Kwa watu wa mkoa wa Mara

[/COLOR]

Nimewasoma. Yote ni heri ila hilo hapo juu la katiba ya ubaguzi wa kuwabagua wasio vijana halitatuvusha! Liangalie upya wewe mwenye katiba yako.
Hayo ni mawazo yako,yaani una maana kuwa na umoja wa vijana ni kubagua wazee?kuna mtu kawakataza kuwa na umoja?kuna uvccm na bavicha, mbona wazee wa ccm na cdm hawajalalamika.Au ulimaanisha nini? au unashauri nini?
 
Mura "SAGANKA" mimi nakuunga mkono 100%. Mimi binafu ni mkurya wa Nyamongo ila nimejenga Bunda. Nipo Bunda huu ni mwaka wa Tatu sasa, nilipo hamia Bunda ndugu na jamaa walikuwa wanasema kukame, hakuna maji, wilaya maskini na mengi mengineyo. Kiukweli naomba niwaeleze kuwa Bunda siyo wilaya masikini hata kidogo na wala siyo kame kama inavyosemekana. Nilijaribu kufanya research ni kwa nini sifa hizi mbaya zinaelekezwa Bunda nikagundua kuwa hii ilikuwa ni propaganda ya watu waliohofia umaarufu wa Bunda kama ingesifiwa ingeliweza kuwa makao makuu ya mkoa wa Mara na kuleta ramani ya maendeleo. Kumbuka Bunda iko katika ya mkoa wa Mara ambapo wilaya zote za mkoa huo zina access nayo, mbuga ya serengeti, ziwa victoria na mengi mengineyo. Natumaini kwa great thinker mtajua nikisema kuwa kama wilaya ya Bunda ingepewa kuwa makao makuu ya mkoa wa mara, leo hii ingeitwa jiji, make uwepo wa mahoteli ya kitarii Arusha ungekuwa na utata pai na vyuo vya utalii na mambo mengine yanayo husu mbuga ya Serengeti. Naomba tutafutane na kuangalia hiyo katiba ya vijana wa mkoa wa Mara ili kuangalia mapungufu yake kabla ya reg. yake. Kwa sasa nipo nje ya mkoa wa Mara ntakuwepo Bunda kuanzia katika ya mwezi wa 11.2012.
Nitafute tata kwenye 0782 577 006 tuongee mustakabari wa mkoa wetu.
 
jamani naona tatizo siyo ukabila ila ni uzalendo kwa hawa viongozi wetu Hebu fikirieni wakati wa PM msuya, Mr mgonja, kwa ufupi waliyowafanyia wachaga wenzao msuya kapeleka Lami hadi marangu cheki Mgonja alivyoiboresha Rombo sie tulikuwa na majenerali wangapi tumewahi kuwa na PM sasa hivi tunao viongozi wangapi wa ngazi za juu ambao wanaushawishi kabisa wawa kuweza kufanya mambo kila m2 akakubali tunae waziri na katibu mkuu wa nishati na madini lakini mkoa wa Mara umeme vijijini ni tatizo tujifunze kwa ngeleja alivyowapatia wana Sengerema umeme vijijini nafikiri Mkoa wa Jimbo maskini kuliko yote ni Jimbo langu la M mwibara jimbo hili jimbo linabahati ya kuwa karibu na mwambao wa ziwa na wakazi wake wakubwa ni wavuvi lakini tatizo ni ubinafsi wa viongozi wetu mikopo itolewayo haina tija kwa wao lakini kungekuwepo uwezekano mabeenki yakawakopesha hawa watu mashine za uvuvi kama wanavyokopeshwa wakulima hizi power tila nafikiri mvuvi angejikomboa lakini wao hilo hawalioni na kuna uwezekano mkubwa sana mabenki kuleta vitu kama hivyo serikali ikaweka mkono wake wavuvi wakapewa hizo mashine lakini tatizo linabaki pale la UBINAFSI wala siyo ukabila kama wengine wanavyoaminiy
 
Post yako nimeisoma na nimeilelewa lakini siyo katika ufahamu ule ambao nilkihitaji kuelewa Napata shida kidogo katika post yako naona kama imeegemea upande wa kisiasa zaidi kwangu mimi naoana kama ni post inayofanana na zile za wanasiasa ambao huzitumia katika kuomba ridhaa ya kuongoza wananchi katika nyanja fulani Sina maana ya kuwa wewe ni mwanasiasa la hasha ila ukweli unaujua wewe binafsi Mimi mwenyewe napata shida kubwa kabisa kuelewa ni kwa nini mkao wetu kila kukicha ndo unazidi kurudi nyuma nilikuwepo mwaka huu baada ya miaka kadhaa kuwa nje ya mkoa lakini yale niliyoyaacha hayapo tena na hakuna dalili ya kurejea tena Hapa suala siyo kumtegemea kongozi ajaye sisi wenyewe ni viongozi hebu fikiria kama kweli mtu unakata miti kwa kuchoma mkaa je hapa kiongozi wa nini na kati anajua ni nini madhara yake hapo baadaye Haya ni maoni yangu tu
 
Mm sio mwana Mara ila nawashauri kitu kimoja, msikubali kuwa Chagga_body guards. Sifa za kijinga zimewatawala.
 
Post yako nimeisoma na nimeilelewa lakini siyo katika ufahamu ule ambao nilkihitaji kuelewa Napata shida kidogo katika post yako naona kama imeegemea upande wa kisiasa zaidi kwangu mimi naoana kama ni post inayofanana na zile za wanasiasa ambao huzitumia katika kuomba ridhaa ya kuongoza wananchi katika nyanja fulani Sina maana ya kuwa wewe ni mwanasiasa la hasha ila ukweli unaujua wewe binafsi Mimi mwenyewe napata shida kubwa kabisa kuelewa ni kwa nini mkao wetu kila kukicha ndo unazidi kurudi nyuma nilikuwepo mwaka huu baada ya miaka kadhaa kuwa nje ya mkoa lakini yale niliyoyaacha hayapo tena na hakuna dalili ya kurejea tena Hapa suala siyo kumtegemea kongozi ajaye sisi wenyewe ni viongozi hebu fikiria kama kweli mtu unakata miti kwa kuchoma mkaa je hapa kiongozi wa nini na kati anajua ni nini madhara yake hapo baadaye Haya ni maoni yangu tu

Jambo lolote linalohusu mustakabari wa watu,huwezi kuliepusha na siasa,au labda hujui maana ya siasa.Siasa ni maisha ya kila siku ya mwanadamu(MAISHA YOTE YAMETAWALIWA NA SIASA),Siasa kama field nyingine ambayo ni ya kweli inafanywa kisayansi.Sikiliza hii stori,wakati nilipokuwa mdogo,kuna bwana mmoja jirani yetu aliitwa Gregory,huyu bwana alikuwa na sifa ya urafi(kupenda kula kupita kiasi),watu wengi wakamchukia sana,akapoteza heshima mbele za watu na watu wote wanaomfahamu wameshindwa kuwapa watoto wao wanobatizwa jina la Gregory,je unafikiri ni kwa sababu ya jina baya au tabia ya mwenye jina?vivyo hivyo kwa siasa,wanasiasa ndo wabovu.Na ndio maana nimekwambia kuwa wanasiasa wametufikisha hapo tulipo na sio siasa.Lakini pia kama jambo hili nitalifanya bila kujali maneno kama yako.Siwezi kuacha nia yangu njema eti kwa sababu tu umesema nimeongea kama wanasiasa.Naomba uniunge mkono tuijenge MARA yetu.
 
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mzee Isdori Shirima aliwahi kuitisha mkutano wa uwekezaji kwenye mkoa ule. Alipohamishwa kila kitu kikapotea. Kwa maoni yangu hata hii TANAPA ilipaswa kujenga makao makuu yake pale Mugumu badala ya Arusha. Mara ina kila kitu lakini watu wake, mh! Wanaoneana wivu, wanabaguana, wanadharauliana, ubinafsi ndio wao.
ni kweli tata makao makuu yanatakiwa kuwa mugumu . by all standards mie sio mbaguzi na Mungu apishie mbali nisiwe mbaguzi lakini kiukweli roho huwa inaniuma sana ninapoona wanaofaidika na mbuga ya serengeti sio wazawa wa serengeti na mkoa wa mara kwa ujumla! anyway the end is near, I can not see the change, but I can smell it!
 
Aksante sana mleta hoja.
Dhamira ya dhati pamoja na kusimamia na kutekeleza dhamira yenyewe ndiyo msingi wa mabaliko.
Vijana wa Mara wanaweza kuleta mabadiliko sana kama wakiamua.
Jambo la kwanza la kuanzia ni kuachana na mambo ya ukabila na ushabiki wake then wafocus kwenye vitu vya maendeleo. Coz hata kwenye huu uzi naona baadhi ya watu wameanza kutiririka kwa kiluga utadhani Mkoa wote wa mara ni wa Kabila moja.
Narudia kusema, Kama mleta hoja na wachangiaji wenye interest na mkoa wa mara wanataka mabadiliko ya kweli
inabidi elements zote za kikabila na kikoo zisiruhusiwe kabisa. then watu waangalie kinachowaunganisha zaidi ndiyo kipewa kipaumbele.
 
Asante bwana ka-rabbit,tupo pamoja sana,kwa mabadiliko tuwasiliane kwa namba 0782577006
 
Ni kweli, mimi pia mzaliwa wa huko tena hapo Mtaa wa Kawawa.Hali ya mkoa si nzuri kihistoria na kiuchumi. Hatuna sababu sana ya kujigawa kijimbo ili tufaidi rasili mali zetu ila kuna haja ya KUBADILIKA kitabia, sifa za kijinga pamoja na kukumbuka kurudi nyumbani.

Sio mpaka upate cheo ndio ukumbuke kurudi nyumbani kama Prof. Mhongo alivyofanya hivi karibuni. Kama wanavyofanya wana-diaspora huko ughaibuni basi kuna haja ya kuwahamasisha wana Mara kuwa na tabia ya kurudi nyumbani, kuwekeza, kujenga pamoja na kushiriki shughuli za maendeleo hata kama si kwa kupitia siasa.

Mimi binafsi nimewahi kuchangua ku-elimisha watoto wa huko home yaani kuwapiga shule.Nimepita na darasa langu la tuition hapo Mkendo Primary na hatimaye Mwalimu wa kawaida hapo Mwembeni Secondary.Huu kwangu ulikuwa mchango pia.

Tabia ya kukatalia Dar na kwinginepo na hatimaye kurudi tukiwa ndani ya sanduku kwa kweli ni fedheha. Tazama viongozi hao uliowataja hawakujenga kwao, hawajui maisha ya kwao na kila wakipita kikazi ni Hotelini na kukimbia mji kisa eti uchawi ama kukwepa kuombwa pesa na ndugu zao walio duni.

Wanafurahia sasa kuonekana wako juu,vyeo,pesa huku kutoa msaada ni kama mbingu na ardhi.Tuache tabia hizi wana MARA.
Tata hiyo umenena kabisa
 
Tata mwitongo sijajua una umri gani,lakini kama mnaweza naomba tuanzishe "MUUNGANO WA VIJANA WA MARA"Usiokuwa na itikadi yoyote kisiasa(maana siasa zimetufikisha tulipo),utakuwa na nguvu,ili vijana watumie fursa za kiuchumi zilizopo kimkoa,kitaifa na hata kimataifa kujijenga kiuchumi,kimaamuzi na kuiokoa mara yetu.Nabhamwe tole bhamura.Kwa kuanza tu nimeandaa katiba ya muungano huo,imebaki kufany reg.na kuiweka hadharani tayari kwa kuomba kuungwa mkono na vijana wa Mkoa wa Mara.
Mkuu naona huu uzi ni WA Muda kidogo lakini bado uko hai. Kweli Mkuu SAGANKA naunga hoja.
 
Similar Discussions

14 Reactions
Reply
Back
Top Bottom