Jiwe Linaloishi
JF-Expert Member
- May 24, 2008
- 3,736
- 2,139
Mimi huwa nashangaa wanawakewanaowapa waume za watu mapenzi
hao wake zao ni wa nini? K
wanandoa, ebu tuelezane ukweli hapa, hivi ni kwa lipi hasa linatufanya baadhi yetu tuwe tunatoka nje ya ndoa zetu ilhali tuna wenza wetu tunaowapenda kwa dhati? hivi ina maana pale mnapofunga ndoa mmoja wenu huwa anadanganya au anajaribu ndoa au? tunaweka mazingira yasiyovutia hasa kwa wale wasio kwenye ndoa kutotamani kuingia huko kwa kuwa kila kukicha wanachokisikia kuhusu ndoa ni bad news. jamani karibuni tujuzane ni kwa nini hali hii imekithiri sana siku hizi, na ni namna gani tutajaribu kuelimishana ili basi tuachane na mambo hayo na kuheshimu ndoa zetu.
nawasilisha.
Kubwa zaidi ni tamaa na kutokuwajibika ipasavyo ndani ya ndoa. Wengi tulio ndani ya ndoa tunajisahau sana na kukosa ubunifu ...
hili nalo neno...pia naona ni kuzoeana kutokana na kutokuwa wabunifu katika suala zima la mapenzi na kulinda ndoa na kila mmoja kuwa commited na uhusiano huo..duh, sasa suluhu sijui ni gani maana changamoto ni nyingi sana!
Mtasema mengi...na theory kibao lakini nature ina baki pale pale u cant fight it.
mke mmoja mme mmoja mpaka kifo kiwatenganishe haitekelezeki.
na ukijua kuwa kuambiana na kuelekezana ni kuzuri kamwe hutataka kutoka nje maana hakuna mkamilifu. na hicho unachopata huko nje ukikipata nyumbani utafurahi zaidi, hakuna asiyefundishika si mwannaume wala mwanamke. ndoa ni tamu na ndoa ni chungu kama tu nyinyi wawili hamtajua namna ya kuishi changamoto za kawaida zipo. ila sababu ya kutoka nje kwa visingizio hivi si nzuri.ni kweli iron lady
kwangu mimi hii ishatokea sana,na nishaongea nae sana
atleast now mambo yanaenda vizuri
sasa si tunaambiana hali halisi?
hahahah wake zetu wanakuwa wasumbufu kama tigo ilivyozingua leo kama huna mbada kimeo... tigo zingua unatulia na zain presha inapungu.. unaendelea kuwa hewa!! (kwa mwanaume unaendelea kuwa active)
naomba kukiwa na ile get together ya jf dar uje tushauriane kwa pamoja na kwa mapanasasa kama unafananisha wanawake na mitandao huna haja ya kuoa maana kuona ni kujifunga huo uhuru wa kubadilibadili ulishatoka pale uliposema ni huyu tu. usioe kaa tu uwe huru ubadilibadili kama mitandao ya simu.
halafu kiongozi, hata sisi wanawake ukituuliza nasi tunasema kuwa nyinyi ni wasumbufu sana tunawavumilia tu. somo hapa ni kujuana na kuvumiliana na kurekebishana.
Lara one, unafurahishaga sn kama kweli vile, lkn kuna kaukweli ndani yake.THE LAW OF DIMINISHING MARGINAL UTILITY!!!!!!!!! Baaaaaaaaaaaaaassss!
naomba kukiwa na ile get together ya jf dar uje tushauriane kwa pamoja na kwa mapana
Nilipobold umenena ila kuna wengine wagumu...[/QUOTE]
kadri mnavyoishi utamlainisha tu kdri unavyojua weakness zake na strength zake utajua wapi pakumpatia na hapohapo ndio utatumia kumbadilisha kumfundisha nakumuelekeza. mwisho mtaendana tu. ni kweli ni ngumu lakini inawezekana.
Fanyeni mabadiliko upande wenu na haya yote yataisha.
Wamama wetu waliwezaje unakuta mama yupo bize ana watoto nyumbani kama 6 na anaenda shambani kulima kama baba anavyolima akirudi anaanza kutwanga mpunga hadi unakuwa mchele. Na bado ana keep ndoa yake intact miaka inakwenda. Lakini siku hizi mkishakuwa bize kidogo tu baaas housegirl anakuwa in charge...
na ukijua kuwa kuambiana na kuelekezana ni kuzuri kamwe hutataka kutoka nje maana hakuna mkamilifu. na hicho unachopata huko nje ukikipata nyumbani utafurahi zaidi, hakuna asiyefundishika si mwannaume wala mwanamke. ndoa ni tamu na ndoa ni chungu kama tu nyinyi wawili hamtajua namna ya kuishi changamoto za kawaida zipo. ila sababu ya kutoka nje kwa visingizio hivi si nzuri.
tujifunze kufundishana na kukubaliana na kukamilishana maisha yataenda na ndoa itastawi.