Kwa wataalamu wa ICT

Kwa wataalamu wa ICT

Prince Luanda

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
3,496
Reaction score
5,341
Nafungua uzi huu kwa masikitiko kwa kidogo ila kwa njia ya swali ambalo linaweza kuwa rahisi kwa wataalamu husika waliotajwa kwenye heading hapo juu.
Hivi ni mbinu gani inatumiwa na mtu kukutengenezea website yenye customized domain na ikawa hewani kabisa kwa mkataba wa mwaka mmoja then baada ya siku au tatu inapotea inakua haiexist kabisa wakati huo pesa unakua umeshamlipa?
Sina lengo la kujifunza aina hii ya utapeli but sijaelewa jinsi niliingizwa mjini kirahisi hivi na website ilishakuwa hewani tayari?narudia tena lengo ni kujifunza ili wengine wasije wakapigwa pesa kama mimi nawasilisha.
 
Mtengenezaj anakuwa na uwezo wa kucontrol website ivo anaweza kuibadili kidogo na kuuza kwa mtu mwengine
 
Hapo ni kama umeeka picha yako kwenye facebook account ya rafiki yako halafu huyo mwenye facebook ameifuta ama kala ban.

Niliona kwenye uzi fulani ulitumia mbongo kwenye hio issue, (nisahihishe kama nimekufananisha)

Hosting nyingi za watanzania ni resseler hosting yaani wanaenda kwenye website kubwa za ughaibuni mfano GoDaddy kisha wananunua package kwa jumla na kuja kuziuza huku rejareja, hivyo website za huyu resseler zinakuwa tied na yeye mwenyewe akizingua asipolipia, akifanya jambo ovu ama tatizo lolote la kuvunja terms za website mama ujue na nyie mlionunua kwake mtapata tabu.

Pia situation nyengine inayowezekana imekukuta ni mtu amekusajilia website trial. Website hosting company mbalimbali wanatoa trial ya siku 3 ama wiki ama mwezi etc, ndani ya huo muda wa trial unaangalia huduma zao ukipenda utanunua na kama hujapenda una cancel huduma. Pengine jamaa ali register kama trial akatengeneza website kisha akakukabidhi, trial ilivyoisha na website yako automatic ikawa canceled na kupote.

Possibility nyengine server ambayo website yako ipo hosted haipo tena online.

Kunatokea nini sasa hivi ukiingia website yako?
 
Mimi sio mbongo....
Umeeleza vizuri sana nimekuelewa lakini wewe ndiye ungekuwa unauza sidhani kama ungemuambia mteja wako haya mambo[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] asante kwa kufunguka mkuu.
Kwa sasa sina access ya dashboard halafu ukivisist website address browser yako itakuambia site can not be reached..
 
Jaribu kufanya hivi
-angalia domain yako kwenye who is uone nani anaimiliki ni wewe au kampuni/mtu mwengine
-jaribu kusearch domain yako kama inamilikiwa na mtu ama ipo free kutumika
 
scenario nyingine inaweza kuwa kuihost site temporary kwenye cloud server. payment policy ya cloud hosting ni tofauti na ya shared hosting(web hosting). cloud hosting ni pay per use. yani wanacharge kwa muda ambao umetumia tu. mfano $0.015 per hour. so mtu anaweza akaihost site temporary kwenye cloud kwa siku kadhaa halafu baada ya hapo akaifuta server aliyohost site.
 
Asante mkuu
 
Back
Top Bottom