Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Unajua kuhusu hizi dramas tunatofautiana tastes ni vyema kuheshimu za mwenzako kama mimi action sio tastes zangu huwa siwezi kuangalia action dramas mbili consecutively huwa nachoka haraka

Ukienda kule kwenye reviews hata Empress Ki na Defendant kuna watu wanazipa negative reviews hapa ndio utaelewa drama huwa si bora katika macho ya kila mtu as you know binadamu tunatofautiana katika kupenda kitu

Si vyema kuiponda drama waziwazi kila mtu akiishi na tastes zake moyoni haiwezi kutokea kama ya kijana mmoja humu huwa anazua ubishani na akina Dada
Kwa maoni yangu sioni ni vibaya mtu akiponda drama nyingine mwisho wa siku haiathiri chochote kwako as long as ana hoja kupitia hayo mabishano mtu atajua uzuri na ubaya wa hiyo drama it means inampa option nzuri
 
Mzee wa Defendant na The Last shabiki ndakindani wa Ha Ji Won

Wiki hii naangalia Pandora ile Beneath The Paradise i think nilifanya mistake kuiruka hii drama mwaka jana ikiwa ongoing
Me nawapeni vitu vikali nyie mnapuuzia madhara yake ndio hayo unakumbuka shuka kushakucha nakupa na nyingine inaitwa nothing uncovered ya mwaka huu ni completed sasa kazi kwako
 
Me nawapeni vitu vikali nyie mnapuuzia madhara yake ndio hayo unakumbuka shuka kushakucha nakupa na nyingine inaitwa nothing uncovered ya mwaka huu ni completed sasa kazi kwako
Sasa tastes zangu zipo kwa romance na historical,hizo huwa nacheki nikiwa bored
 
Mbona mie nimeweza kudownload hapo hapo kimoi tena ina episode 50 naivuta yote ikiwa mbovu ntakuja kukulalamikia kwa gazeti reeefuu kupita la chawa mwashambwa
Numbisa nimejaribu kwenye kimoitv kudownload inakataa kama unaweza kunipa website nyingine yenye hiyo drama itakuwa vizuri
 
U
Mbona mie nimeweza kudownload hapo hapo kimoi tena ina episode 50 naivuta yote ikiwa mbovu ntakuja kukulalamikia kwa gazeti reeefuu kupita la chawa mwashambwa
Unatumia app ipi kudownload? Me kila nikifika kwenye getting ready unabonyeza vizuri unaambiwa timeout
 
Habari ndugu zangu.

Leo nawajuza kuna drama inaitwa MONSTER ni ya 2016 inajumla ya episodes 50 ni drama kali kama mnavyonijua napenda story kali na zenye matukio yakuvutia inayomfanya mtazamaji awe na shauku yakufuatilia kila episode inapoisha na hii drama inahiyo sifa.Hii drama haichagui kabila, rangi au kipato yoyote yule anaweza kuicheki naakaburudika.

Tuje sasa kwenye drama yenyewe inamuhusu kijana mmoja ambaye nikipofu kwenye familia ya kitajiri, kwenye hiyo familia kuna competition ya kurithi Mali kuna jamaa atawaua familia wa huyo dogo ili iwe rahisi kuchukua Mali na kweli anafanikisha na dogo anakuomba masikini. Bahati nzuri anakuja kusaidiwa na organisation moja ambayo inamuahidi itamfanyia surgery na itamsaidia Kwenye kulipa kisasi but kwa makubaliano maalumu kwenye jamaa wanamsaidia rasmi anaingia kwenye ulingo jambo la kwanza ataingiaje kwenye hiyo tahasisi ambaye kuna mbaya wake, jambo la pili nikuwin trust ya huyo jamaa ili iwe rahisi yeye kulipa kisasi wakati huo huo huyo mbaya wake anataka kumweka mtoto wa nje wa kiongozi mkuu na mmiliki wa hiyo tahasisi nafasi ya Vice President ili iwe rahisi kumcontrol na kumsaidia kutimiza malengo yake na pia mtoto wa nje pia ana malengo yake binafsi, movie ndio inaanzia hapa kuwa tamu huko ilikuwa trailer tu.
Numbisa
Intelligent businessman
 
Natumia UC browser ipo playstore hata chrome inakubali pia
Asante sana vipi umeanza kuicheki? me nipo episode ya 27 yaani ni tamu sana aisee alafu haina hata promo alafu kali kiasi hichi.Najua unapenda genre ya Romance humo ipo yaani in short ipo full package
 
Bado sijaanza kuangalia ila nimeshaidownload yote. Saiv Nipo na knight flower
Asante sana vipi umeanza kuicheki? me nipo episode ya 27 yaani ni tamu sana aisee alafu haina hata promo alafu kali kiasi hichi.Najua unapenda genre ya Romance humo ipo yaani in short ipo full package
 
Back
Top Bottom