Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

EMPEROR WANG GUHN DRAMA
imenichukua miaka takribani mitatu kuiangalia hii drama and finally usiku wa jana nimeimaliza, drama kama hizi zinaangaliwa zaidi na wale binadamu wabishi, watemi na vichwa maji kama damushin ambao kwa kiasi kikubwa muda wao mkubwa huutumia kwa ajili ya kuangalia televisheni kuliko kufanya kazi mpaka anayaletea athari macho yake aliyopewa na muweza wa yote ulimwenguni.

jumla ya episode 200 na kila episode inachukua wastani wa dakika 48- 53, kilichonivutia ni kwamba 85% ya matukio yalioigizwa humu ndani yamerikodiwa kwenye vitabu vya historia na kwa kuwa washindi walikuwa ni goryeo basi kivyovyote maandishi ya kihistoria yaliorekodiwa yatakuwa upande wa kuisifu Goryeo.
Neno goryeo(koryeo) ndio msingi wa neno korea.
  1. wang gun amezaliwa na kufariki (31 January 877 – 4 July 943)
  2. ni mzaliwa wa shilla lakini chimbuko la ukoo wao ni watu kutoka goguryeo ya zamani, ukoo wao ulikuwa na heshima kubwa sana na utajiri uliotokana zaidi na biashara walizokuwa wakizifanya kwa njia ya bahari.
  3. kwa mujibu wa drama na maandishi ya kihistoria aliwahi kuwepo muhadhiri wa imani ya buddhism aliyeitwa dosun ambaye aliwahi kutabiri ya kwamba wang guhn atakuja kuwa mtawala mwenye nguvu kwenye hizi nchi tatu za baadae (laer goryeo+ later baekje +shilla)
  4. wang guhn alitawala goryeo kwa miaka 25,ndipo madaraka yake yakarithiwa na mtoto wake wa kwanza ambaye ni wang mu lakini alifariki baada ya miaka miwili ya kuwa madarakani
  5. wang guhn alioa wanawake takribani 30, kwa kiasi kikubwa alifunga ndoa zaidi za kisiasa kwa dhumuni la kuunganisha damu dhidi ya koo tofauti ambazo ziliamua kujisalimisha kwa wang guhn.
  6. upande wa pili alikuwepo jamaa anayeitwa gong ye ambaye alizaliwa na mfalme wa shilla lakini kupitia kwa mwanamama amabye ni concubine, huyu jamaa alikutana na mitihani mingi sana uddogoni mwake alipokuwa shilla ikiwemo kupoteza jicho lake na alishuhudia kifo cha mama yake jambo lililopelekea aikimbie nchi yake na kuwa MONK.
  7. Gong yae baadae alipata nguvu kubwa sana na kufanikiwa kuanzisha taifa lake ni kulipa jina la Taebong, ukoo wa wang guhn waliamua kujisalimisha kwa gong yae na hatimaye akapewa cheo cha general, mfalme gong yae alivutiwa sana na wang guhn kiasi ambacho alifikia hatua ya kumtangaza wang guhn kama ni mdogo wake.
  8. miaka ilizidi kusogea huyu jamaa akawa na chembe chembe za kidikteta, miongoni mwa vitendo vyake vya ovyo ni kuisambaratisha familia yake mbele ya hadhara, baadae gong yae akamua kulibadilisha jina la taifa lake kutoka Taebong kuelekea Majin.
  9. mwaka 918 takribani wanajeshi wanne wenye nguvu nchini Taebong waliamua kumfuata wang guhn nyumbani kwake kwa dhumuni la kumshauri ashiriki kwenye kampeni yao ya kutaka kumpindua mfalme gong yae ambaye alikwisha vuka mipaka kwa matendo yake maovu, wang guhn alikataa mpango huo lakini baadae baada ya kubembelezwa na mke wake hatimaye akaongoza kampeni ya kumuondoa madarakani mfalme gong yae kwa njia ya mapinduzi.
  10. mfalme gong yae aliuawa pamoja na wafuasi wake na hatimaye wang guhn akabeba ufalme na kutangaza rasmi utawala wa goryeo(goguryeo mpya).
  11. alikuwepo general aliyeitwa kyu hwon kutoka shilla, huyu general nayeye alifanya mapinduzi kwa kuivamia shilla maeneo ya mujinju na hatimaye baadae akaanzisha taifa lake ambalo ni HUBAEKJE ( baekje mpya)
  12. wenye lugha yao wanadai ya kwamba kama utashindwa kuiongoza familia yako haijalishi wewe ni shujaa unayeogopeka basi pia utashindwa kuiongoza tawala yako kwa amani na ndicho kilichomkuta huyu mfalme.
  13. alitokezea kumpenda sana sana mtoto wake wa mwisho huku akimchukia mnoo mtoto wake wa mwanzoni kupitia kwa mke wa mwanzoni, jamaa aliipa mafanikio makubwa sana hubaekje ikiwemo kampeni yake ya kuivamia shilla na kumuua mfalme wa shilla huku akimweka mfalme mwengine aliyekuwa akiendana na maamuzi yake lakini vita ya familia ilipelekea anguko la nchi yake.
  14. mtoto wake wa kwanza aliitwa shin guhm ambaye aliamua kufanya mapinduzi kwa kumuondoa madarakani baba yake na pia aliamua kumuua ndugu yake wa kambo aliyeitwa keum gang na hatimaye akawa mfalme wa pili baekje.
  15. kyu hwon hatimaye akaamua kukimbilia goryeo ili apate hifadhi kutoka kwa wang guhn ambaye ni adui wake wa muda mfrefu ambaye wameshakutana mara kwa mara vitani, mzee aliona ni bora ajisalimishe kwa wang guhn kuliko kumuunga mtoto wake wa kumzaa awe mfalme.
  16. vita ya mwisho hatimaye hubaekje wakajisalimisha kwa goryeo na baadae shilla pia wakajisalimisha kwa goryeo, bila ya kusahau taifa la balhae ambalo lilianzishwa na general daejoyong kutoka goguryeo nao pia walijisalimisha kwa goryeo.
  17. hawa balhae utawala wao uliangushwa na wahuni wanaoitwa KHITAN, hatimaye goryeo wakafanikiwa kuziunganisha kingdom tatu na wang guhn kupewa heshima ya emperor.
  18. shilla waliziunganisha tawala tatu kwa kutumia msaada zaidi kutoka nchi za kigeni hususani Tang.
  19. wang guhn hakutegemea nguvu za nchi za kigeni kuziunganisha three kingdom za baadae.
maisha ya emperor wang guhn na baadhi ya watoto wake pia yameelezewa kupitia drama zifuatazo
scarlet heart ryeo
shin or go crazy


huyu wang guhn kwa vipindi tofauti alizungukwa na wanadamu wenye akili zaidi kuliko binadamu wengineo kama mimi.

choi ung= aliingia madarakani akiwa na miaka 14 nyakati za utawala wa gong yae, alikuwa ni zaidi ya genius na alifariki akiwa na miaka 35
choi jimong = huyu jamaa alibobea mnoo kwenye elimu ya nyota
View attachment 1098969
Assignment kama hizi unazotoa unadhani lini miye nitaketi na kutazama Drama za mjini?!
 
Kwa Sasahiv hamna drama kaliiii eh?
Natizama Mother of mine dah napenda uhusika wa TJ kwingine naruka ruka, Fiery Priest Yan sio ya kukosea usingizi nilianza Banker naona ina wahusika weng epi. 2 za mwanzo ntairudia tho. Na Waikiki Kuna vitu vinafanana na 1st dah. Au my Mood na Korean iko down kwa sasa
 
teh teh teh lakini mkuu hizi assignment is not compulsory, jisikie huru kuchagua swali ulipendalo.
lakini tu usije ukafuata tabia za punda yule wa juha aliyerudi kwenye mtihani hatimaye kila akiulizwa swali la ngapi umejibu akaishia kusema maswali ni magumu na mengine nimeyasahau majawabu yake.
Nimefanikiwa kuitazama episode 1, inavyoonyesha ni ya 2004-2003,lakini ipo vizuri.
Nimejiongezea Mzigo wakati sijamalizana na Great King na Jeong do jeon
 
Nimefanikiwa kuitazama episode 1, inavyoonyesha ni ya 2004-2003,lakini ipo vizuri.
Nimejiongezea Mzigo wakati sijamalizana na Great King na Jeong do jeon
masahihisho:
mkuu ni ya mwaka 2000 na si 2003/ 2004.
nyakati hizo iligonga rate ya 60% kwa kuangaliwa zaidi nchini korea, si unajua tena ilikuwa ni mwendo wa TV za serikali.:):)
 
  1. mkuu zipo baadhi ya website(tovuti) zimewekwa kitufe cha download kwa mfano ondramanice na mdogo wake dramacool.
  2. zipo nyengine mpaka uwe na special download software mfano IDM.
  3. ondramanice: https://www2.ondramanice.tv/
View attachment 1101750
nimejaribu kuattach IDM setup pamoja cracked file lake ambayo itakuwezesha kutumia bila ya kuletewa ujumbe wa kufanya malipo japokuwa ni makosa (illiegally) lakini sidhani kama inawezekana labda unitumie email yako (barua pepe)

or tembelea link hii upate kupakua setup ya IDM ambayo itakuwezesha kutumia kwa siku 30 bure,
Shukrani sana mkuu kwa taarifa hizi nzuri......bahati nzuri katika kustruggle nimefanikiwa kuweka mambo sawa aiseh....
 
[QUOTE="Daemusin
2020 presidential election
nimesikia kuna timu uchwara zikiongozwa na maembe mabichi, lipumbavu, mzito mwepesi, kitundu kidogo na wengineo wameshaanza vikampeni uchwara kwa dhumuni la kurithi madaraka ya Tanzania Bank.

nimebaki nawacheka muda huu kama katuni ya zootopia, sina haraka ya kuingia uwanjani na mshambuliaji wangu machachari anayevuruga pande zote bila ya kuangalia sura ya adui haijalishi mpinzani ana kichogo, kichwa bapa kama ng'ombe, masikio kama panya n.k

kama walalahoi wa tanzania bank mumechoka kuongezewa interest rate, kama mumechoka kushuhudia benki yenu inatumika kutakatisha fedha chafu za wanasiasa uchwara pamoja na wafanya biashara basi ni muda muafaka wa kumshawishi baadae kumpigia kura auditor noh dae ho kupitia vita ya uraisi.

kwa nini tumchague?
  • kwa sababu ana ndevu kama sefu wa pemba.
  • ana elimu kama alivyo lipumbavu.
  • ana sifa ya kujua kuchanga karata zake kama maembe mabichi.
  • si muoga wala mkurupukaji kama mfungaji aliyesahau kula daku hatimaye akaamka saa 11 za alfajiri huku chipsi kuku zikiwa bado hazijaliwa
  • ukitaka mijadala ya jazba pia anaweza kuliko tundu dogo la kupitishia maji machafu
  • hana sifa za kijinga kama juma soda mzee aliyenunua kunguru 10 wasioliwa.

kama bado munataka kuendelea kutafuta maji ya kuosha nyuso zenu kwa kutembea kilomita 10 kama wehu basi wachagueni wanasiasa uchwara, lakini kama munataka kuyafaidi maisha na kushuhudia.
mgombea pekee asiyekabia( kuchomekea) koti kama alivyofanya mzee hassira
mifereji kutoa maziwa ya kondoo,
umeme wa sauti,
kila mtanzania kumiliki private jet,
kila mtanzania kukoga mara tano kwa siku kama samaki
hatolala na nyinyi mbele wala nyuma kama bwana yule anavyotishia
wanaume wote kubarikiwa nguvu za kiume bila ya kutumia vumbi la unguja
wanawake wajawazito kuacha kula udongo mwekundu kama jongoo (millipedes)
wafugaji wa kimasai wote kumiliki magari ya kupakia ng'ombe zao pindi wanapoelekea mipaka ya nchi nyengine
wachaga wote kutoa michango kwa fedha zao kama mzee regina kidogo (nimemnukuu madaladala).

nawaomba ifikapo october 2020 mumchague auditor noh dae ho kupitia chama cha hatulali na njaa milele.
je kina dada mutampaaaaa
je ma ahjumma wote mutampaaaaaaa
wanaume mutatoaaaaaaaaa japo kwa siriii
nimekusudia kura jamani

team kampeni itaongozwa na damushin bin makinikiyya bin noah bin DED bin korooshooo.
napokea michango kuanzia leo.​
==================================================================================================

hii wiki imekuwa ya furaha sana kiupande wangu kwa sababu kwa mara ya kwanza tokea nianze kufuatilia korean drama kama kumbu kumbu zangu zipo sahihi nimeshuhudia drama mbili zinazoonyeshwa na vituo tofauti kumaliza kwa siku moja.

finally nimemaliza kuangalia the banker drama, hatimaye auditor noh dae ho a.k.a professor assad amefanikiwa kumuangusha president kam sang do ambaye ni raisi aliyedumu kwa muda mrefu kwenye daehan bank.

daebak, ilikuwa ni vita ngumu sana kuliko vita kati ya simba na bwana mtembeza bakora kwa wapinzani wake jimboni (code nyepesi hii)

likizo yangu inakuja muda si mrefu.
ramadhan kareem
View attachment 1101984
[/QUOTE]
huyo mzee wa kushoto bado nina mfaidi huku kama Mfalme 대조( Taejo/tejo) cha kushangaza Yi Bangwon ( 이 방원) ndo anaanza harakati za kuchukua Nchi, Confucious scholar( Ha- ryun) anamfanyia mipango Bangwon, wakati upande wa Pili huku Ha ryun kalazimishwa kujiuzulu na Mfalme 대종( Lee Bangwon) .mbali zaidi Sejong the great ameshika nchi but hana nguvu, mshua wake bado yuko powerful licha ya kujiuzulu.
We acha tu ni uhondo baada ya uhondo, cha kuvutia drama zote hizi mbili zimeshea washiriki kwa asilimia 80. Hata hii niliyoianza ni mulemule.
 
Nimetimiza siku 380 tangu nilipojiunga Jamvini. Majukwaa niliyowahi kubandika nyuzi ni la kimataifa, Intelligence, Hoja mchanganyiko. Since nilipoingia kwenye uzi huu mwezi wa 11, sijawahi kuyatembelea majukwaa mengine.
 
So Ji Sub Writes Heartfelt Letter To Fans Following News Of His Relationship

View attachment 1102044


kuna vishabiki uchwara hawajafurahishwa na habari za bwana so ji sub kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na bidada jo eun jung mwenye miaka 25. dunia hii mwenye haki miliki ya kuwa na mahusiano ya kimapenzi na korean celebrities ni Khantwe noona peke yake jamani na kidogo aminas ahjumma mtarajiwa, sasa mwenzangu na mimi unasaga meno na kuumia kisa lee min ho amemchumbia mwanamke mwenzako

alah! una nini bikiroboto unaugua ugonjwa wa dengue wakati unaishi bara la baridi.
celebrities na wao ni binadamu kama wewe hivyo basi wana haki ya kuchagua wapenzi wanaowapenda wao haijalishi wana sura zisizovutia kama mkate wa yesu.
sioni umuhimu wa bwana so ji sub kuwaomba radhi mashabiki wake​
ni muda muafaka kwa ahjussi mtarajiwa kupata mwenza atakayempa utulifu, miaka 41 bado hajaingia kwenye maisha ya ndoa na anamiliki kila kitu,

sasa mwenzangu na mimi ukipata kielfu 15 chako kwa siku unakimbilia ndoa kwa kauli mbiu "MUNGU ATALETA".
kweli mungu analeta ndio maana damushin chumbani kwake anamiliki mifugo mbali mbali kama vile kunguni, mende, mbu, punda, sungura, kima, nyoka, twiga utadhani mbuga ya wanyama.

wakati wenzangu wanamiliki apartment za ukweli hata nzi hatui
View attachment 1102055

likizo yangu inakaribia
Aigoo sunbaenim, nini mbaya? Sio kwa povu hilo. Kwani huyo binti ana kasoro gani?
 
Kwa wale ambao walikuwa bado wanaitafuta Dae Jo young. Mzigo kamili upo hapa


The_King_Dae_Joyoung02.jpeg


Cc Nifah SPYMATE
 
Back
Top Bottom