Kwa watu wa mkoa wa Mara

Wa mura!kama kweli kuna ndoto ya umoja!Vitu kama koo,dini au madhehebu,elimu,uchumi kwa muhusika visipewe kipaumbele,cha muhimu tu awe MwanaMara,tofauti na hapo tutaendelea kulalamika kama kawaida yetu Watz.Wazo nzuri kinachohitajka ni mbolea tu.
 
obhanto bhano....mi nafikiri ni mda wa action.mi npo chuon dar..lakin ntahakikisha kazi nakuja kufanyia nyumban kwetu mara.ntaanza kuwaonesha wenzngu fahari ya kupata elim na kuwatumikia watu wa kwenu!
 
Tatizo hata vijana wa Mara walioko mikoani nao wamekalia majungu tuuu, mkikutana vikao badala ya kuongea issues wanaanza kujadili watu na maisha yao, ni vikao vya show off zaid...fursa ziko nyingi nchi hii wala sio suala la kusema ni Mara pekee, nchi hii ina vitu vingi vizuri ila tumelala usingizi wa majungu,na ghilba tu...
 
Ninyi wa Serengeti hata msilalamike! Mnajiponza wenyewe na mapenzi yenu kwa CCM! Mnavuna mnachopanda!
Mapenzi kwa ccm yameanza lini?kama tatizo ni ccm,hatukatai,ni wakati sasa wa kuorodhesha obstacles,ikiwa ccm ni moja wapo iorodheshwe kwani kujua matatizo na hatua nzuri sana.
 
WildCard umesema jambo muhimu nililosahau,tunawadharau wahaya,lakini hawa jamaa ni wazalendo,wanajenga kwao nyumba nzuri,mjini wanajenga za biashara.Sisi tumekuwa limbukeni mno.Tumebaki kubaguana kikabila,vikabila vyenyewe vidogo,halafu maskini sana,shida tupu.Nimeandaa katiba,nataka nipate reg. ili tuanzishe muungano wa vijana wa Mara,naomba mniunge mkono.
Labda kwa ninyi vijana umoja wa aina hii unawezekana. Lakini hawa wazee wenzangu waliozaliwa miaka ya 40, 50 na 60 taabu kweli kuwaunganisha. Ukiwaweka pamoja kama Wakurya watakuuliza Mkurya yupi? Mnyamongo? Mtimbaru? Mkenye? Mwirege? Ukimwambia Mkenye atakuuliza Mkenye wa wapi? Wegero? Kongoto, Kabhainja?
 
Wa mura!kama kweli kuna ndoto ya umoja!Vitu kama koo,dini au madhehebu,elimu,uchumi kwa muhusika vipewe kipaumbele,cha muhimu tu awe MwanaMara,tofauti na hapo tutaendelea kulalamika kama kawaida yetu Watz.Wazo nzuri kinachohitajka ni mbolea tu.
 
Wa mura!kama kweli kuna ndoto ya umoja!Vitu kama koo,dini au madhehebu,elimu,uchumi kwa muhusika visipewe kipaumbele,cha muhimu tu awe MwanaMara,tofauti na hapo tutaendelea kulalamika kama kawaida yetu Watz.Wazo nzuri kinachohitajka ni mbolea tu.
Umenena ndugu,naamini hakuna kinachoshindikana.Kama nilivyosema nimeandaa draft ya katiba ya MUUNGANO WA VIJANA WA MARA,kwangu mimi ni step muhimu ya kuanzia.Mniunge mkono ndugu.
 
Kaaazi kweli!
Osaka tumuulize huyu jamaa ni wawapi?hakuna kinachoshikana,sisi tukiamua kuungana hatutaki kauri kama hizi.Tunataka kuungana,wangoreme,wakurya,wajita,wazanaki,waikizu,wakwaya vitu gani hivi.Kutaja tu na kujisifia kimakabila kutaleta maendeleo kiuchumi kweli.Watu wazima kabisa tunazungumzia vi sub-tribes hivi.
 
Mura, Obambiri mahene mura. Tugegehiri. Bonse tuberi kya barisya!

Mara tuamke. Kweli hata kwetu Majimoto hali ni mbaya kabisa. Kiagata ndo usiseme. juzi tumechimbiwa bwawa la hovyo kabisa kabisa! Wanaume tukalikataa. Sasa tuamke tuuendeleze mkoa wetu. lakini kwa shemeji zangu Majita nao ni bure kabisa. Kuna wasomi-madaktari na maprofesa wasiokuwa na idadi, lakini wote wanajenga Dar, Mwanza, Moshi, Arusha, Dodoma na kadhalika. Wanaogopa kujenga Murangi, Mabui Merafuru, Kinyambwiga hadi Masita (Busekera) kwa sababu ya kuogopa kulogwa. Huu nao ni ujinga mura! tuamke!

Sasa mkoa una mawaziri wasira, kabaka, makongoro mahanga, muhongo, mkangara; lakini wote bure. Una makatibu wakuu kama yule wa biashara, mifugo, maswi wa madini, na wengine kibao, lakini bure kabisa.

Mkoa una mkuu wa JKT ambaye ni mzanaki, una Katibu wa Chama Cha Magamba, una Mwanasheria Mkuu (Werema) na Naibu Mwanasheria Mkuu (Masaju); hawa wote hakuna kitu! Una majenertali Kiaro, Waitara, na Musuguri; lakini mambo mabaya kabisa. Wengine ongezeni jamani!
Mimi huwa nawaheshimu sana watu wa Mara maana huwa hawana unafiki wa kijinga.

Yes ni yes na no ni no.

Kitu cha maana ni kukuza biashara na vitega uchumi ndani ya mkoa.
Vitu hivyo vitaajiri vijana wengi na kuongeza pato la mtu mmoja mmoja.
Vitega uchumi si lazima iwe vile vizito vizito, hata viwanda vidogo vidogo vya kusindika mazao na ku process malighafi kwa kiwango cha viwanda vidogo vinatosha kuanzisha chachu ya maendeleo.

Nimefanya kazi huko kuanzia Sirari , Musoma hadi Bunda.
Mara is rich.
 
Mura, Obambiri mahene mura. Tugegehiri. Bonse tuberi kya barisya!

Mara tuamke. Kweli hata kwetu Majimoto hali ni mbaya kabisa. Kiagata ndo usiseme. juzi tumechimbiwa bwawa la hovyo kabisa kabisa! Wanaume tukalikataa. Sasa tuamke tuuendeleze mkoa wetu. lakini kwa shemeji zangu Majita nao ni bure kabisa. Kuna wasomi-madaktari na maprofesa wasiokuwa na idadi, lakini wote wanajenga Dar, Mwanza, Moshi, Arusha, Dodoma na kadhalika. Wanaogopa kujenga Murangi, Mabui Merafuru, Kinyambwiga hadi Masita (Busekera) kwa sababu ya kuogopa kulogwa. Huu nao ni ujinga mura! tuamke!

Sasa mkoa una mawaziri wasira, kabaka, makongoro mahanga, muhongo, mkangara; lakini wote bure. Una makatibu wakuu kama yule wa biashara, mifugo, maswi wa madini, na wengine kibao, lakini bure kabisa.Mkoa una mkuu wa JKT ambaye ni mzanaki, una Katibu wa Chama Cha Magamba, una Mwanasheria Mkuu (Werema) na Naibu Mwanasheria Mkuu (Masaju); hawa wote hakuna kitu! Una majenertali Kiaro, Waitara, na Musuguri; lakini mambo mabaya kabisa. Wengine ongezeni jamani!
Mwitongo, emwe nemwe abhasubhe murobhoha, etwe abhakari tukorebhwi?
 
MIMI ni born town wa IRINGA ila wazo hilo ni zuri sana.tatizo ni watu kujitambua na kujali waliko toka. wengi wetu tunadhani ukijenga Dar wewe umeukata kumbe ni ulofa tu.kila watu na wawe na DAR yao.tukiwa na ukereketwa wa huko tutokako tutaendelea. nimewahi kukaa na mmarekani mmoja kwao menisotta,alikuwa anaijali sana usiombe.badilikeni wandugu,na huu ni mwanzo mzuri, MMEJITAMBUA NA MMEGUNDUA TATIZO.Awork started is a work completed.
 
Kamwene,karibu sana mkoa wa mara.
Ita mukaruka ako ka msemo kakopo kana utatako.Nafikiripo umeterezako mwamba,eti
 
Mimi huwa nawaheshimu sana watu wa Mara maana huwa hawana unafiki wa kijinga.

Yes ni yes na no ni no.

Kitu cha maana ni kukuza biashara na vitega uchumi ndani ya mkoa.
Vitu hivyo vitaajiri vijana wengi na kuongeza pato la mtu mmoja mmoja.
Vitega uchumi si lazima iwe vile vizito vizito, hata viwanda vidogo vidogo vya kusindika mazao na ku process malighafi kwa kiwango cha viwanda vidogo vinatosha kuanzisha chachu ya maendeleo.

Nimefanya kazi huko kuanzia Sirari , Musoma hadi Bunda.
Mara is rich.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mzee Isdori Shirima aliwahi kuitisha mkutano wa uwekezaji kwenye mkoa ule. Alipohamishwa kila kitu kikapotea. Kwa maoni yangu hata hii TANAPA ilipaswa kujenga makao makuu yake pale Mugumu badala ya Arusha. Mara ina kila kitu lakini watu wake, mh! Wanaoneana wivu, wanabaguana, wanadharauliana, ubinafsi ndio wao.
 
Mkuu ukiangalia mbuga ya serengeti in jumla ya hotel 940,inzidiwa mara 5 na mbuga ya Masai Mara,wakati masai mara inaingia mara 4 kwenye ukubwa wa eneo la Serengeti.Watalii wanapata huduma nzuri wakiwa Masai mara kuliko serengeti,TANAPA wapo,viongozi wa serikali wapo,wanasiasa wapo na wananchi majasiri wapo.Tunaijenga Mara tunabomoa.Hakuna uwanja wa ndege wa maana,watalii wanatua Mwanza au Arusha.Uwanja wa ndege wa Mugumu umekuwa kitendawili.Tusaidiane tuiokoe Mara yetu jamani.
 
Ninyi wa Serengeti hata msilalamike! Mnajiponza wenyewe na mapenzi yenu kwa CCM! Mnavuna mnachopanda!

ccm ni sehemu tu ya matatizo mengi yanayochangia kurudisha nyuma maendeleo ya wilaya yetu ya Serengeti.
SAGANKA nakushukuru kwa kuleta hoja hii, najaribu kukusoma jinsi ulivyokereka kutokana na lugha uliyotumia lakini ujumbe wako umefika, na ndugu yangu Mwitongo nimekusoma hoja zako ni za kweli kabisa.

Mimi nimezaliwa na kukulia Kijiji cha Kibeyo, kata ya Kisangura wilayani Serengeti, kwahiyo ninaifahamu vizuri sana wilaya yetu ambayo nimefanikiwa kufika/kuitembelea karibu kona zote; kuanzia Machochwe, Mbirikili, Bonchugu, Rwamchanga, Miseke,Robanda, Bwitengi, Natta, Issenye, Ring'wani, Masinki, Kisaka, Kenyamonta, Majimoto, Iramba, Mara Somoche, Kebanchebanche, Merenga, Nyansurura, Mbalibali na kwingineko kwa kutaja vijiji vichache.

Cha kwanza kabisa kilichoturudisha nyuma, kwa upande wetu wilaya ya Serengeti ni mapigano ya koo. Kulikuwa na mapigano baina ya wangoreme na wanyabasi + watimbaru tangu miaka ya sabini huko ambayo yaliua watu wengti sana, hadi miaka ya hivi karibuni mapigano yamepungua sana lakini chuki na uhasama baodo upo. Tumeshuhudia mapigano mabaya sana miaka ya 80s baina ya wanyabasi + watimbaru dhidi ya wakira + walenchoka, tumeshuhudia mapigano baina ya wanyabasi + watimbaru dhidi ya waikoma + wanata + waisenye. Kama hiyo haitoshi, kulikuwa na uhasama mkubwa sana baina ya wakurya na wamaasai toka mkoa wa Arusha ambao walikuwa wakiiba ng'ombe kwa wingi sana toka wilayani kwetu hadi mwishoni mwa miaka ya tisini ndipo hali hiyo imekaoma kabisa baada ya kufanyika jitihada kubwa na mazungumzo baina ya wamaasai na wakurya.

Kama nilivyodokeza hapo awali sasahivi mapigano baina ya koo hizi yamepungua sana kama si kuisha lakini bado kuna chuki miongoni mwao na watu hawa hawaaminiani sana. Kipindi chote cha mapigano kwa ujumla koo zote zilishindwa kuweka mazingira mazuri ya elimu na afya. Hawakuweza kuwekeza vya kutosha katika elimu, hawakusomesha watoto wao bali walijikita katika kuwafundisha ujasiri wa kupambana na kulinda koo zao. Na ikumbukwe kwamba katika mapigano yote yaliyokuwa yakitokea baina ya koo kama nilivyotaja hapo awali, wizi wa mifugo hasa ngo'mbe, mbuzi na kondoo walikuwa wakiibiwa/kutaifishwa kwa wingi sana toka upande ulioshindwa vita, na kwakuwa koo zote za wilayani serengeti kwa sehemu kubwa ni wafugaji kwahiyo wakajikuta wakiishia kuwa fukara.

Jambo jengine ambalo lilisababisha kuendelea kuwepo kwa mapigano baina ya koo zetu ni viongozi wa kisiasa na vyombo vya dola, ambao walinufaika sana na hizi vurugu kwakuwa walitumia mwanya huo kupora mifugo ya wananchi kwa kisingizio cha kukabiliana na wizi na hatimaye kujigawia wao wenyewe. Viongozi wakubwa walionufaika sana na uporaji huo walikuwa ni wakuu wa wilaya-hapa namkumbuka marehemu Makunenge na mwingine mmoja akiitwa Zuberi ama Omary aliyefariki ghafla akiwa amelala, makamanda wa polisi wilaya(OCDs), wenyeviti wa baraza la madiwani-hapa namkumbuka mwenyekiti mmoja wa baraza la madiwani mwishoni mwa miaka ya 80 hadi mwanzoni mwa miaka ya 90 aliyekuwa akitokea ngoreme akiitwa Luge(nadhani alikuwa mwanajeshi mstaafu) alifaidika sana na ng'ombe wa koo za kikurya (wanyabasi, watimbaru na wakira).

Kwahiyo hiyo utaona ni kwa kiasi gani wananchi walikosa kabisa muda wa kufanya kazi za kujiletea maendeleo. Katika hali kama hiyo hata walewachache waliokuwa wamefanikiwa kusoma na kutaka kuwekeza nyumbani walishindwa kwakuwa hali ya usalama ilikuwa ni ndogo sana. Nakumbuka majengo mengi sana yaliyokuwa yameanza kujengwa mjini mugumu miaka ile ya themanini yote yaliishia kuporomoka kufuatia vita mbaya sana baina ya wanyabasi + watimbaru dhidi ya wakira + walenchoka, hii ilitokana na ukweli kwamba watu wengi waliokuwa na uwezo na kuanza kufanya ujenzi mjini mugumu walikuwa ni wanyabasi na wakira, sasa katika mazingira yale ya vita hakuna mtu aliyekuwa na uwezo wa kufanya ujenzi.

Ni miaka ya tisini ndipo sasa mji wa mugumu ulianza kujengwa kwa kasi sana baada ya kumalizika kwa uhasama mkubwa baina ya koo hizi na watu kujielekeza katika shughuli za maendeleo. Ndipo watu wakapata mwamko wa kuanza kuwekeza katika elimu, shule ya sekondari ya Serengeti ambayo wananchi wote wa wilaya walikuwa wameichangia tangu miaka ya sabini ndipo ikapata kufunguliwa na kuanza kupokea wanafunzi. Ikumbukwe kwamba kabla ya hapo wilaya yetu ilikuwa na shule moja tu ya sekondari ambayo ni ngoreme secondary.

Jambo jingine lililopelekea wilaya yetu kuwa nyuma sana kimaendeleo ni jamaa zetu waliofanikiwa kimaisha hasa waliosoma kwakuwa miaka ile wasomi ndio walikuwa na uwezo mzuri wa kufanya uwekezaji, wakaamua kususia nyumbani kwao, wakaamua kuwekeza huko wanakofanya kazi na kusahau kwamba nyumbani nako kunawahitaji. Na kwakuwa hawakuwekeza nyumbani kwao japo kujenga nyumba nzuri tu za kuishi, hata wanapostafu utumishi wao wanalazimika kuendelea kuishi huko huko mijini walikojenga majumba mazuri na kufanya uwekezaji kadhaa. Labda sasahivi ndio watu wanajitahidi kukumbuka kwao, nimeona wasomi wa siku hizi japo si wengi wanapofanikiwa wanakumbuka kurudi nyumbani na kujenga ingawa si kwakiwango kikubwa, na hivyo inabidi tuendelee kuhamasishana ili kila mmoja aone wajibu wake wa kukumbuka kwao.

Kwa sasa niishie hapa, nikipata muda nitachangia sababu nyingine nyingi zilizosababisha kurudi au kuwa nyuma kimaendeleo kwa wilaya yetu ya Serengeti.
 
Last edited by a moderator:
Acheni ukabila maana hapo hakuna zaidi ya ukabila wa mgawanyiko kwani hata mkipata mali hamji kujenga kwenu sasa awajengee nani?
Wanasema Mwalimu alikuwa Rais wa NCHI hii kwa zaidi ya miaka 20. Hakujenga Butiama. Hakujenga uwanja wa ndege. Hakujenga barabara za lami. Na wao hawana pa kuanzia zaidi ya kujenga vibanda ambavyo majeneza yao yatafikia kama hawatazikwa hapa Dar.
 
Back
Top Bottom