Kwa watu wa mkoa wa Mara

Maelezo yako na ushauri wako nakubaliana nao kwa kiasi kikubwa.
Isipokuwa nilitaka nikufahamishe jambo moja kwamba wakazi wa serengeti kwa asili shughuli zao kubwa ni ufugaji, kilimo na uwindaji, wamekuwa wakifanya uwindaji huo miaka na miaka lakini bado hawakuvuruga ecosystem kama ambavyo tumekuwa tukilazimishwa kuamini. Wananchi wa serengeti hawajawahi kutegemea uwindaji kama njia kuu ya kujipatia kipato ama maendeleo bali kilimo na ufugaji.

Suala la vijana kukaa kijiweni lilikuwepo na bado lipo kutoakana na kutokuwa na mwamko wa elimu, ingawa sasa mambo ni tofauti sana, vijana wengi sana sasa wanasoma na hao ndio mategemeo makubwa kwa ajili ya maendeleo ya wilaya yetu.

Nikizungumzia ajira za Mahotelini sio kweli sana kama unavyodai, tunao vijana ambao si wengi waliokuwa wamesomea kozi za hoteli na utalii lakini bado hawakupata ajira katika mahoteli yaliyoanzishwa, hii ilisababishwa na mameneja waajiri wengi kuajiri watu wao ama watu kutoka huko kwao, kiujumla kulikuwa na upendeleo mkubwa sana. Mimi binafsi mdogo wangu alikuwa amemaliza certificate ya hotel management lakini alifanya intervie mara tatu na kuachwa, alipokuja dar akafanikiwa kupata kazi hotel moja hapa jijini. Baada ya wananchi kulalamika kwamba watoto wao hawaajiriwi na badala yake wanaajiriwa watu wengine hasa kutoka Arusha, Kilimanjaro, Mwanza na Kenya ndipo baadhi ya waliokuwa na sifa wakapata nafsi ya kuajiriwa na mdogo wangu wakamuita na kwakuwa walimpa maslahi mazuri comapred na huku alikokuwa nikamshauri aende.

Lakini pamoja na hayo yote niliyosema bado tunawajibika kupigana zaidi ili kufikia malengo kama mikoa na wilaya nyingine.

Mkuu kwa jinsi watu wa wilaya ya serengeti na tarime walivyo wachapa kazi wakiamka kielimu naamin watafika mbali sana japo kuna vikwazo vya kimfumo kama vile makao makuu makuu ya hifdhi kuwekwa Arusha bila sababu za msingi.Tuweke mkakati wa pamoja ili vijna wasomi + wengine wa maeneo hayo wakumbuke kuwekeza huko kwani tuko ambao sio wa huko kiasili lakin tunapenda mkoa huo kwa jinsi tunvyoujua tofauti na watu wengine ambao huwa wanakimbilia tu kukosoa mkoa huo kw maneno bila kufanya critical analysis ili kujua undani wa masuala yalivyo.Lets work up,wakisikia kuna fursa watakuja mbio tu.
 
Duh! lugha kali sana hiyo.Lakini ujumbe umefika,lugha uliyotumia tutaitumia kama changamoto kuanzisha muungano huu.Asante sana

Ndugu yangu nakuambia mimi sio mtu wa mkoa wa Mara lakini from my heart nachukizwa sana na vijana wa mkoa huu, wamejaa ukabila, ubaguzi na zaidi wanapenda vitu vyepesi vyepesi hawataki kuhangaisha akili zao walio wengi.Sasa ulishaona wapi eti kijana anaishi kwa kutafuta vimoro najua unajua nachomaanisha kama unatokea pande hizo.Eti kazi yake ni vimoro na kama msimu wa vimoro ni taabu basi yeye anakaa kijiweni kupiga stories mpaka usiku.
Mimi kuna kijana alifukuzwa kazi sehemu (secret) akaja akaniambia kuwa kibarua kimeisha, nilikaa nae nikampa mikakati nikamwambia huyo mwajiri sio mwisho wa maisha yako, there is another world somewhere waiting for you.Tulipeana mikakati nikamwambia maisha sio luxury maana sometime unatakiwa kijitesa but at the end of the day you remain focused.
Navokuambia kijana nilimpa mikakati nikamuunganisha Dar kwa jamaa zangu wanafanya kazi za umachina, nikamwambia ataanza kutembeza maji ya kunywa na juice za Azam.Kusema ukweli ilikuwa ngumu sana kumshawishi lakini alinikubalia nikamwambia for the first 4 months atakaa kwa hao jamaa zangu then baada ya hapo kitaeleweka tu.Nakuambia leo hii kashaachana na biashara ya maji sasa ananunua nguo Tandika then anakuja kuziuza Mwenge.Wewe unaona zile nguo za Mwenge pale unadhani eti watu wamefungua mabero mapya, hamna kitu zile nyingi zinachukuliwa Tandika, Tandale na Karume then kwa kuwa sie wa maofisini tuko busy tunapigwa bei mara mbili na jamaa anaishi sasa.
Cha msingi vijana wa mkoa wa Mara kwanza muachane na ukabila eti yule Muikizu,Mjaluo,Muikoma,mara wakurya wamegawanyika kuna wakurya wakila HAVITAWASAIDIA hata kidogo.Elimisheni vijana kuwa maisha ni mapambano na sio kutega vimoro, pia mkipata chance kwenye sehemu za Migodi na kwenye mahotel waiteni vijana wenu wafanye hata zile kazi ndogndogo na wakishaingia kwenye system watachanganya na zakwao.Please, tata mura mnialike kwenye kikao hicho maana nina hasira sana na vijana wa mkoa wa mara
 
Aii Muraah hayo nughambile ila notutokile bhukong'u abanto bha Mara.
Oronde ogi urasagi enduraneli.
Ghasi bhono nkehayo babe obhugile.

Ushauri wako una maana saana kwa watu wa Mara kutolewa sifa hizo ulizoziolodhesha hapo.
CDM itatuondoa kwenye masifa yale yaliyoasisiwa na CCM ya kuwa VIITIKIO kwenye
mikutano yao huku wachache wakifaidi kwa vigelegele vya walalahoi.
 
Mkuu hapana fikiria Kilimanjaro ni dizaini kama mkoa wa mara,kuna Wakibosho,wamarangu tena wakiraracha,wamachame,wakishimundu sijui wa mwika.Wao wanaenda ,mbalio sana hadi wanabaguana kwa koo.Mbona mambo yao yako sawasawa?

labda wao wanathamini wakina mama na michango ya kina mama maana ndugu zangu wa Mara kwa kudhalilisha wanawake siwawezi.
 
Bila kuwa na upendo miongoni mwetu kamwe hatutaweza wa2 wa Mara kiukweli hatutakiani mafanikio. Hili nimeliona kwangu mwenyewe kipindi nasaka ajira kama mjuavyo mbali na uwezo binafsi ajira bongo zinawezeshwa na nani anakupigia debe sehemu husika, kuna taasisi kama tatu niliitwa interview ya kwanza kulikuwa na wakubwa 2 from hometown Tarime tena walitia moyo kazi nimepata mwisho holaaa 2. bosi alikuwa 4rm Trm tena alinikubali sana na kunipromise ajira walai nikaangukia pua, ya 3 vilevile nikatamani hata majina yangu yasiwe ya kiukoo bt finally nikapata kwenye kampuni ambayo hakukuwa na n person 4rm Mara. nilijifunza nini hapa watu wa bukoba, mbeya kilimanjaro wanapendana hivyo vijana wao wengi sana wanaingia ktk mfumo wa ajira ili waweze kusaidia huko watokako sisi wapi zaidi ya kila 1 kutaka sifa za kuwa na uwezo zaidi?? ni vyema kama kuna nia ya dhati tuanzie swala la ajira kama m2 ana vigezo na uwezo upo na nafasi ya kusaidia ipo fanya hivyo naamini... wenye kuleta mabadiliko ya Mara ni ww mwenye uwezo kifedha na elimu kichwani na ondoa umimi mimi nimeanza kupigia debe vijana wetu wa Mara kupata ajira muhimu sifa anazo then namshauri kuangalia kuendeleza eneo la kijijin kwake.
 
tatizo ni la kuamini kwamba JWTZ ni Jeshi la Wakurya na Wajita Tangu Zamani
 
Nashukuru kwa post yako, ina mambo ya maana na ya kijinga pia,Mimi pia ni mzaliwa wa Serengeti kata ya Issenye, japo asili yangu ni Karatu Arusha,Tatizo kubwa la watu wa Mara ni ukabila, koo hili ni tatizo, mfano mzuri ni huyu mbunge wa sasa wa Serengeti nadhani ni mwiba kwa maendeleo ya Wilaya yetu. Ni mbaguzi sana nakumbuka kuna wakati tumemwomba kuandaa kikao cha pamoja cha wana serengeti waishio dar ili kujadili changamoto za wilaya yetu cha ajabu alikuja na watu toka Ngoreme tu, mwisho wa siku anasema yeye hawezi andaa tuandae halafu tumwite yeye atafacilitate, sasa jiulize huyu ni mtu wa aina gani ambaye hawezi kuandaa kikao na kuongea na watu wakelakini pia tusisahau adui mkubwa wa Serengeti na Mara kwa ujumla ni CCM, bila kuiondoa CCM hakuna litakalofanikiwa, nina mifano michache. Nimebahatika kufanya fatiti kadhaa Mkoa wa Mara na bahati nzuri nimepita vijiji vingi sana, wilaya ya Bunda inatisha kwa umaskini nimefanya utafiti wa umaskini na hali ya chakula na PACT nilichogundua tofauti na wilaya zingine za mkoa wa Mara huko Bunda hasa maeneo ya Kibara zaidi ya 50% ya wakazi wake wanapata mlo mmoja kwa siku. Nimezunguka Wegita, Maghena, Nyamongo, Murito, Kewanja, Kemambo na maeneo mengine huko Tarime kuna umaskini wa kutisha. Unyanyasaji kwa raia hasa maeneo yanayozunguka hifadhi na migodi ni mkubwa sana. Labda nitoe mfano mdogo tu Nyamongo kuna mzee mmoja wakati wanalipwa fidia kupisha upanuzi wa mgodi alipewa cheki ya milioni 60 kama malipo ya nyumba na shamba lake akakataa akasema ngoja awasiliane na wakili wake baada ya siku 2 alipelekewa cheki ya bilioni 2.labda kidogo nizungumzie Serengeti, kuna hifadhi 93.6% ya ardhi yote ya serengeti ipo ndani ya hifadhi na sasa 246 km2 zimemegwa kutoka kwenye vijiji kuingizwa kwenye WMA lakini wananchi hawafaidiki. Nipo Serengeti nafanya research kwa ajili ya dissertation yangu ya masters, na ninaangalia benefit sharing ya wildlife resources, kuna madudu mengi sana nimeyaona kwa kuwa bado sijasubmit siwezi weka data hapa ila hapo baadaye nitaleta but for clarification gnashon@yahoo.co.uk nitakujibu. Suala la barabara nadhani ni haki yetu kama raia wengine kuwa na barabara ya rami, kama hotel imejengwa kwenye migration corridor barabara ikipita kuna ubaya gani?Kuna diwani mmoja alikaimu uenyekiti wa council kwa miezi tisa mapato yaliongezeka kutoka milioni 600 mpaka 1.9 bilioni sasa jiulize ukusanyaji wa mapato serengeti ukoje?
 
Ni matumaini yangu kuwa mpo salama,kwa upande wangu namshukuru Mungu.
Kwanza kabisa ni-declare interest kwamba mimi ni wa mkoa wa Mara,wilaya ya Serengeti,tarafa ya Ngoreme,kata ya Kenyamonta.

Nina machache leo ya kuzungumza na wana-Mara wenzangu kuhusu mkoa wetu.

Mkoa wa mara ulikuwa na kasifa hivi hasa kalikoletwa na mwl nyerere,kwamba baba wa taifa kutoka mara.Zaidi ya hapo tunabaki na sifa za kijinga tu ambazo kimsingi haziujengi mkoa wetu bali kuudidimiza na sisi tunabaki kuchekelea tu huku nyumba inaungua.

Mji mkuu wa mkoa wa Mara ni Musoma mjini,mtakubaliana nami kuwa mji ule umekuwa kama mtoto aliyesumbuliwa na kwashiakoo kwa muda mrefu,yaani umedumaa,hauna mabadiliko chanya tangu nianze kuwa na ufahamu,bali unakuwa kwa kwenda nyuma.

Wilaya ya Serengeti na Taarime zimekuwa zikisifika kwa fujo na watu wake eti kuitwa majasiri,hizo ni sifa za kijinga na wanaotuita hivyo wanafanya makusudi kutudumaza kimaendeleo.

Wilaya ya Serengeti,Musoma vijijini,na Bunda zinaelekea kugeuka jangwa.Wachoma mikaa wamefyeka kupita kiasi,huku watendaji wa serikali wakiwepo tu.Hawana uchungu maana wengi wao ni wa kupita tu,sisi wakudumu ndo tumeamua kujitengenezea jangwa.


Ujasiri wetu uko wapi kama si ujinga,tuna sehemu kubwa ya ziwa victoria,samaki wanavuliwa,minofu inatolewa,kisha watu wetu wanakula mifupa(mapanki),huo ndio ujasiri.

Mbuga ya Serengeti kwa asilimia kubwa ipo mkoani Mara,lakini kupata nyama kama kitoweo kwa siku hizi kupitia mbuga ni dhambi ambayo adhabu yake ni kupigwa risasi hadi kufa.Kama mtakumbuka zamani kulikuwa na kipindi fulani kwa mwaka wanaruhusu wananchi kuwinda kwa ajiri ya kitoweo.Hakukua na tatizo,wala hatujawahi kusikia wanyama wamepungua,ilikuwa ecosystem ya kawaida kwani sisi ni sehemu ya mbuga.Mfumo umefutwa,mbuga sasa iko na VIP,ukitaka kutangulia mbele ya haki katiza mbugani.Tumebaki kuangalia tu,wamefika mahali twiga wanabebwa na kupelekwa nje,eti mkoa wa Mara ni majasiri,sifa za kijinga.


Madini ya dhahabu yapo kwa wingi mkoani Mara,kuna Nyamongo,Buhemba,Park Nyigoti,Majimoto japo kwa uchache.Tunafaidije kama si kusaidia mkoa wa Mara kuwa na takwimu ya juu kwa virusi vya ukimwi na ukimwi(7.8%)
Eti mkoa wa Mara ni majasiri,sifa za kijinga.


Mkoa umekosa chuo cha maana cha utalii na Hotel management,vipo vya hovyo tu.Vyuo vya maana vipo Arusha na hivyo waajiriwa wengi wa hotel za mbugani wanatoka Arusha,Mara tunabaki kulalamika tu.Eti sisi ni majasiri,sifa za kijinga hizi.

Rais analazimisha kupitisha barabara ya lami mbugani kwa maslahi yake binafsi(Kwa sababu ana hotel mbugani),watu wa mkoa wa mara tumenyamaza tu,wakati tunafahamu madhara yake.Eti majasiri,ujinga huu.

Mbuga ipo kwetu,ukipita barabara ya mbugani unalazimika kulipa ada ya kupita mbugani,kama vile wewe ni mtalii.Huu ni uhuni tunafanyiwa,udau wetu juu ya hii mbuga upo wapi.Kwanini ulazimishwe kukatwa pesa hiyo wakati hukuwa na mpango wa utalii.Eti Mara majasiri.

Tukiendelea kubweteka na sifa hizi za kijinga kuna wakati utafika Mara itatambulishwa kama sehemu ya Arusha,"AMINI NAWAAMBIENI"

Waliotufikisha hapa wanajulikana,imefika wakati Mkoa wa Mara kuanzisha muungano wa vijana wa MKOA.Vijana wa Mara wakiwa na sauti moja,wanaweza kupanga vipaumbele vya mkoa,na mwanasiasa yeyote atakaetaka ridhaa yetu aonyeshe nia ya dhati kabisa ya kushughulikia vipaumbele hivyo.Vijana tunaweza kufanya hivyo,lakini pia umefika wakati wa sisi vijana kuufanyia kitu mkoa wetu pamoja na taifa kwa ujumla.

Nilikuwa naongea na mmoja wa wabunge wa mkoa wa Mara eti anasema mkoa umedhorota kwa sababu vijana wake wengi ni walevi,so what?ana maanisha hakuna mabadiliko?kwanini aliomba uongozi.

Naomba tupeane maoni juu ya mkoa wetu,tukosoane kwa kujenga na ikiwezekana tuje na harakati mpya za kuujenga mkoa wetu.

Mods kama kuna madainayoendana na hii ilishatolewa naomba msii-combine,nataka kupata maoni ya wadau
.

mura bana nyia amnaga dogo mora mutarianzisha kweri mura!
 
Mkoa wa Mara umekuwa ni wa kuchuma mali. Viongozi wateule hawana uchungu wala hawafikirii kuendeleza mkoa wetu. Tusiposhtuka ndo hivo tena tutaendelewa kuliwa hadi tubaki mapanki.
 
Jambo moja linalonikera sana ambalo bado nalitafutia njia muafaka ya kuli address ni kitendo cha TANAPA kuweka makao makuu ya mbuga ya serengeti (SERENGETI NATIONAL PARK-SENAPA) mkoani Arusha. Hii ni dharau kubwa sana kwa wanaSerengeti lakini ajabu ni kwamba hakuna kiongozi yeyote anayeliona hili na kulipigia kelele.

Ndugu zangu wana Mara pamoja na mambo mengine, ni lazima tuishinikize serikali itupe haki yetu ya makao makuu ya mbuga ya serengeti kuwepo mkoani kwetu, wilayani kwetu mjini Mugumu.

Nimebahatika kufikka katika baadhi ya hifadhi/mbuga zetu zilizopo hapa nchini kama Mikumi, Manyara, Ngorongoro, Udzungwa, Ruaha, Kitulo, Saadani, Mkomazi, Tarangire huko kote makao makuu ya watendaji/ofisi za mbuga/hifadhi hizo ziko katika mbuga/hifadhi husika, kwanini sisi ya kwetu Serengeti iwekwe Arusha? kwa maslahi ya nani?

Mkuu Mimi mwenyewe nimezaliwa Serengeti na shule ya Msingi nimesoma Hukohuko, na juzi tu nilikuwa huko na kwakweli kuna Tatizo kubwa sana Wilaya ya Serengeti ila mimi niwalaumu sana wakazi/wazawa wa huko, Mimi sitakilaumu CHAMA CHA MAPINDUZI ingawa mimi ni CDM

1. Wakazi wa kule wamelala usingizi wa Pono

2. Ubunifu ni zero, hakuna ubunifu wowote, watu wamekalia kujenga Gest tu na Maduka ya rejareja

Wakazi wa Serengeti wanatakiwa kuamushwa, wamelala mno, kuna furusa nyingi sana Serengeti labda kuliko wilaya yoyote ile ya Mkoa wa Mara, Ila hakuna mtu anaye zifanyia kazi, watu wale wanahitaji elimu ya hali ya Juu kuhusu Ujasiriamali na uwekezaji,

KUHUSU SWALA LA MAKAO MAKUU YA HIFADHI YA SERENGETI

-Mkuu hapo napingana na wewe kwa asilimi 100, Makao makuu ya hifadhi ya Serengeti yapo Fort Ikoma, zamani yakikuwa Seronera ila kwa sasa ni Fort Ikoma,

- ARUSHA, kuna makao makuu ya hifadhi zote za Taifa means TANAPA
- Na kuhusu ishu ya Kujenga makao makuu ya TANAPA serengeti, hiyo si ishu sana hata kama yangejengwa wapi yasingekuwa na maana yoyote ile mkuu,

- Na kama ni ishu ya Mapato Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro ndo inaongoza Tanzania kwa kuingiza fedha nyingi sana kuliko hifadhi yoyote ile basi makaua makuu yangejengwa huko Kilimanjaro, na kilimanjaro inafuatiwa na Serengeti pamoja na Ngorongoro,

ILA WATU WA SERENGETI WANATAKIWA KUAMKA WENYEWE NA HAPO ISISINGIZIWE CCM,
 
Habari wanajanvi, mimi ni mzaliwa wa Mara hapo Musoma Mjini, kata ya Mwigobero, mtaa wa kawawa.Shule ya msingi nimesoma Mwembeni miaka ya themanini mpaka tisini na baadae Mara secondary.

Namshukuru mleta thread amejaribu kuelezea mambo muhimu sana na pengine kutukumbusha wengi wetu umuhimu wa nyumbani.Kwa kweli hali ya Mkoa wa Mara kwa Vijana na Wazee ni ya kusikitisha sana. Ukiangalia hali ya vijiji vya wazazi wangu yaani Mugango na Kwikubha pamoja na Bwai yaani ni bora hata alipokuwa mkoloni (kulikuwa na viwanda) leo hii ni magofu tu. Hali ya makazi duni na vijana ni pombe na mabinti.

Msaada mkubwa unahitajika kuuokoa mkoa kwa ujumla, tuna haja ya kubadilika kitabia na tulio nje tufikiri kurudi nyumbani mara kwa mara ili kusaidia ndugu zetu kimawazo na kimaendelea.

Zamani kulikuwa na ajira za kutosha kuanzia ziwani, bandarini na kilimo cha pamba.Leo hii yaani ufukara umetamalaki si mijini wala vijijini yaani ''bhonse manzi ga nyanza''.

Vijana wamekimbilia mijini na kazi kubwa sasa ni piki piki na baskeli.Tunashukuru kwa kusaidia suala la usafiri lakini wanatumiwa na wanaofaidika ni wale wenye mitaji (wamiliki wa piki piki hizo) na matokeo yake biashara isipokwenda vizuri ni kuishirizia kunyang'anywa na hatimaye vijana kushindwa kumudu maisha hivyo kuwa wezi.

Ziwani leo hakuna kitu, ujio wa viwanda vya samaki umekuwa na matokeo tofauti kabisa kwa wana Mara na havina tija sana kwa vijana wetu kwani soko na uvuvi vimetekwa na wachache wenye pesa hivyo kutumikisha nguvu kazi (vijana) kwa ujira tegemezi.

Vijana wametumiwa na wanasiasa mpaka kuvurugika akili (wako tayari kuwafia wanasiasa hao huku wanacho nufaika hakipo).

Kwa utangulizi huu, ni kujaribu kuonyesha hali iliyopo katika mkoa wangu.Nitarudi kutoa hatima ya ufumbuzi kwani pamoja tukishirikiana tunaweza.
 
Mkoa wa Mara ulipaswa kuwa one of the beautiful regions! Lakini mji umekufa, hakuna maendeleo, hotel nzuri leo nenda baada ya miezi michache imekufa e.g. matvla!
 
Kama nilivyoahidi kutoa suruhisho ama mchango kwa wanaMara wenzangu.

1) Kukubali sasa kubadilika kitabia kwa maana kuacha kubaguana kikabila wala kutumia ukabila kama nyenzo ya kujitambulisha katika mambo yasiyo ya msingi (kujinufaisha binafsi).

2)Kuacha kutumiwa na Wanasiasa uchwara wenye nia binafsi ya kujijenga huku vijana wakitumika kama ngazi (matumizi ya rushwa za muda na kuwaacha hoehae)

3)Vijana wetu kuzingatia elimu na kuepuka tamaa za kupata maisha ya anasa na ya haraka pasipo kusoma (hapa kuna changamoto japo zinaongeleka)

4)Viongozi wetu wasiowajibika ni muhimu wakawajibishwa na wananchi wenyewe (Hii imewahi kufanyika miaka fulani Mkurugenzi akang'ooka pamoja na baadhi ya madiwani wa Nyamatare,Mukendo kama sikosei.

5)Vijana na kina mama kuwezeshwa
kwa maana ya kupewa elimu ya ujasiria mali pamoja na mitaji katika fani tofauti kama vile ufugaji, kilimo cha bustani, ufundi mbao,uvuvi wa kawaida, kazi za matofali n.k ili kuwaondoa katika hali tegemezi ya wafanyabiashara wanyonyaji.

6)Kupeleka haraka huduma za kijamii kama vile umeme,maji, afya na bara bara zinazoweza kupitika muda wote.Hii itasaidi baadhi ya vijana kuona kijijini ni mahali bora pa kuishi na hivyo kupunguza idadi ya vijana kukimbilia mijini ambako kunashida kubwa badala ya neema.

7)Tuliofanikiwa nje ya Mkoa na Tanzania, kukubali kurudi nyumbani sio kisiasa tu ila kusaidi katika ushauri pamoja na mitaji katika umoja (saccos) ambao ni muhimu kuanzishwa na kina mama na vijana kila mtaa,kata,tarafa na pengine wilaya na mkoa kwa ujumla.Hapa tutasaidia kuinua watu wetu na kuwaondoa kwenye mikono ya wanyonyaji wanaokopesha kwa riba kubwa kama inavyofanyika sasa.

8)Kuwepo ushirikiano mkubwa baina ya viongozi wote wa mkoa pasipo kujali itikadi zao za kisiasa.Kuunganisha nguvu za wananchi ili kujiletea maendeleo yao pasipo kuwagawa kidini,kikabila na itikadi za kivyama.Hii ni sambamba na kusaidia kuibua miradi, kuweka mazingira bora ya kujiajiri pamoja na kuhakikisha usalama wao.

9)Kuwepo na uhakika wa soko la mazao toka shamba na hii itawezekana kwa kulima mazao yanayokubali ukame (kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi) na yenye matumizi ya aina mbili kama chakula na biashara (Mahindi,mihogo,mtama,ulezi!) hii itamsaidia Mkulima kuwa na akiba ya chakula pamoja na kuweza kuuza.Hali iliyopo sasa ni soko la msimu na njaa kali vijijini hasa kipindi cha kiangazi.Leo hii bei ya debe la Mahindi ama Udaga (mhogo) haishikiki si mijini na hata vijijini.

10)Kujaribu kuwa wabunifu kwa kuibua miradi na masoko nje ya nchi hasa kwa kutumia vizuri mpaka wa Sirari.Hali iliyopo sasa kiuchumi katika mpaka huo hairidhishi.Biashara za magendo ni kubwa na rushwa isiyomithirika mpakani hapo.

11)Kuwa makini sana na Wawekezaji uchwara ambao nia yao ni kuwanyonya wazalendo wa mkoa hasa Viwanda hivi vya ndugu zetu waasia.Ajira huko hazieleweki, bidhaa hasa samaki zinauzwa bei ya kutupa, malipo kuchelewa, umiliki wa ziwa na kuwaacha Wananchi kutonufaika na Ziwa lao.Leo kupata samaki wa kula nyumbani shida na gharama yake haishikiki kisa viwanda.

Haya ni machache nadhani wenzangu mna mengi katika maeneo tofauti ya mkoa.Sikuzungumzia bandari, mwaro wa Mwigobero, mbuga, madini kwani wenzangu wameongelea sana. Nimeepuka kuchomeka siasa kwani sasa tunajadili kwanza technical issues na siasa tutakabiliana nazo huko site.
 
Tanzania ni ya wote, sehemu palipo dumaa wakulaumiwa ni watanzania sote. Mnalaumu utafikiri kuna serikali za majimbo, ingeingia kidogo akilini kama kungekuwa na bajeti za mkoa na viongozi wa mkoa wawe wazawa ndo wanasimamia bajeti hiyo.

Tatizo la mahala fulani la kimaendeleo ni tatizo la kihistoria na linatakiwa lichambuliwe kulingana na historia. Mikoa iliyoendelea, sio kwamba imeendelea eti kwa sababu wameamuka ama nini.
Lazima tujifunze historia sio tu kwa kukumbuka bali pia kwa kuambatanisha viabata vyake ikiendana na uhalisia ulio sambamba na mkabala kulingana na majanibu husika.

Tukirejea, virejesho vya ukoloni ni kwamba kwa kuvipaparua juu juu vionjo vyake ni kuwa wakoloni waliendeleza kwa kiwango chao sehemu walipokubalika, na bahati mzuri ama mbaya wakoloni wa tanganyika walikuwa wazungu na walipokubalika ndo kuliandelezwa ili ku- embrace machief wengine ktk sehemu waliopinga mienendo ukwaju ya kikoloni.

Hili ni sawa na kusema kwanini umasaini hapajaendelea, eti ukajenga hoja na kuisimamia na kuiiamini ya kwamba wamasai hawajaendelea ama maeneo yao ni duni kwa sababu wanapenda ukabila.

Nina unga vuguvungu la chief Mkama-G'winangwa wa majita sehemu zile za chumwi kwa kusimama kidete kupinga sera kandamizi za kikoloni, na hata hivyo kidete bado tumekishikilia cha kupinga uvamizi na ukandamizaji japo bado tunalipa gharama kwa kuitwa tumelala fofo, wakabila nk.
 
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mzee Isdori Shirima aliwahi kuitisha mkutano wa uwekezaji kwenye mkoa ule. Alipohamishwa kila kitu kikapotea. Kwa maoni yangu hata hii TANAPA ilipaswa kujenga makao makuu yake pale Mugumu badala ya Arusha. Mara ina kila kitu lakini watu wake, mh! Wanaoneana wivu, wanabaguana, wanadharauliana, ubinafsi ndio wao.

Hakuna kitu kinanikeraga kama hiki. Yaani mbuga ipo Mara lakini makao makuu Arusha. Badala hata yangekua Mugumu ili waikoma, wangoreme, wanata na makabila mengine ya hapo yapate hata vibarua hapo.
 
Ni matumaini yangu kuwa mpo salama,kwa upande wangu namshukuru Mungu.
Kwanza kabisa ni-declare interest kwamba mimi ni wa mkoa wa Mara,wilaya ya Serengeti,tarafa ya Ngoreme,kata ya Kenyamonta.

Nina machache leo ya kuzungumza na wana-Mara wenzangu kuhusu mkoa wetu.

Mkoa wa mara ulikuwa na kasifa hivi hasa kalikoletwa na mwl nyerere,kwamba baba wa taifa kutoka mara.Zaidi ya hapo tunabaki na sifa za kijinga tu ambazo kimsingi haziujengi mkoa wetu bali kuudidimiza na sisi tunabaki kuchekelea tu huku nyumba inaungua.

Mji mkuu wa mkoa wa Mara ni Musoma mjini,mtakubaliana nami kuwa mji ule umekuwa kama mtoto aliyesumbuliwa na kwashiakoo kwa muda mrefu,yaani umedumaa,hauna mabadiliko chanya tangu nianze kuwa na ufahamu,bali unakuwa kwa kwenda nyuma.

Wilaya ya Serengeti na Taarime zimekuwa zikisifika kwa fujo na watu wake eti kuitwa majasiri,hizo ni sifa za kijinga na wanaotuita hivyo wanafanya makusudi kutudumaza kimaendeleo.

Wilaya ya Serengeti,Musoma vijijini,na Bunda zinaelekea kugeuka jangwa.Wachoma mikaa wamefyeka kupita kiasi,huku watendaji wa serikali wakiwepo tu.Hawana uchungu maana wengi wao ni wa kupita tu,sisi wakudumu ndo tumeamua kujitengenezea jangwa.


Ujasiri wetu uko wapi kama si ujinga,tuna sehemu kubwa ya ziwa victoria,samaki wanavuliwa,minofu inatolewa,kisha watu wetu wanakula mifupa(mapanki),huo ndio ujasiri.

Mbuga ya Serengeti kwa asilimia kubwa ipo mkoani Mara,lakini kupata nyama kama kitoweo kwa siku hizi kupitia mbuga ni dhambi ambayo adhabu yake ni kupigwa risasi hadi kufa.Kama mtakumbuka zamani kulikuwa na kipindi fulani kwa mwaka wanaruhusu wananchi kuwinda kwa ajiri ya kitoweo.Hakukua na tatizo,wala hatujawahi kusikia wanyama wamepungua,ilikuwa ecosystem ya kawaida kwani sisi ni sehemu ya mbuga.Mfumo umefutwa,mbuga sasa iko na VIP,ukitaka kutangulia mbele ya haki katiza mbugani.Tumebaki kuangalia tu,wamefika mahali twiga wanabebwa na kupelekwa nje,eti mkoa wa Mara ni majasiri,sifa za kijinga.


Madini ya dhahabu yapo kwa wingi mkoani Mara,kuna Nyamongo,Buhemba,Park Nyigoti,Majimoto japo kwa uchache.Tunafaidije kama si kusaidia mkoa wa Mara kuwa na takwimu ya juu kwa virusi vya ukimwi na ukimwi(7.8%)
Eti mkoa wa Mara ni majasiri,sifa za kijinga.


Mkoa umekosa chuo cha maana cha utalii na Hotel management,vipo vya hovyo tu.Vyuo vya maana vipo Arusha na hivyo waajiriwa wengi wa hotel za mbugani wanatoka Arusha,Mara tunabaki kulalamika tu.Eti sisi ni majasiri,sifa za kijinga hizi.

Rais analazimisha kupitisha barabara ya lami mbugani kwa maslahi yake binafsi(Kwa sababu ana hotel mbugani),watu wa mkoa wa mara tumenyamaza tu,wakati tunafahamu madhara yake.Eti majasiri,ujinga huu.

Mbuga ipo kwetu,ukipita barabara ya mbugani unalazimika kulipa ada ya kupita mbugani,kama vile wewe ni mtalii.Huu ni uhuni tunafanyiwa,udau wetu juu ya hii mbuga upo wapi.Kwanini ulazimishwe kukatwa pesa hiyo wakati hukuwa na mpango wa utalii.Eti Mara majasiri.

Tukiendelea kubweteka na sifa hizi za kijinga kuna wakati utafika Mara itatambulishwa kama sehemu ya Arusha,"AMINI NAWAAMBIENI"

Waliotufikisha hapa wanajulikana,imefika wakati Mkoa wa Mara kuanzisha muungano wa vijana wa MKOA.Vijana wa Mara wakiwa na sauti moja,wanaweza kupanga vipaumbele vya mkoa,na mwanasiasa yeyote atakaetaka ridhaa yetu aonyeshe nia ya dhati kabisa ya kushughulikia vipaumbele hivyo.Vijana tunaweza kufanya hivyo,lakini pia umefika wakati wa sisi vijana kuufanyia kitu mkoa wetu pamoja na taifa kwa ujumla.

Nilikuwa naongea na mmoja wa wabunge wa mkoa wa Mara eti anasema mkoa umedhorota kwa sababu vijana wake wengi ni walevi,so what?ana maanisha hakuna mabadiliko?kwanini aliomba uongozi.

Naomba tupeane maoni juu ya mkoa wetu,tukosoane kwa kujenga na ikiwezekana tuje na harakati mpya za kuujenga mkoa wetu.

Mods kama kuna madainayoendana na hii ilishatolewa naomba msii-combine,nataka kupata maoni ya wadau
.

Unastahili sifa. Umetoa Changamoto kwa wana Mara. Jamani Wana Mara tuamke.
 
Natoka Serengeti mtoa mada naomba uwakumbushe viongozi wote wanaotoka Mara maneno haya ya Mahatma Gadhi kuwa
ISHI KAMA VILE UTAKUFA KESHO,VILEVILE JIELIMISHE KAMA VILE UTAISHI MILELE.Natumai Mwl Jk yeye alijielimisha hivyo ndio maana bado ataishi milele.
 
Nawashauri kila mwenyeji wa mkoa wa Mara, kwanza wajikubali kwamba kwao ni Mara, pili kila mmoja aliyepata nafasi ya fanikiwa kiuchumi arudi nyumbani kuwekeza kuanzia makazi bora na kuanzisha biashara za huduma ya jamii. Na hii na kwa wakazi wa mikoa yote TZ, igeni 'December Chagga migration from all over the world to K'njaro'.
 
Back
Top Bottom