tinkanyarwele
JF-Expert Member
- Dec 30, 2016
- 2,017
- 1,940
Salaam, Leo imesikika kuwa hakimu amemhukumu kunyongwa hadi kufa Mwl, aliyetoa adhabu hadi kupelekea mauti ya mwanafunzi wake. Naamini kila mzazi au mlezi au mwalimu hakupendezwa na kifo cha mtoto baada ya kuadhibiwa na mwalimu, lakini naamini kwa mwalimu yeyote aliyesikia Hukumu hii lazima ametafakari kwa undani juu ya hatima yake katika kazi yake. Binafsi napenda kuwashauri WALIMU ACHANA na watoto wa watu, nashauri mwalimu abakize kazi moja tu ya KUFUNDISHA NA KUELEKEZA.
Nahisi wakati umefika wa mwalimu kuachana na kutoa adhabu kwa watoto hasa adhabu zinazo gusa mwili moja kwa moja, hakuna anayependa mtoto alelewe hovyo lakini kwakuwa Nafsi ya MTU ni TAMU ni vyema kabisa mwalimu apoteze kazi siku ukibainika umeshindwa kuwalea vizuri wanafunzi kuliko kupoteza UHAI wako Kisa tu ulikuwa unamjenga mtoto wa MTU. Acha wafeli, acha wawe majambazi, acha wawe na nidhamu mbovu, acha wabebe mimba nk lakini msitoe adhabu ambazo zinaweza kupelekea matatizo makubwa kama kuuwaumiza watoto kiasi cha kuleta Ulemavu, Matatizo ya kisaikolojia na pengine kuleta Vifo.
Nimeyaandika Haya kwani naamini mwalimu ni mlezi, mlezi hawezi kutoa adhabu akiwa amelenga kumdhuru mtoto, lakini hakuna ajue kilicho mbele yake , unaweza kumgusa mtoto kumbe huo ndo ulikuwa mwisho wake, hatimaye unaishia kwenye mikono ya kitanzi, jera nk. Haya mambo yanaumiza sana, hakuna mzazi anayependa kumpoteza mtoto wake vivyo hivyo hakuna mwalimu anapenda kupoteza maisha yake au kazi yake. Walimu nawaomba na kuwasihi, jitafakari upya na kama itawezekana hata nchi nzima huo uwe mfumo na utaratibu, kama mwanafunzi atakuudhi kupindukia basi omba ruhusa rudi nyumbani kalale.
Usiogope, wakifeli hutakosa la kujieleza, wakikufukuza kazi rudi kwenu shika jembe kalime maisha si lazima upate msahara wengi hatuna mishahara na tunaishi. Poleni walimu, poleni wazazi, poleni wadau wa elimu na poleni walimu.