Kaka mimi si anti Chadema na sishabikii vyama kwani wao wanatutumia sisi kujinufaisha wao, nina mifano mingi tu hili vuguvugu unaloliona leo la chadema lilishawahi kutokea Kenya kina Mwai Kibaki wakashika madaraka wakati wao walipokuwa wapinzani kama Chadema agenda yao kuu ilikuwa katiba yaani same as here lakini walivyoingia madarakani kilichotokea twakijua kama hujui muulize koffi annan atakuambia na acampo.
Nimesema sisi ndio tunaowatuma wanasiasa wakatuwakilishe kwa maana nyepesi sisi ndio waajiri wao, inabidi kwanza tujitambue nini tunawatuwa ili wafanye yale yenye matakwa yetu na manufaa yetu na si kinyume na hapo.
Angalia vizuri post zangu utaona kuna sehemu nyingi sana nakubaliana na CDM na kiheshimu kama chama cha siasa na nawaheshimu sana viongozi wake na naamini mchango wao utasaidia kuelekea kule tunapotaka Tanzania ifike. Lakini siwezi kunyamaza na kusifia kijinga nikiona kitu ambacho kinaitoa CDM kwenye mstari kwani wakipoteza mwelekeo ile safari yetu itakuja kugeuka ndoto.
Turudi kwenye suala la NCCR, TLP na UDP kuto kuwa vyama vya upinzani, mimi naamini ni vyama vya upinzani ikiwa kosa lao kupeana bashasha na wanaccm na viongozi wa ccm bungeni basi wanakuwa wao ni wasaliti sioni mantiki ya siasa hapa. Hivi unataka kuniambia CDM watakuwa wanawanunia wenzao wa ccm eti tu wao ndio wapinzani wa kweli? Siamini watu makini kama kina Mbowe wanaweza wakawa na mawazo kama yako! Kumbuka kuwa siasa si kununiana ndio maana uliona hata ile picha ya Slaa na Pinda Slaa kakauka kucheka huku akigonga! Ndugu yangu vitendo vingine vinasababisha maneno ya kejili na kuna wengine wana upeo mdogo wa kufikiri wakachukulia zile kejeli ni kweli. Mfano kuna baadhi ya wabunge walisikika wakiwaa mbia wacdm wakati wanatoka naomba ni nukuu "Tumewazoea kukimbia, kwisha, uchoyo, weak politicians, na kwenye posho msije, mnadaiwa na mabenki,"walisikika wabunge wakisema kwa kupiga kelele" wapo watu wataanza kufikiria pengine hizi hoja zinaweza zikawa na ukweli ndani yake
Naomba niishie hapa ila ifike wakati tuvichambue hivi vyama na kuangalia je vinatekeleza malengo yetu au wanatekeleza malengo yao kama wanasiasa?