Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,064
- 22,757
Maxence Melo: Wamiliki wa JamiiForums (JF) ni Watanzania wanaoitumia.
Naam, wanaoimiliki na kuitumia JamiiForums ni Watanzania wanaoisimamia katika mfumo wa uendeshaji wa jumla...JF haiendeshwi na mtu moja. Maxence Melo si mwanzilishi pekee wala mmiliki pekee wa Jf na ndiyo sababu, pamoja na yeye kushikiliwa na Jeshi la Polisi, tupo tunaendeleza mapambano.JF ni jukwaa la habari, jukwaa la mijadala na jukwaa la elimu, zote kwa pamoja, na kwa sababu hiyo inawagusa Watanzania wote kwa namna moja ama nyingine. JF ni jukwaa huru na mtu yeyote mwenye umri usiopungua miaka 18 yuko huru kujiunga bila usumbufu na kufyonza elimu itolewayo.
JF ni jukwaa ambapo koleo huitwa kwa jina lake na nyani ngeledi hukomwa bila kumtizama uso wake. Vita iliyotangazwa dhidi ya JF ni vita dhidi yetu Watanzania. Watawala wa nchi hii wameamua kutuziba midomo tusihoji tulikotoka, tuliko na tunakoelekea. Uhuru wa maoni uko hatarini kutoweka.
Hapana, hatukubali. Tukisalimu amri kwa vitendo vya hawa walevi wa madaraka, tumekwisha na hatutakuwa na nchi. Uhuru wa kujieleza ni haki na wajibu wa kila mwananchi ndani ya taifa hili. JamiiForums kimekuwa chombo pekee mbadala pale vyombo vingine vya habari vilipokubali kutumika kuficha ukweli.
[HASHTAG]#freemanxencemelo[/HASHTAG] now!
Herbert Hoover: Every dictator has climbed to power on the ladder of free speech. Immediately on attaining power each dictator has suppressed all free speech except his own.
Kila dikteta alipanda madarakani kupitia ngazi ya uhuru wa kujieleza. Mara baada ya kutwaa madaraka kila dikteta amekandamiza uhuru wa watu kujieleza isipokuwa wake mwenyewe.