Kwa watu wa mkoa wa Mara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa watu wa mkoa wa Mara

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SAGANKA, Oct 24, 2012.

 1. S

  SAGANKA JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2012
  Joined: Jun 9, 2012
  Messages: 313
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ni matumaini yangu kuwa mpo salama,kwa upande wangu namshukuru Mungu.
  Kwanza kabisa ni-declare interest kwamba mimi ni wa mkoa wa Mara,wilaya ya Serengeti,tarafa ya Ngoreme,kata ya Kenyamonta.

  Nina machache leo ya kuzungumza na wana-Mara wenzangu kuhusu mkoa wetu.

  Mkoa wa mara ulikuwa na kasifa hivi hasa kalikoletwa na mwl nyerere,kwamba baba wa taifa kutoka mara.Zaidi ya hapo tunabaki na sifa za kijinga tu ambazo kimsingi haziujengi mkoa wetu bali kuudidimiza na sisi tunabaki kuchekelea tu huku nyumba inaungua.

  Mji mkuu wa mkoa wa Mara ni Musoma mjini,mtakubaliana nami kuwa mji ule umekuwa kama mtoto aliyesumbuliwa na kwashiakoo kwa muda mrefu,yaani umedumaa,hauna mabadiliko chanya tangu nianze kuwa na ufahamu,bali unakuwa kwa kwenda nyuma.

  Wilaya ya Serengeti na Taarime zimekuwa zikisifika kwa fujo na watu wake eti kuitwa majasiri,hizo ni sifa za kijinga na wanaotuita hivyo wanafanya makusudi kutudumaza kimaendeleo.

  Wilaya ya Serengeti,Musoma vijijini,na Bunda zinaelekea kugeuka jangwa.Wachoma mikaa wamefyeka kupita kiasi,huku watendaji wa serikali wakiwepo tu.Hawana uchungu maana wengi wao ni wa kupita tu,sisi wakudumu ndo tumeamua kujitengenezea jangwa.


  Ujasiri wetu uko wapi kama si ujinga,tuna sehemu kubwa ya ziwa victoria,samaki wanavuliwa,minofu inatolewa,kisha watu wetu wanakula mifupa(mapanki),huo ndio ujasiri.

  Mbuga ya Serengeti kwa asilimia kubwa ipo mkoani Mara,lakini kupata nyama kama kitoweo kwa siku hizi kupitia mbuga ni dhambi ambayo adhabu yake ni kupigwa risasi hadi kufa.Kama mtakumbuka zamani kulikuwa na kipindi fulani kwa mwaka wanaruhusu wananchi kuwinda kwa ajiri ya kitoweo.Hakukua na tatizo,wala hatujawahi kusikia wanyama wamepungua,ilikuwa ecosystem ya kawaida kwani sisi ni sehemu ya mbuga.Mfumo umefutwa,mbuga sasa iko na VIP,ukitaka kutangulia mbele ya haki katiza mbugani.Tumebaki kuangalia tu,wamefika mahali twiga wanabebwa na kupelekwa nje,eti mkoa wa Mara ni majasiri,sifa za kijinga.


  Madini ya dhahabu yapo kwa wingi mkoani Mara,kuna Nyamongo,Buhemba,Park Nyigoti,Majimoto japo kwa uchache.Tunafaidije kama si kusaidia mkoa wa Mara kuwa na takwimu ya juu kwa virusi vya ukimwi na ukimwi(7.8%)
  Eti mkoa wa Mara ni majasiri,sifa za kijinga.


  Mkoa umekosa chuo cha maana cha utalii na Hotel management,vipo vya hovyo tu.Vyuo vya maana vipo Arusha na hivyo waajiriwa wengi wa hotel za mbugani wanatoka Arusha,Mara tunabaki kulalamika tu.Eti sisi ni majasiri,sifa za kijinga hizi.

  Rais analazimisha kupitisha barabara ya lami mbugani kwa maslahi yake binafsi(Kwa sababu ana hotel mbugani),watu wa mkoa wa mara tumenyamaza tu,wakati tunafahamu madhara yake.Eti majasiri,ujinga huu.

  Mbuga ipo kwetu,ukipita barabara ya mbugani unalazimika kulipa ada ya kupita mbugani,kama vile wewe ni mtalii.Huu ni uhuni tunafanyiwa,udau wetu juu ya hii mbuga upo wapi.Kwanini ulazimishwe kukatwa pesa hiyo wakati hukuwa na mpango wa utalii.Eti Mara majasiri.

  Tukiendelea kubweteka na sifa hizi za kijinga kuna wakati utafika Mara itatambulishwa kama sehemu ya Arusha,"AMINI NAWAAMBIENI"

  Waliotufikisha hapa wanajulikana,imefika wakati Mkoa wa Mara kuanzisha muungano wa vijana wa MKOA.Vijana wa Mara wakiwa na sauti moja,wanaweza kupanga vipaumbele vya mkoa,na mwanasiasa yeyote atakaetaka ridhaa yetu aonyeshe nia ya dhati kabisa ya kushughulikia vipaumbele hivyo.Vijana tunaweza kufanya hivyo,lakini pia umefika wakati wa sisi vijana kuufanyia kitu mkoa wetu pamoja na taifa kwa ujumla.

  Nilikuwa naongea na mmoja wa wabunge wa mkoa wa Mara eti anasema mkoa umedhorota kwa sababu vijana wake wengi ni walevi,so what?ana maanisha hakuna mabadiliko?kwanini aliomba uongozi.

  Naomba tupeane maoni juu ya mkoa wetu,tukosoane kwa kujenga na ikiwezekana tuje na harakati mpya za kuujenga mkoa wetu.

  Mods kama kuna madainayoendana na hii ilishatolewa naomba msii-combine,nataka kupata maoni ya wadau
  .
   
 2. Mwitongo

  Mwitongo JF-Expert Member

  #2
  Oct 24, 2012
  Joined: Jan 30, 2009
  Messages: 311
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Mura, Obambiri mahene mura. Tugegehiri. Bonse tuberi kya barisya!

  Mara tuamke. Kweli hata kwetu Majimoto hali ni mbaya kabisa. Kiagata ndo usiseme. juzi tumechimbiwa bwawa la hovyo kabisa kabisa! Wanaume tukalikataa. Sasa tuamke tuuendeleze mkoa wetu. lakini kwa shemeji zangu Majita nao ni bure kabisa. Kuna wasomi-madaktari na maprofesa wasiokuwa na idadi, lakini wote wanajenga Dar, Mwanza, Moshi, Arusha, Dodoma na kadhalika. Wanaogopa kujenga Murangi, Mabui Merafuru, Kinyambwiga hadi Masita (Busekera) kwa sababu ya kuogopa kulogwa. Huu nao ni ujinga mura! tuamke!

  Sasa mkoa una mawaziri wasira, kabaka, makongoro mahanga, muhongo, mkangara; lakini wote bure. Una makatibu wakuu kama yule wa biashara, mifugo, maswi wa madini, na wengine kibao, lakini bure kabisa.

  Mkoa una mkuu wa JKT ambaye ni mzanaki, una Katibu wa Chama Cha Magamba, una Mwanasheria Mkuu (Werema) na Naibu Mwanasheria Mkuu (Masaju); hawa wote hakuna kitu! Una majenertali Kiaro, Waitara, na Musuguri; lakini mambo mabaya kabisa. Wengine ongezeni jamani!
   
 3. N

  Nyalutubwi JF-Expert Member

  #3
  Oct 24, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 572
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Kwa jamaa wa Majita pamoja na uprofesser unahitaji kufanya kazi ya ziada kuwaingiza katika mpango huu.
   
 4. nyamemba

  nyamemba JF-Expert Member

  #4
  Oct 24, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 689
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 60
  umeonyesha njia,tupo pamoja
   
 5. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #5
  Oct 24, 2012
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  kumbe akili unazo mkuu, hawa ndg zetu sijui wana nini! kule jamaa mwanasheria mkuu... usitaje magamba, hapo atakuambia kichwa kazi yake si kufugia..., tuna kila sababu ya kutafakari juu ya mkoa wetu.
   
 6. S

  SAGANKA JF-Expert Member

  #6
  Oct 24, 2012
  Joined: Jun 9, 2012
  Messages: 313
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Tata mwitongo sijajua una umri gani,lakini kama mnaweza naomba tuanzishe "MUUNGANO WA VIJANA WA MARA"Usiokuwa na itikadi yoyote kisiasa(maana siasa zimetufikisha tulipo),utakuwa na nguvu,ili vijana watumie fursa za kiuchumi zilizopo kimkoa,kitaifa na hata kimataifa kujijenga kiuchumi,kimaamuzi na kuiokoa mara yetu.Nabhamwe tole bhamura.Kwa kuanza tu nimeandaa katiba ya muungano huo,imebaki kufany reg.na kuiweka hadharani tayari kwa kuomba kuungwa mkono na vijana wa Mkoa wa Mara.
   
 7. Mihayo

  Mihayo JF-Expert Member

  #7
  Oct 24, 2012
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Wewe umefanya nini mkuu au unalalamika tu, mimi binafsi sipendi watu wanaolalamika tu bila action plan.Ni kweli pana tatizo. Bunda ndo wilaya kwanza kwa umaskini, sasa chukua hatua tuanzie hapo mkuu
   
 8. Majita

  Majita JF-Expert Member

  #8
  Oct 24, 2012
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 606
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Bwana Sigitang'oma.Unakumbuka ule uzi nani kawaloga wajita??
  Anyways,mkoa wa Mara nafikiri kuna tatizo linaloitwa "Nyerere hang over" Hili kwangu naona ni tatizo kubwa sana.Pia Mpango wa sehemu hasa ya kujenga mji wa musoma i mean hapo ulipojengwa pia haukuwa sawasawa.Musoma kama ingejengwa say makutano nafikiri mambo yasingekuwa kama yalivyo.

  Kwa sasa Musoma haiwezi kubadilika zaidi ya ilivyo.Pale "much knows" si haba.Kule majita labda kizazi cha waliozaliwa miaka ya 80 kipite ndo yatatokea mabadiliko kwani dhana ya ukijenga kwenu utalogwa LABDA itakuwa imepotea.

  Namalizia kwa kusema kuwa may be wingi wa makabila na vi-kabila vingi mkoa wa Mara nao linaweza kuwa tatizo.kuna wakati nilikuwa nakaa Bunda lakini ukabila pale ulikuwa unasabisha watu ama kuogopa kufanya mambo ya maendeleo au kuwa na wivu kuwa kabila fulani wakifanya hiki itatokea vile.

  Viongozi wa mkoa wa Mara hawana umoja,period.Fikiria Wassira aliwahi kushitakiana na Warioba, acha wote kuwa wamoja lakini wote ni mtu na shemeji yake kabisa.Hiyo chuki haiwezi kwisha mielele amina.

  Mukama wa CCM wakati akiwa mkurugenzi wa jiji Dar alikuwa akisikia wewe ni Mjita anakaribia kutapika.That's why namalizia kwa kusema "who Bewitched the Yego's"
   
 9. W

  WildCard JF-Expert Member

  #9
  Oct 24, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Mtabaki hivohivo. Ukabila, ukoo zinawatafuna sana. Kokote mliko mnajitambulisha kwa vikabila na viukoo vyenu. Ninyi hamuwezi kuwa wamoja. Nani atawaunganisha? Mongoreme kama mtoa mada akiitwa Mkurya anaona katukanwa wakati mila, desturi hata matambiko ni yaleyale! Mruri au Mukwaya hataki kuitwa Mjita. Msizaki naye sio Mwikizu! Mmegawanyika sana. Vipo vyama vya watu wa Mara hapa Dar na kwingineko lakini vyote vimejengeka kikabila na kiukoo sana. Tarafa kama ile ya Kiagata wote ni Wakurya lakini angalia hata vijiji vyake vilivyojengeka kiukoo! Dhambi hii itaendelea kuwatafuna sana tu.
   
 10. T

  Twigwe Member

  #10
  Oct 24, 2012
  Joined: Apr 11, 2012
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tata, Nawaunga mkono mia kwa mia anzeni ili tufanye kitu pls naomba muwe seriou na hili
   
 11. Majita

  Majita JF-Expert Member

  #11
  Oct 24, 2012
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 606
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Mkuu hapana fikiria Kilimanjaro ni dizaini kama mkoa wa mara,kuna Wakibosho,wamarangu tena wakiraracha,wamachame,wakishimundu sijui wa mwika.Wao wanaenda ,mbalio sana hadi wanabaguana kwa koo.Mbona mambo yao yako sawasawa?
   
 12. apolycaripto

  apolycaripto JF-Expert Member

  #12
  Oct 24, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 636
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Ni kweli, mimi pia mzaliwa wa huko tena hapo Mtaa wa Kawawa.Hali ya mkoa si nzuri kihistoria na kiuchumi. Hatuna sababu sana ya kujigawa kijimbo ili tufaidi rasili mali zetu ila kuna haja ya KUBADILIKA kitabia, sifa za kijinga pamoja na kukumbuka kurudi nyumbani.


  Sio mpaka upate cheo ndio ukumbuke kurudi nyumbani kama Prof. Mhongo alivyofanya hivi karibuni. Kama wanavyofanya wana-diaspora huko ughaibuni basi kuna haja ya kuwahamasisha wana Mara kuwa na tabia ya kurudi nyumbani, kuwekeza, kujenga pamoja na kushiriki shughuli za maendeleo hata kama si kwa kupitia siasa.

  Mimi binafsi nimewahi kuchangua ku-elimisha watoto wa huko home yaani kuwapiga shule.Nimepita na darasa langu la tuition hapo Mkendo Primary na hatimaye Mwalimu wa kawaida hapo Mwembeni Secondary.Huu kwangu ulikuwa mchango pia.

  Tabia ya kukatalia Dar na kwinginepo na hatimaye kurudi tukiwa ndani ya sanduku kwa kweli ni fedheha. Tazama viongozi hao uliowataja hawakujenga kwao, hawajui maisha ya kwao na kila wakipita kikazi ni Hotelini na kukimbia mji kisa eti uchawi ama kukwepa kuombwa pesa na ndugu zao walio duni.

  Wanafurahia sasa kuonekana wako juu,vyeo,pesa huku kutoa msaada ni kama mbingu na ardhi.Tuache tabia hizi wana MARA.
   
 13. n

  nyabhera JF-Expert Member

  #13
  Oct 24, 2012
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 425
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Uzii tu umekaa kikabila... Ok mi Mjita endeleeni.
   
 14. T

  Twigwe Member

  #14
  Oct 24, 2012
  Joined: Apr 11, 2012
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hili nalojambo tata, tutafute jinsi ya kumaliza kwanza, maana mjita anajiona yuko juu, mkurya anajiona yeye ndiye kabisaa, ukija kwa wajaluo ndio usiseme, tofauti zetu ziko dhahiri wala hatufichi kama wachaga wanavyo ficha.Tuamke mula mambo yamebadilika sana and days are running very fast.
   
 15. W

  WildCard JF-Expert Member

  #15
  Oct 24, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Nje ya Kilimanjaro WACHAGGA ni wamoja sana. Hata kwao bado ni wamoja sana. Angalia kwa mfano ilivyo taabu kunywa soda ya Pepsi au maji ya Uhai pale Moshi. Sikiliza pia matangazo ya vifo pale Radio One! Kama ulikuwepo uchaguzi wa mwaka 1995 wakati Mrema anagombea Urais kwa mara ya kwanza utafahamu jinsi WaChagga walivyo wamoja. Mara hakuna kitu kitawaunganisha!
   
 16. Majita

  Majita JF-Expert Member

  #16
  Oct 24, 2012
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 606
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  . wana-diaspora h
  Hapo ni tatizo.Bado hata wale wanaochangia michango haiji Musoma.Niliwahi kuona kikundi ama umoja unaitwa TAUS-Tanzania Adventists in US wakitoa michango iliyoelekewzwa Dar wakati asilimia 80 ya wanachama ni kutoka mkoa wa mara,funny enough hata mwenyekiti wake wakati huo wa michango akiwa ni kutoka mkowa wa mara, hukoo majita B
   
 17. S

  SAGANKA JF-Expert Member

  #17
  Oct 24, 2012
  Joined: Jun 9, 2012
  Messages: 313
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  WildCard umesema jambo muhimu nililosahau,tunawadharau wahaya,lakini hawa jamaa ni wazalendo,wanajenga kwao nyumba nzuri,mjini wanajenga za biashara.Sisi tumekuwa limbukeni mno.Tumebaki kubaguana kikabila,vikabila vyenyewe vidogo,halafu maskini sana,shida tupu.Nimeandaa katiba,nataka nipate reg. ili tuanzishe muungano wa vijana wa Mara,naomba mniunge mkono.
   
 18. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #18
  Oct 24, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ninyi wa Serengeti hata msilalamike! Mnajiponza wenyewe na mapenzi yenu kwa CCM! Mnavuna mnachopanda!
   
 19. S

  SAGANKA JF-Expert Member

  #19
  Oct 24, 2012
  Joined: Jun 9, 2012
  Messages: 313
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kwanini unasema umekaa kikabila?,tusaidiane ili turekebishe,Mara ni yetu yego.
   
 20. Osaka

  Osaka JF-Expert Member

  #20
  Oct 24, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 1,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Kaaazi kweli!
   
Loading...