wameshafanya yao kwenye penalt.
Hiyo ndio shida yao hao jamaa ila kwenye refund wapo poa.
Equity nimepotezea refund kama mbili hivi toka aliexpress.
So bora BANCABC japo umakini wahitajika