Kwa wapenda Electronics design na electronics kwa ujumla

Transistor

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
970
1,461
Habari wakuu

Leo ningependa kuongea na wadau ambao wanapenda kufanya electronics.

Tufahamu kuwa technolojia inakuwa kila siku kwa speed kubwa sana lakini..

kitu kizuri ni kwamba katika kanuni zetu za kielectronics hakuna kinacho badilika.

Ila kitu kibaya ni kuwa kuna ongezeko la matumizi makubwa ya Intergrated Circuit (IC) katika teknolojia ya vifaa vya sasa vya kielectronics.

Kwanini nasema kibaya sababu vijana wengi wanaoingia katika kujifunza electronics wanaanza na separates circuits na matumizi ya individaul divices kama vile capacitor,resistor diode n.k vyote hivi vilikua peke ake peke ake.

Lakini sasa hivi kutokana na kukua kwa tekinolojia mifumo imebadilika sana sababu IC moja inaweza ikabeba circuit ndogondogo zaidi ya 1000 ndani ya kitu kisichozidi sentimiter 3.

Na ubaya ni kwamba vitabu vingi vya kielectronics viliandikwa kipindi ambacho mifumo hii mipya ilikua bado.

Hivyo kwa wataalamu wachanga inawawia vigumu kuja kufanya electronics yenye tija katika ulimwengu wa sasa kama hawajui mifumo ya utendaji kazi wa hizi IC mpya.

Kitu kingine ifahamike kuwa electronics ya sasa kwa asilimia kubwa imekuwa computerized nikiwa na maana matumizi makubwa ya logics circuits mfano flip flop zimesababisha kutengenezwa kwa mifumo complex zaidi ambayo haihitaji vitu vingi sababu matumizi ya vitu hivyo yanasaidia kufanya matendo ambayo yalio katika kumbukumbu za speed ya bits zaidi kuliko vifaa harisi.

Mfano wa vifaa hivyo ni micro-processors

Na zaidi matumizi ya vifaa kama hivi kwa sasa yamefanya iwe raisi kubadili matendo ya kielectronics kwa urahisi a speed zaidi sababu badala vifaa hivi vipokee taarifa za kielectronics kutoka katika circuits flani sasa hivi vifaa hivi vinaweza kuamua matendo kutokana na lugha ya kicompyuta mbayo unaweza ukaiandika na uka ifeed katika kifaa na kikafanya maamuzi kama ulivyo taka.

NINI CHA KUFANYA.

Wapenda electronics tupende kujifunza mambo mapya ya kila siku ili tuweze kubadilika katika ufahamu wetu na uundaji wa vifaa vyetu.

Baada ya kubobea katika individual circuit pia Tuthubutu kuanza kutumia hizi IC mpya ili kupunguza nguvu nyingi na kuboresha vifaa tunavyo viunda.

Tujikite zaidi katika electronics design sababu kwa mifumo hii mipya vifaa vingi vitakua havitengenezeki kirahisi na tutapoteza ajira.

Sababu lengo la hawa jamaa ni kifaa kikiharibika kikanunuliwe kingine siyo kitengenezwe.

FURSA KWA TEKNOLOJIA HII MPYA KWETU.

Kwa uwepo wa IC hizi sasa inakuwa rahisi zaidi kwetu kubuni vitu mbalimbali kwa urahisi na matumizi machache ya vifaa,lakini pia unaweza kudesign kitu ambacho ni complex katika eneo dogo kabisa.

Kuunda vifaa vinavyotumia umeme kidogo,fahamu kuwa uboredhaji wa vifaa vya kielectronics pia umejikita kuhakikisha unaunda IC ambazo zinatumia umeme kidogo kabisa na usionyonya zaidi battery.

MSINGI WA ELECTRONICS.

Msingi mkuu wa electronics ni kujua unafanya nini na kifaa flani kinafanya kazi gani.

Epuka kuiga michoro ya watu wengine jitahidi ujifunze uchore michoro yako ni kitu rahisi kama ukiamua.

Lakimi hili hautaliweza kama hutajua kazi na matumizi ya kila kifaa cha kielectronics.

Hakuna kifaa kisicho na umuhimu hakikisha unafahamu kila kitu kinafanyaje kazi na kwanini na kikiunganishwa na kingine cha aina flani nini kinatokea.

Tuepuke shortcut kama kweli tunataka kuwa expert wa electronics.

kwa watu wanao kimbilia kutumia microprocessor na ARDUINO bila kujikita katika kujifunza vifaa vinavyounda mifumo ya hizo ARDUINO na hizo microprocessor wanajidanganya.

Mimi binafsi hua nawafananisha wanao tumia arduino kuunda circuit za electronics na wale wanao tumia software kuunda website wakati hata coding hawajui siku website ikipata shida hawajui wapi pa kuanzia.

Hivyo si vibaya kutumia vifaa hivyo ila kwa mwanafunzi unakua unajichelewesha hakunaga shortcurt katika kufikia utaalamu flani.

Mi nawashauri tujikite katika kufahamu basic circuits,basic parts kila kitu kinavyofanya kazi hii itasaidia hata kama utatumia mchoro wa mtu mwingine utaweza kuu-advance au kuupunguza.

Bila hivyo tutabakia kukariri michoro ya watu tunashindwa hata kuongeza ama kupunguza kitu.

ELECTRONICS NA AJIRA.
Ukifahamu electronics vyema utaweza kubuni kitu chako,au ukadesign kitu ambacho kinatatua shida flani katika jamii bila ku google michoro.

Hivyo ili uweze kuona electronics ina tija ya kiuchumi kwako hakikisha unaweza kubuni kitu chako,ambacho kinatija katika jamii inayo kuzunguuka.

Jamii yetu ina matatizo mengi na kati ya hayo electronics inaweza kuyasolve.

NINI CHA KUDESIGN KIKUPE PESA.

Angalia jamii yako inakabiliwa na tatizo gani,na angalia kama hilo tatizo linaweza kuwa solved electronically kama linaweza kuwa solve basi andaa idea yako kaa chini andaa saketi yako unda kifaa kitakacho solve hilo tatizo.

Ukiunda kifaa hiko mpe mwanajamii mmoja akitumie kusolve hilo tatizo wengine wakiona watahitaji basi hapo utapata soko tena soko la kifaa chako tu.

Hivyo ili kuweza kukuza uchumi kupitia electronics ni lazima tuwe zaidi ya mafundi tuwe wabunifu na hili litawezekana kama tutajitahidi kujifunza na mwisho wa siku tutabobea katika sekta hii ya kielectronics.

Naomba kwa leo niishie hapo

Kwa ,practical na theory za electronics aina yoyote karibu tuwasiliane

Pia kama una project yako unataka msaada tuwasiliane.

Kwa ubunifu wa kitu chochote au idea yoyote tuwasiliane

Mawazo na ushauri pia tuwasiliane

WHATSUP 0629068815

Kama una swali au chochote angusha hapa chini katika comments tujadiliane.
 
Nina kinanda changu nilikuwa nakisafisha baada ya kumaliza baadhi ya batan hazipigi.
Shida nini?
 
Mkuu Transistor binafsi natamani sana kufahamu utendaji kazi wa vifaa katika SIMU.
Mfano Ic's zake zinafanyaje kazi na njia zake.

ROM,Ram,Jina lako,

Achana maelezo ya kina Santos.

Nimekufuatilia sana wewe ni mwalimu mzuri ambaye MTU asiyesomea chochote kuhusu umeme ni rahisi kukuelewa hasa kwa kuwa unatumia kiswahili na kwa mifano

Vipi waweze leta somo kuhusu UTENDAJI KAZI WA SIMU.
 
Poa bosi sawa nitaanda chapisho moja murua na nitalichapa hapa

Hizo ROM sijui RAM ni advance digital system hasa katika kutunzaji wa taarifa za kielectronics na kuzichata.

Yaani ukilifahamu chanzo cha vifaa hivi ambavyo ni complet utashangaa.

Mfano RAM inaundwa na tudude flani hivi ambato wengi wamevisoma vinaitwa flip flop

Humo ndani wameweka logic gates katika kutunza kumbukumbu za tendo flani na ujue kielectronics matendo yanatunzwa na kitu kitaalamu kinaitwa BIT nso mana unakitu kinaitwa Megabites Gigabites Telabites

Hivi ni vipimo vya uwezo wa vifaa hivyo katika kutunza kumbukumbu katika mfumo wa bit.

Hivyo vitu vidogo vidogo wakaviunda kwa wingi ndo vikatengeneza IC.

Hizi IC ndo zimesaidia hata maumbile ya vifaa vya electronics siku hizi yakawa madogo.

Unajua bila IC simu yako ingekuwa kubwa sawa na ukubwa wa gari la YOUTONG
 
Ntashukuru nakusubiri sana

Nimeipenda hii
Hongera Bro
 
Huwa naiona Eletronics kama ni uchawi fulani hivi, leo nimeiona IC ambayo inafanya rectification...
 
Mkuu Transistor binafsi natamani sana kufahamu utendaji kazi wa vifaa katika SIMU.
Mfano Ic's zake zinafanyaje kazi na njia zake.

ROM,Ram,Jina lako,

Achana maelezo ya kina Santos.

Nimekufuatilia sana wewe ni mwalimu mzuri ambaye MTU asiyesomea chochote kuhusu umeme ni rahisi kukuelewa hasa kwa kuwa unatumia kiswahili na kwa mifano

Vipi waweze leta somo kuhusu UTENDAJI KAZI WA SIMU.
Tatizo la watanzania wengi ni wavivu wa kusoma siyo vitabu tu na hata magazeti. Tatizo la pili kubwa tunapenda siasa katika kila kitu. Tunang'ang'anua kiswahili katika kila kitu. Ni vitabu vingapi vya electronics vimeandikwa kwa kiswahili? Hakuna. Tatizo lingine hata bookshops zetu hazina vitabu vya maana vya teknolojia.

Kuna vitabu vingi sana free kwenye internet. Lakini vingi ni vya kiingereza. Google chochote kwenye internet 9 out if 10 utapata. Usipende kutafuniwa kila kitu. Tumia muda wako kidogo kufanya utafiti.

Ukitumua hata 10% ya muda wako ambao unatumia kwa mambo ya umbea utashangaa matokeo yake.
 
Back
Top Bottom