Hatupangiani maisha ila ni ushauri tu kuanza mwaka 2024

rejuehan

Member
Dec 19, 2023
10
16
Niwaze kama kichaa

Mshahara total kwa mwezi 350,000/-

Chumba: 70,000×6=420,000/=

Ndani kwake
TV inch 50=750,000/-
Show case =120,000/-
Kitanda =300,000/-
Godoro =250,000/-
Jiko la Gas plate 2=140,000/-
Mtungi wa Gas mkubwa =110,000/-
Oven =160,000/- hadi 200,000/-
Pressure COOKER =130,000/-
Jug la Umeme =16,000/-
Ana Dstv =25,000/- per month
Umeme bill =10,000/- per month

Ukiangalia gharama zote hizi Kwa kijana ambaye hana Familia Ni mzigo Mkubwa ambao kamwe kwa Mshahara wake huu Hawezi kujenga.

Vijana wananunua vitu ambavyo hawana Matumizi navyo Kwa show off mfano Kijana bachelor ana jiko la Gas plate mbili, ana pressure COOKER pia ananunua Oven(Misuse of resources)

Mwisho wa siku Utakuta unatumia Zaidi ya Unachokiingiza utazeeka na utaongeza lawama.

Kijana kama huna familia Nunua vitu vya muhimu pekee tu,

Mfano Gas ni Muhimu nunua
Nunua Vyakula ni muhimu
Nunua Maji ya kunywa ni muhimu
Lipa bill ya Umeme ni muhimu
Usijaze Mavyombo Mengi siyo Muhimu
Godoro ni Muhimu nunua
Kitanda ni option
Kabati la nguo Nunua
Kabati la vyombo siyo muhimu saana
Show case siyo Muhimu kwa kijana wa kiume
TV ni option vijana Mechi wengi tunakwenda Bandani na tuna TV ndani
Oven siyo muhimu Kwa kijana wa kiume
Fridge siyo muhimu saana

Bajeti hela yako ukae Sehemu nzuri kuliko kujaza vitu Ambavyo havina Maana Saana ndani.

Mwisho Kila mmoja ana njia zake za Kuishi Ushauri unaweza kuutumia au ukauacha

Mfano mimi niliiga Maisha Ya Mchina Mmoja ambaye ni Boss wa kampuni Kubwa hapa Mjini ,Siku moja nilikwenda Kwake inshort sikuamini nilichokikuta

Hana Familia hivyo Ana Godoro tu la mtu mmoja lakini Godoro ni kama nchi 15 sijui lile

Anapanga kwenye apartment lakini siyo full finished

Ana mito miwili na viti viwili na meza

Alafu Ukutani kaweka TV yake ya nchi 32 hii siyo (kwaajili ya kucheki movie) amefunga Kamera kwajili ya Kuangalia OFISI zake

Ana jiko la Gas plate mbili hapo anakwambia Mtungi unakaa mpaka miezi 6 ule mkubwa.

Nikamwangalia mtu ambaye anaingiza zaidi ya 500M per month ana Maisha simple kiasi kile inakuwaje Sisi makapuku tunaishi kitajiri??

Kwanini Una mshahara wa 350k per month alafu Unaishi kwa bajeti ya 800k?

HIVI VITU WAACHIE WANAWAKE SISI WANAUME TUISHI KWA MALENGO KAMA MABAHARIA.
 
Title yako "New Member"

Mpangaji mpya(mgeni).....

Umeanza kutupangia namna ya kuishi humu!?..... Wapangaji uliotukuta!

Vipi ukimaliza mwezi!?... Mbona hatutapumua!

Tupunguzie spidi kiongozi!

Kwanza hivi unajua hata funguo ya toilet nani anakaa nayo humu!?
Kupumua lazima mkuu!
Nimeona nianze kuyawaza ya 2024
 
Sijui kwanini umeamua kuwapangia... Ku dream big ni pamoja na kumiliki hivyo vitu...garama zikiwa juu atajiongeza namna ya kupata kipato mbadala.

Hata kama maisha ni magumu acha watu waishi maisha yao.
Wapo ambao wanaweza kuyaishi hayo maisha tena urahisi na wapo ambao kwao ni changamoto ko anaweza kuuchukua kama ushauri ila tisa kumi maamuzi ya mhusika mwenyewe
 
Maisha hayana formula Mkuu....sisemi ulichosema hakina maana....kina maana kubwa tu...ila saa zingine maisha hayana formula.
 
Uko sawa kabisa mkuu.

Kwa mwenye akili timamu ataelewa umemaanisha nini. Ndo maaana wabongo wengi hatuendelei cause tunaishi kwa mashindano na sio uhalisia. Unakuta kijana anaamua kujipa mzigo wa kununua vitu vya gharama ili nayeye aonekane mjanja au anazo. Kumbe hivyo vitu gharama yake jumla ni mtaji tosha amabo angeutumia vizuri ungemfanya aingize zaidi ya hiyo 350k
 
hapo ndio utagundua kuna watu wana mawazo ya kimasikini sana

kumiliki vyombo vyake binafsi anasema si muhimu lakin jioni utamkuta anakunywa konyagi
Friji ni muhimu lakini kwa wakati wake! Baada ya kuona vitu vingine vimeenda kama ulivyokusudia.
 
Uko sawa kabisa mkuu.

Kwa mwenye akili timamu ataelewa umemaanisha nini. Ndo maaana wabongo wengi hatuendelei cause tunaishi kwa mashindano na sio uhalisia. Unakuta kijana anaamua kujipa mzigo wa kununua vitu vya gharama ili nayeye aonekane mjanja au anazo. Kumbe hivyo vitu gharama yake jumla ni mtaji tosha amabo angeutumia vizuri ungemfanya aingize zaidi ya hiyo 350k
Salute!
 
Back
Top Bottom