Niliwahi kupost hii, baadhi wakabisha na wengine wakaunga mkono..sasa tunazidi kumuona huyu HR ni mtu wa aina gani!! naomba nirudi kupost/kukumbushi hii tena,
***********************************************************
Binafsi nilikuwa simjua vizuri Mh. Hamad Rashid zaidi ya kumsikia juu juu tu kwenye vyombo vya habari. Lakini baada ya kuangalia mdahalo wa ITV kati yake na M. Mbowe nimegundua kuwa Mh Hamad Rashid ni mtu:-
1. Anapenda kutoa sentensi za vitisho. (ana u-dikteta).
Hapo nahisi au siku ile alikuwa hajuia/hana uhakika na anachoongea alitaka tukubaliane naye tu, au alikuwa anapindisha ukweli kwa maslahi binafsi, au hizo sentensi zinatokana na shinikizo flani alilopewa. mfano alirudia rudia "let be seriouse on this"
2. Haijui vizuri katiba ya JMT na kanuni za bunge
Alikaa bungeni zaid ya miaka 15 na alishashika madaraka mbali mbali serikalini. lakini haijui vizuri katiba ya nnchi na kanuni za bunge, kiasi cha kushindwa kujua kutoka bungeni kwa wabunge wa CHADEMA sio kuvunja katiba wala kanuni yoyote ya bunge.
3. Anapenda madaraka.
Yupo tayari kufanya lolote apate madaraka mfano, walifanya malidhiano serikali ya Mh. Mkapa (bila kuwashirikisha wananchi)akateuliwa mbunge, kwa malidhiano hayao hayo w wanataka kuingiza kwenye katiba ya muungano cheo cha Makamu wa Rais wa ZNZ atambuliwe kikatiba (bila kushirikisha wananchi) na Sasa zaid, anataka kuingiza kwenye kanuni za bunge atambulike kama kiongozi wa upinzani mdogo bungeni (Ili aendelee kupata mil 100 na malupulupu mengine).
4. Ana element flani za udini.
Mara ninyi alikuwa akitumia mifano ya udini kujengea hoja. mfano ule wa ndesa, aliungiza hata palipokuwa hapastahili ili tu afikishe ujumbe.
5. Anamchukia Mh. Mbowe kama Mbowe kuliko CHADEMA na upinzani
Sijui kwa sababu amechukua kiti chake au la!
kwa maana, Alioneka mara nyingi akitoa mifano ya kushirikiano na Dr. Slaa ,Ndesa n.k hii ina maana ya kujisafisha juu kutokuwa na mahusiano mazuri na CHADEMA.
6. Anajivunia uzanzibar kuliko utanzania. (ni mmbaguzi)
Kauli zake zinadhihilisha kilcho moyoni mwake.
7. Mpenda sifa za kijinga
Mfano, alisifia mara nyingi kufa kwa watu 45 kwenye kudai katiba ambayo sasa wamengia tkt serikali ya mseto bila kushikisha mwazo ya wananchi hao hao waliomwaga damu, badala yake waliwashirikisha kupiga kura ya serikali ya maseto tu. Hamna hata hatua za kushinikza waliomwaga damu zao wachukuliwe zilizochukuliwa, sijui ndo inawasaidia nini wahenga wao waliadhilika na umwagaji damu, au usaliti!
8. Ana ubinafsi (Anajijali yeye kuliko chama chake/watu wake).
Alikuwa akijisifia yeye kama yeye zaidi ya chama chake na watu wake.
9. Ni kigeu geu / Hana msimamo
Amekuwa akitoa kauli zinazopingana. Kwanza alishasema kwamba Mh.Mbowe hakumualika kuunda kambi ya upinzani, the akasema aliambiwa akakataa kutoka na tofauti za kimisimamo. Hata alipoulizwa aseme ipi ni kauli sahihi aliruka kwa ukali ule ule kwamba "mimi nipo very seriose na kauli zangu". Sijui swali hakuliewa ? alitumia ukali kuficha udhaifu au ndo udikteta?
10. Ana dalili za kifisadi.
Msimamo wake unaonyesha kuegemea upande wenye mslahi binafsi zaidi kuliko maslahi ya Taifa
******************************************************************