Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Kuna ulevi mwingine mbaya sana. Kuna viapo sio vya kuapa kisha ukavivunja vinatesa sana

Saiv nateswa na ongoing tatu
At eighteen
Doctor detective
Rookie historian
sielewi ni sababu ipi inayowafanya wengine muzichukie hizi going on drama, kiupande wangu navutiwa zaidi na drama zinazoendelea kuliko zilizokamilika kwa sababu zinanipunguzia mzigo wa kupoteza muda mwingi wa kuangalia drama.

jana tu ndio nimeangalia final episode ya hotel del luna,
inshaalllah sitoangalia tena drama mpaka ijumaa pindi zitakapotoka episode zote mbili za when the devil calls your name drama.
baadae nasubiri tena jumapili nipate kuangalia episode mbili za mwisho za doctor john drama pamoja na episode ya 13 ya arthdal drama.
kwa ufupi kwa wiki moja naweza kuangalia episode 8 tu za drama nne tofauti.

ndani ya mwaka huu nimepata drama takribani 10 zilizokuwa zipo completed lakini zimenishinda kuzingalia sababu kubwa naziona kama zimeshachuja kiubora.
  • beautiful mind = jang hyuk
  • hyde jekill and me = hyun bin
  • kill me heal me drama = ji sung.
  • protect the boss = ji sung
  • gentleman dignity drama = jang dong gun
  • woman of dignity drama = kim hee sun and kim sun a.
  • the good witch drama = lee da hae, ryu soo young.
  • n.k

ukija kwenye hizi compeleted drama kwa mfano katikati ya mwezi uliopita nilirejea kiporo changu kinachoitwa age of warriors drama kwa sababu nilikuwa sina mission muhimu za kufanya basi ilikuwa kila nikiangalia ule mzuka wa kutaka kufahamu kinachojiri mbeleni ndio unazidi, hatimaye nikajikuta ndani ya siku mbili nimezidownload na kuziangalia episode takribani 30.
 
daah hizo rules kiboko, ngoja nizikopi nikaziapply
 
Nimeipenda Sana hi namalizia ep ya 16 Leo...nitaimiss
 
Ongoing mateso sana kusubiria. Naweza kuvumilia kusubiria isidingo pekee sio vikorea.

Hizo ulizovuta zote hazina mzuka ndio maana zikakushinda.
 
Kwa list hio mwanamke ana matatizo makubwa khaa sio kwa uboss huo.
 
Wadau Nisaidieni series nzuri 5 za mwka 2018/2019 sanasana zi base kwenye genre ya comedy.

Niliipenda sana " The fiery Priest" na mwanadada "Lee Ha-Nui" alinivutia sana ila nilipokuja kumfwata tena kwenye "Please Come Back, Mister" ameniangusha sana. Hivyo nataka niachane nayo, naombeni msaada wa zipi nzuri 18/19
 
Itafute utaipenda Sana Ina episode 51 Ina matukio mengi yenye kuvutia na yenye kugusa maisha yetu.Hii series imenifanya nilie hasa episode za kukaribia mwisho zinauzunisha km una moyo ndogo unaweza kulia.
kwa mara nyengine tena ahsante sana brother kwa hii recommendation.
ila usisahau wakorea wana project nyingi sana hivyo basi sidhani kama itawezekana kuziangalia zote kwa mkupuo.
pia inawezekana project unayoiona wewe ni nzuri pengine kwangu mimi nisivutiwe nayo.

empress ki niliwahi kuiangalia hadi episode 15 nikaiweka kiporo miaka mitatu iliopita,
binafsi si mshabiki mkubwa sana wa mwanadada ha ji won pamoja na ji chang wook ndio maana nilikosa mzuka wa kuiendeleza empress ki drama.
 
Kwanini umkubali ha ji won? kiukwel kwangu huyu dada namkubali ile mbaya kuliko hata waigizaji wengine ila kwa ji Chang wook hata me simpendi
 

Hahaha MAHABA pia ni upofu. Song il gook namuheshimu sana, na niajua uwezo wa juu alionao na nimezicheki drama zake zote, lakini Choi soo Jong, ni bora si tu kwa mapigano na umahiri wake wa kuendesha Farasi, bali anavyokuwa anavyoreact katika hali mbali mbali na kuvaa uhusika wa mtu kiuhalisia, mara ya kwanza nilimuona kupitia drama ya Legend of the Patriots, Dae Joyong, the President, King's Dream, Emperor of the Ocean na Emperor Wang Gun. Pia ubora wa drama siupimi kwa ngumi tu, bali story, ndiyo maana drama yangu bora ya muda wote ni "Dong Yi", kimsingi ni drama isiyokuwa na action/ Martial arts kwa kiasi kikubwa, bali ni uzuri wa story na wahusika walivyobeba uhusika wao na kuwasilisha ujumbe walikuwa wanataka kutufikisha kwa ubora ule ule..

Natokea Pyeongyang.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…