Kwa wasambazaji/dealers wa viswaswadu

Young fadson

JF-Expert Member
Nov 6, 2017
733
772
Nilalalapo na niamkapo naona biashara pekee itakayoweza nfikisha pale napopataka ni biashara ya simu, idea yangu imejikita zaidi katika uuzaji wa simu ndogo kwa kuanzia, hii ni kutokana na udogo wa kianzio nlichonacho,

Mtaji wangu ni 2M, nmejiandaa kusafiri poli to poli hasa ktk kipindi cha mavuno, lengo ni kuwawezesha wamama wa nyumbani wasioamin ktk kwenda maeneo ya mijini hasa kutafuta zana za mawasiliano (simu)

Mazao kama mpunga, mahindi karanga nk. yatatumika kama mbadala kwa mtu asie na pesa in cash ntachukua kila kitu ilmradi malengo yatimie,

Msaada naouhitaji kwa watu wanaojihusisha na biashara za sim, naweza pata sim ndogo kwa bei gani (bei ya jumla) ili niweze kuandaa business plan yangu kwa kiwango faidishi yaani faida kwa mandishi na vitendo

Kuhusu aina ya simu me si mjuzi lakin kwa dealers waweza nisaidia aina ya simu ndogo pamoja na bei zake

Ikiwezekana unaweza tupia na picha kidogo.
 
Back
Top Bottom