Kwa wasio na familia tu: Okoa pesa yako, achana na fasheni kuiga iga

CONTROLA

JF-Expert Member
Sep 15, 2019
6,939
22,990
Inaweza isiwe na umuhimu kwako kwa sababu umeshafanya makosa haya lakini naamini kama ungeyafahamu haya kabla ya kuchukua maamuzi uliyofanya nina uhakika leo hii ungekubaliana namimi kwa hiki ninachoenda kukisema.

Siandiki nikiwa kama mtakatifu "hapana" naandika nikiwa kama muathirika mkubwa wa aina ya maisha ambayo nilisha yapitia,sijilaumu kwani najua kila mtu hukosea na kupitia makosa tunapata somo na kubadilika.

acha nirudi kwenye mada

Siku hizi utandawazi umekua mkubwa kiasi kwamba sasa kadri unavyozidi kukua ndivyo na wengine wanavyopotea,kuna kamsemo flani watu huambiana kila mahali "naenda na fasheni bwana" haka ka msemo kanawapoteza vijana wengi hasa wasiojitambua.

kama wewe unajijua hauna familia epuka kufanya/kununua vitu hivi maana kusema la ukweli unapoteza hela yako,huwezi litambua hilo sasa hivi ila kuna siku itafika utakaa utaona kua uli bugi kutumia hela yako vibaya.

usinunue Friji kubwa
achana kabisa na mbwembwe za sjui watakuonaje,achana kabisa na mbwembwe sjui friji hili ndo lina trend,nunua friji dogo la kuweka vitu vdg vdg siku umepka au unataka kupika, sio mbaya hata ukinunua kale ka singo door kanakutosha sana maana hauna familia,hauna vitu vya kusema ujaze ili visiharibike so okoa pesa yako.Achana na friji kubwa "trust me" huo mfriji mkubwa haukufai kama kweli una malengo yako yanayohitaji ubanaji wa matumizi.

usinunue kabati la vyombo
wewe kama utaona najifurahisha shauri ako ila amini nakwambia wewe kama upo singo kabati la vyombo ni upotezaji tu wa pesa yako,unaweka vyombo gani kwenye hilo kabati na unaishi peke ako? nunua trey lako zuri la vyombo panga sahani zako 4,vikombe vyako vi 4 vijiko vyako,bakuli,sufuria zako tatu hv,nk nk vyombo flani vile common ambavyo huwez maliza wiki hujavitumia.

Acha kununua ma set ya hotpot, set za sfuria ndugu yangu unapoteza mahela yako buree ukweli nakwambia tena,kumbuka unaishi peke ako hivi ule msufuria wa kilo 6 unautumia kupikia nini? au ndio unataka uwe kama CONTROLA (usitake kujua naufanyiaga nn ule msufuria)

Usinunue TV inch 40 na kuendelea
Kusema ukweli siku hizi fasheni vijana imehamia hili eneo,mtu anapambana awezavyo hata kwa kukopa ili tu anunue m tv mkubwa au weke chumbaniseblen kwake,kachumba kenyewe haka ka ndugu yangu FUSO alikajenga kwa bajeti s kidogo kapga 10 kwa 10,kikubwa ndio kina 10 kwa 12 halafu mtu anatia m flat tv inch 40, serious!!!

kwanini usinunue ka tv kako simple kwani unakosa nini kwenye ka tv kako ka inch 25, au 27 au 28 kipi utachopungukiwa au wewe una matatizo na tv ndogo? fahamu kwamba TV kubwa zimetengenezwa kwa ajili ya watu wenye sehemu kubwa na wanakaa mbali na tv, sasa wewe kachumba kako hako kadogo inch 40 unaifanyia nn? shtuka ebu.

Usinunue kitanda
Hapa ndugu zangu sikulazimishi ufate ila kwa upande wangu mimi kitanda kwangu hakina nafasi naona ni upotezaji wa hela tu maana kusema ukweli siwezi nunua kitanda saivi nipo singo nitanunua nikishakua na familia (mke)

nikisema sinunui kitanda sio kwamba nalala chini hapana (sina masharti ya mganga) napenda kulala sehemu nzuri tu i mean nina inch 12 yangu nimeilaza juu ya zulia langu zuriiii na pata usingizi mzuri kabisa, nikiongelea kitanda naongelea lile mbao mbao lile (ondoa godoro) so lile ndio kwangu naona kama linanletea kiwingu tu. so kama na wewe unapenda bana matumizi (ungana kuwa mwanachama) kuna utamu bana kulala juu ya godoro bila kitanda,"kuna watu wananielewa" najua sana tu.

Usinunue seti ya makochi
asee katika vitu najutaga maisha yangu yote ni kununua haya mataka taka,nilikoseaga nikatungua set nzima aseee najuta hadi kesho kutwa na bahati mbaya ni kwamba hayauziki si unajua ile unanunua kitu Bei ya juu then ukitaka kuuza mteja anakutajia robo ya bei uliyonunua, unaona kuliko utupe kwa hsara bora yakae hapo kwan yana shda gani ila laiti ningepata mtu akanitonya kama mimi ninavyowatonya leo hii asee nisingeingia mkenge ule.

nilishaenda kwa rafki angu mmoja akanikaribsha seblen kwake jamani tuache masihara ile sebule nilitamani kuwe kwangu,kuna vitu vichache na sebule ina uwazi mzuri hadi raha tulikaa chini kwenye zulia moja nene hiloooo,tumezungukwa na mito everywhere na vistuli flani amaizing navionaga kwenye Tv TU kwakweli nilipenda ile sebule "yes naongelea sebule ya namna hiyo"

achana na hayo makochi ndugu yangu,kwanza unayakalia saa ngapi,unatoka 11 unarudi 5 usiku ukifka unaoga direct chumban hilo koch unakaa saa ngap,wageni unao wakukaa? ukiwa singo hata aje pastor/imamu akiingia lazima ataelewa hii sebule ni ya bachelor.

Ishi kwa malengo
kuambiwa usinunue hiki au usifanye kile kwanza tambua sio sheria wala sio amri na isikufanye uishi kama mtumwa, nyumba yako itakua na vitu vichache lakini hakikisha inakua nzuri na inapendeza machoni mwako wewe mwenyewe, sio kila kitu usinunue then hela hujui inaenda wapi huo ni ujinga ni bora ununue kama unajua huna malengo.

ukiwa singo ni raha sana hasa ukiwa na vitu vichache na vizuri,na sio vizuri tu bali vichache na QUALITY mtu anakuja kwako kila anapogusisha jicho moyo una mruka yani unamuona kbsa "huyu mtu akili yake haipo hapa" yes iwe hivyo sasa ishi maisha flani simple but EXPENSIVE one.

amini nakwambia hayo matv,makabati,mavitanda,mavyombo mengi ukija kuwa na familia hutotaka hata kuyaona yatakua kero machoni mwako,hama hama hizi za nyumba za kupanga hilo kabat utalivunja mpk yani kubali ukatae muda wako wa kuanzisha familia ukifika Hamna hata kimoja utachokitamani uendelee nacho hapo mana utakua umekichoka na pia raha ya mapenzi matamu ni pale mnapokubaliana kitu mkiwa baba na mama mnunue nini cha nyumbani.

Utapanga na mkeo/ mumeo mnunue TV gani,friji gani,gari gani yani hamna raha kama kununua kitu ndani ya nyumba ambacho ni muunganiko wa wazo la mama na baba amini nakwambia kile kitu mtakipenda na kitatunzwa kuliko ukisema ununue leo Tv ambayo mkeo/mume hajui bei wala hajui imetoka wapi,umenunua mkitanda leo tena wadada wa siku hz mavitanda yao ya chuma "maweeeeee" sijui huo mkitanda utamlaza nani.

kama mimi ndio mumeo siku nakuoa nakukuta na huo mkitanda asee utaugawa nakwambia maana sipendi kabisaa,mifano ni mingi maelezo ni mengi hapa tunapeana tips tu za kuokoa hela zinazopotea kwasababu ya iga iga na kwenda na fasheni.. fashen ndio zinawapoteza hizo.

save and invest
 
5. Usinunue kopo la chooni tishu zinakutosha
6. usinunue shuka, unaweza lala na sweta inatosha
7. usiweke pazia, waweza weka mabox dirishani inatosha
8. Usiende gest tumia geto lako inatosha
9. Nunua boksa mbili tu zinatosha kubana matumizi
10. ogea sabuni ya JAMAA Kipande tsh 100 tu
 
Back
Top Bottom