Well ukisema hivyo napata point yako na taratibu naanza kukuelewa.
Kama kalazimisha mwenyewe tena kwa nia mbaya then nakosa jinsi ya kumtetea. Good luck xfactor ila hakikisha kwamba hulindi ndoa yako ukasahau kumlinda mtoto.
Kwa nini unapendelea hivyo?
Kwasababu mama ana uchungu sana na mtoto kuliko mama wa kambo. Wapo mama wa kambo ambao wana roho nzuri lkn hawezi kuwa na uchungu sawa na mama mtoto.Pia Mara nyingi ni ngumu kwa baba wa kambo kunyanyasa mtoto kuliko mama wa kambo.
Lingine ni kwamba akiishi na mama yake hizi complication ambazo mleta mada kazipata zinakuwa zimepungua kwa kiasi kikubwa
Sometimes inabidi wachangiaji tuwe extrimist tuu no way out!
Baba ndio kichwa cha nyumba hakuna mwingine wa kumpangia ratiba wala cha kufanya
Ukiwa umezaa kabla ya ndoa iwe bahati mbaya au makusudi kaa tayari kwa mitatizo kama hii
Huwezi kupanda mchongoma ukavuna bolibo
Am out!
kwa wanaume wetu hawa, mi nafikiri mwanamke ukishaamua kuzaa unatakiwa ujue majukumu ya mtoto ni yako kwa asilimia kubwa sana whether umeolewa or not. huyo mama mtoto alifanya kosa kumuacha mwanae akalelewe na mwanamke mwingine wakati yeye yupo. apart from kukataliwa kwenda kuona mwanao, huna hakika na malezi ya huyo mke mwenzio. Wanaume hawalei watoto,kina mama ndio tunalea. Mtoto anaweza kuwa anapitia magumu bila wewe kujua.Hilo la kuhakikisha mtoto hanyanyaswi ni jema, ni vizuri una uhakikisha hilo. Lakini bado hutumii busara wala haki kusema mtoto asiende kwa mama yake kamwe. Kama ulijua ulozaa nae sio mwema kwanini ulizaa nae on the first place. Ungesubiri ukazaa na ambae ni mke wako ili kusiwe na mtafaruku wa aina yoyote ile.
Aisee!
Wengine tunapenda kuwa na watoto wetu 24/7 365.
Na kuwa mtu ambaye hawatendei vizuri haiwezekani kabisa.
Huyo mke wako ana visa kupitiliza.
Kwanini usimrudishe huyo mtoto kwa mama yake ukatoa hela ya matumizi huko?!Kuna sababu yoyote ya msingi inayozuia mtoto kuishi na mama yake?! Mwanzo kabla hujaoa kulikuwa na utaratibu gani kuhusiana na malezi ya mtoto?! Ni sababu zipi zilipelekea umchukue mtoto baada ya kuoa na sio kabla?! Mke wako anam-treat vipi huyo mtoto?!
Anaenyanyaswa KWELI hapo ni mama mtoto na mtoto wala sio huyo mkeo. Fanya umtendee haki mtoto na mama yake pia. Usisombwe na ubinafsi + visa vya mkeo ambavyo vinaonekana havina logic.
Simuachii mwanangu mwanaume. Sitaki mwanangu alelewe na mama wa kambo.
Na hata akigoma kulea poa tu, nitalea mwenyewe!!!
Niliwahi kuishi na bro wangu pale Arusha miaka ya 2006, yeye kabla ya kufunga ndoa na mkewe tayari alikwishazaa nje watoto wa3, wakike yupo kateshi, wakike yupo mbulu na wakiume yupo kisongo ila hakuwa amemwambia mkewe.
Alipoamua kufunga ndoa mke wake wa sasa aliyezaa naye watoto wawili aliamua kutest zali la kumweleza mkewe na kwenda kumchukua yule mtoto wa kiume pale kisongo akiwa darasa la nne na kuja kuishi naye ngusero akisoma s/m sokoni one.
Maskini mtoto alinyanyaswa na kuteswa na yule shemeji mpaka huruma, akampa marufuku mama yake kuja kumwona pale nyumbani, shuleni wala kanisani au hata kuongea kwa simu.
Mtoto akawa anajaribu kutoroka kwenda kwa mama yake anakaa huko wk 2 basi akirudi pale home atasemwa na kusingiziwa kuwa katoka kuchukua madawa ya uchawi ya kumuua yule shemeji ili mama yake arudie ndoa na yule mtoto atanyolewa nywele zote za kichwani, kwapani mpaka matako.ni ili atolewe huo uchawi.
Hayo yalikuwa yanafanywa na shem bila bro kujua na kale katoto kalikuwa hakasemi ila alipokuja kugundua akaamua kumhamisha shule na kumpeleka kwa bibi yake huko songea ndo ikawa pona ya yule mtoto.
Baadhi ya wanawake ni makatili sana kwa watoto ambao sio wao na akipata mwanya wa kumfanya atakacho anamfanya kweli huyo mtoto.
Hutaki mwanao alelewe na mama wa kambo, sawa.
Je, huna tatizo akilelewa na baba wa kambo?
........Akilelewa na baba wa kambo is okay, sababu mimi nitakuwa naye mwanangu muda wote.
Na baba wa kambo akishanipenda mimi, basi atampenda na mwanangu. Wanaume wengi hawanaga tatizo na watoto wa kambo kama wanawake.
Aisee! Mi nilidhani kiasili wanawake ni watu wenye upendo sana.
Sasa kama hivyo ni kweli, iweje wawe na tatizo na watoto wao wa kufikia?
Na je, wewe unaweza ukalea mtoto wa kambo?
Au katika kusema kwako kwamba huwezi kumwacha mwanao alelewe na mama wa kambo umejitumia mwenyewe kama kipimo cha jinsi mwanao atakavyolelewa kwa kujiangalia na kuona kama na wewe unaweza kulea mtoto wa kambo au la?
Aisee! Mi nilidhani kiasili wanawake ni watu wenye upendo sana.
Sasa kama hivyo ni kweli, iweje wawe na tatizo na watoto wao wa kufikia?
Na je, wewe unaweza ukalea mtoto wa kambo?
Au katika kusema kwako kwamba huwezi kumwacha mwanao alelewe na mama wa kambo umejitumia mwenyewe kama kipimo cha jinsi mwanao atakavyolelewa kwa kujiangalia na kuona kama na wewe unaweza kulea mtoto wa kambo au la?
Ishu ni mbili hapo mkuu,Hata kama yeye hana tatizo kulea mtoto wa mwanamke mwenzie
1. Mama wa kambo Hata kama atakuwa ni mzuri na muelewa lakni hawezi kuwa zaidi ya mama wa mtoto
2. Sisi wanaume hatuna hizi habari za kunyanyasa watoto wa kambo. Tuna mambo mengi hivyo hatuna michongo ya kuanza kummind mtoto. Ndio maana bora mtoto alelewe na baba wa kambo(alelewe na mama yake) kuliko na mama wa kambo
Ishu ni mbili hapo mkuu,Hata kama yeye hana tatizo kulea mtoto wa mwanamke mwenzie
1. Mama wa kambo Hata kama atakuwa ni mzuri na muelewa lakni hawezi kuwa zaidi ya mama wa mtoto
2. Sisi wanaume hatuna hizi habari za kunyanyasa watoto wa kambo. Tuna mambo mengi hivyo hatuna michongo ya kuanza kummind mtoto. Ndio maana bora mtoto alelewe na baba wa kambo(alelewe na mama yake) kuliko na mama wa kambo