Kwa mliooana kuna siri na siri kuu

Braza Kede

JF-Expert Member
Nov 1, 2012
1,678
3,324
Kuna siri za familia, yes maadam mnaishi kama mume na mke kuna vitu vingi mnashea pamoja. Hivyo vinabaki kuwa siri ndani ya familia na hamsemi kwa wengine.

Lakini kuna siri kuu. Hii ni yako wewe na mungu wako tu ikiwezekana hata mama yako mzazi hajui labda ukifa watakuja kuijua huko bdae ukiwa haupo.

Maana yake sio kila kitu ni cha kumweleza mwenza wako japo mnaishi wote pamoja mnaamka kitanda kimoja wote kila uchwao.

Maana ndoa zenyewe hazieleweki hizi. Hii maana yake nini, kama mkitofautiana huko mbeleni mfano anataka muachane ina maana kama kuna madai ya kugawana vitu kwa mfano, mtagawana vitu anavyovijua yeye tu.

Akisepa kwa mategemeo eti atakupausha, atashangaa wewe hautetereki unasongesha maisha mwendo mdundo tu. Hawa kenge wenyewe hawaeleweki siku hivi. Usimwambie mtu.
 
Back
Top Bottom