Kwa Walimu Wote, Bara na Visiwani

tinkanyarwele

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
1,599
2,000
Salaam, Leo imesikika kuwa hakimu amemhukumu kunyongwa hadi kufa Mwl, aliyetoa adhabu hadi kupelekea mauti ya mwanafunzi wake. Naamini kila mzazi au mlezi au mwalimu hakupendezwa na kifo cha mtoto baada ya kuadhibiwa na mwalimu, lakini naamini kwa mwalimu yeyote aliyesikia Hukumu hii lazima ametafakari kwa undani juu ya hatima yake katika kazi yake. Binafsi napenda kuwashauri WALIMU ACHANA na watoto wa watu, nashauri mwalimu abakize kazi moja tu ya KUFUNDISHA NA KUELEKEZA.

Nahisi wakati umefika wa mwalimu kuachana na kutoa adhabu kwa watoto hasa adhabu zinazo gusa mwili moja kwa moja, hakuna anayependa mtoto alelewe hovyo lakini kwakuwa Nafsi ya MTU ni TAMU ni vyema kabisa mwalimu apoteze kazi siku ukibainika umeshindwa kuwalea vizuri wanafunzi kuliko kupoteza UHAI wako Kisa tu ulikuwa unamjenga mtoto wa MTU. Acha wafeli, acha wawe majambazi, acha wawe na nidhamu mbovu, acha wabebe mimba nk lakini msitoe adhabu ambazo zinaweza kupelekea matatizo makubwa kama kuuwaumiza watoto kiasi cha kuleta Ulemavu, Matatizo ya kisaikolojia na pengine kuleta Vifo.

Nimeyaandika Haya kwani naamini mwalimu ni mlezi, mlezi hawezi kutoa adhabu akiwa amelenga kumdhuru mtoto, lakini hakuna ajue kilicho mbele yake , unaweza kumgusa mtoto kumbe huo ndo ulikuwa mwisho wake, hatimaye unaishia kwenye mikono ya kitanzi, jera nk. Haya mambo yanaumiza sana, hakuna mzazi anayependa kumpoteza mtoto wake vivyo hivyo hakuna mwalimu anapenda kupoteza maisha yake au kazi yake. Walimu nawaomba na kuwasihi, jitafakari upya na kama itawezekana hata nchi nzima huo uwe mfumo na utaratibu, kama mwanafunzi atakuudhi kupindukia basi omba ruhusa rudi nyumbani kalale.

Usiogope, wakifeli hutakosa la kujieleza, wakikufukuza kazi rudi kwenu shika jembe kalime maisha si lazima upate msahara wengi hatuna mishahara na tunaishi. Poleni walimu, poleni wazazi, poleni wadau wa elimu na poleni walimu.
 
Marwa_J_Merengo

JF-Expert Member
Aug 6, 2018
4,337
2,000
sure mkuu,hii adhabu aliyopewa huyu mwalimu ambae mshahara wake hauzidi laki 7 kwa mwezi ni kubwa mno na sijui imetolewa kwa kuangalia vigezo vipi.

Kwa nini basi hakubadilishiwa mashitaka kuwa kuua bila kukusudia.Mbona askari wakiua wakati wa utekerezaji wa majukumu yao hawapewi adhabu za namna hii
 
Espy

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
69,482
2,000
Eti acha wafeli,acha wabebe mimba nk nk......

Mkuu una watoto kweli? Je inamaana kwamba njia pekee ya kumnyoosha mtoto ni kipigo tu?
Tatizo hapa mimi naona ni kutoa adhabu kwa mihemko, hii sio kwa walimu tu bali hata kwa wazazi pia. Tuwasikilize watoto, kisha tufanye ufuatiliaji(hii pia inapunguza mihemko maana hadi ufuatilie na uthibitishe na hasira zitakuwa zimepungua hivyo utatoa adhabu stahiki)
Sheria na miongozo iko wazi ya aina za adhabu zinazopaswa kutolewa kwa wanafunzi, tuzifuate hizo na hatutokuwa na madhara yoyote.

Pia tusipende zaidi adhabu za kipigo as most of times hazijengi zaidi ya kumjengea mtoto uoga na kumfanya kuwa na heshima ya kuigiza awapo machoni pako tu kwa kuogopa adhabu. Tuelekeze zaidi kwa upendo, hiki ni kitu kinachokosekana sana majumbani na shuleni kwa ujumla.
 
breki sifungi

JF-Expert Member
Oct 15, 2014
662
500
sure mkuu,hii adhabu aliyopewa huyu mwalimu ambae mshahara wake hauzidi laki 7 kwa mwezi ni kubwa mno na sijui imetolewa kwa kuangalia vigezo vipi.

Kwa nini basi hakubadilishiwa mashitaka kuwa kuua bila kukusudia.Mbona askari wakiua wakati wa utekerezaji wa majukumu yao hawapewi adhabu za namna hii
we ni mpumbavu kabisa, nadhani hujazaa wewe, huna mtoto wewe unaishi kwa wazazi bado. kwa kosa alilofanya huyo mwl. kwa kumuadhbu vile mtoto bado unasema kapewa adhabu kubwa mno kweli?!! we ni kenge kabisa...watu tunatamani hadi kumkatia rufaa huyo mwl aliyeachiwa huru afu we unaongea mambo ya kipumbavu hapa. kwa fact zilizotolewa mbele ya mahakama ni dhahiri huyo mwl. alikusudia kuua, hiwezi mpiga mtoto kiasi kile. I'm a professional teacher from, adhabu kubwa na ya mwisho kwa mwanagunzi aliyefanya kosa kubwa kabisa hua ni kufukuzwa shule sio kumfanyia unyama kama ule
 
Chief Sam

JF-Expert Member
Jan 21, 2019
1,539
2,000
Na doubt na professional teacher yako aisee ayo matusi kwamba uchungu unao sana we are at the same block but l wonder hujui stress tulizonazo teachers usiangalie upande mmoja imetokea accidentally kwani adhabu alianzia kwa uyo mwanafunzi ni wengi sema day ilifika tu imagine wingi na usumbufu plus mambo ambayo serikali haijamtimizia,mambo ya familia ni pasua kichwa sema mtoa thread nakupongeza umeongea kama ni mtu wa kada na mkosaji salute to you

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chinga One

JF-Expert Member
May 7, 2013
10,560

Stressed teacher,pliz JPM ongeza mshaharA hawa watu
 
Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
12,591
2,000
Fundisho kwa wengine, mna torture watoto wakitoka hapo hawajui UPENDO,CONFIDENCE NA JINSI YA KUISHI NA WENGINE kisa nyie na adhabu zenu physical and psychological..kwa kweli Kama wewe ni Mwalimu una tabia ya kuumiza watoto wa wengine JIREKEBISHE, shuleni sio sehemu ya kuumiza watoto wa wenzio
 
Nyankuru Wankuru

JF-Expert Member
Apr 22, 2018
1,200
2,000
Kwa kigezo cha kuuwa mtoto asiekuwa na hatia
sure mkuu,hii adhabu aliyopewa huyu mwalimu ambae mshahara wake hauzidi laki 7 kwa mwezi ni kubwa mno na sijui imetolewa kwa kuangalia vigezo vipi.

Kwa nini basi hakubadilishiwa mashitaka kuwa kuua bila kukusudia.Mbona askari wakiua wakati wa utekerezaji wa majukumu yao hawapewi adhabu za namna hii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
GreenCity

JF-Expert Member
May 28, 2012
5,611
2,000
Na doubt na professional teacher yako aisee ayo matusi kwamba uchungu unao sana we are at the same block but l wonder hujui stress tulizonazo teachers usiangalie upande mmoja imetokea accidentally kwani adhabu alianzia kwa uyo mwanafunzi ni wengi sema day ilifika tu imagine wingi na usumbufu plus mambo ambayo serikali haijamtimizia,mambo ya familia ni pasua kichwa sema mtoa thread nakupongeza umeongea kama ni mtu wa kada na mkosaji salute to you

Sent using Jamii Forums mobile app
Acheni kujificha kwenye kichaka cha STRESS/FRUSTRATION, kama kazi ngumu acheni lakini sio kugeuka VAMPIRES kwa watoto wetu!
 
Espy

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
69,482
2,000
Na doubt na professional teacher yako aisee ayo matusi kwamba uchungu unao sana we are at the same block but l wonder hujui stress tulizonazo teachers usiangalie upande mmoja imetokea accidentally kwani adhabu alianzia kwa uyo mwanafunzi ni wengi sema day ilifika tu imagine wingi na usumbufu plus mambo ambayo serikali haijamtimizia,mambo ya familia ni pasua kichwa sema mtoa thread nakupongeza umeongea kama ni mtu wa kada na mkosaji salute to you

Sent using Jamii Forums mobile app
Naomba nipingane nawe kidogo, kuna uzi umetolewa humu wa namna mwalimu huyu alivyomuadhibu huyu mtoto. Hata kama ni stress hapana jamani. Kweli walimu tuna mengi tunayopitia lkn isiwe ndio kigezo cha kumalizia hasira zetu kwa wanafunzi. Emagine huyu mtoto angekuwa ni wako ungemuelewa huyu mwalimu kweli?
 
Numbisa

JF-Expert Member
Dec 12, 2016
177,720
2,000
Mwalimu aliyebaki kupiga watoto anajitafutia makubwa. Waalimu wengi walishaacha hizo baada ya kuona hawapewi kipaumbele.

Kizazi cha facebook cha kuandika xaxa badala ya sasa,kurara badala ya kulala ni matokeo ya mgomo baridi wa waalimu enzi na enzi
 
FPT

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
952
1,000
acha kuandika ujinga mkuu, adhabu inatakiwa itolewe ila ni kwa mujibu wa sheria na taratibu na utakapotoa adhabu nje ya utaratibu uliowekwa lolote litakalotokea ulikusudia ufanye hivyo. yaani unamchapa mtoto fimbo zaidi ya kumi tena sehemu mbalimbali halafu tuone sawa tu?

hivi patia picha yule mtoto alivyoteseka wakati anapigwa na kuni tena kichwani,leo unatetea ujinga. na mtanyongwa sana kama mnaona mnafundisha mifugo. kama unaona jukumu la kufundisha bila kutoa adhabu kali acha kazi kuna watu wako passionate kweli na wanapenda ualimu sana waache hao.
 
FPT

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
952
1,000
sure mkuu,hii adhabu aliyopewa huyu mwalimu ambae mshahara wake hauzidi laki 7 kwa mwezi ni kubwa mno na sijui imetolewa kwa kuangalia vigezo vipi.

Kwa nini basi hakubadilishiwa mashitaka kuwa kuua bila kukusudia.Mbona askari wakiua wakati wa utekerezaji wa majukumu yao hawapewi adhabu za namna hii
nime type nimefuta, nimeona uvivu kukujibu.
adhabu imetolewa kulingana na kosa nalo ni kuua kwa kukusudia. Huyu Mungu wa ajabu sana tena sana, ni bodaboda wangapi ukisahau mzigo wako kwake anakuletea? lakini bodaboda wa watu akapeleka mzigo wa watu na hapo ikaonekana mtoto hakuwa na hatia ila mwalimu alikusudia kumuua. Mungu yupo kutetea wanaonyanyaswa na hili ni funzo kwetu sote, usihukumu usije ukahukumiwa
 
Demi

JF-Expert Member
Nov 22, 2016
22,754
2,000
sure mkuu,hii adhabu aliyopewa huyu mwalimu ambae mshahara wake hauzidi laki 7 kwa mwezi ni kubwa mno na sijui imetolewa kwa kuangalia vigezo vipi.

Kwa nini basi hakubadilishiwa mashitaka kuwa kuua bila kukusudia.Mbona askari wakiua wakati wa utekerezaji wa majukumu yao hawapewi adhabu za namna hii
Ameua bila kukusudia? Kivipi yaani?
 
Demi

JF-Expert Member
Nov 22, 2016
22,754
2,000
Na doubt na professional teacher yako aisee ayo matusi kwamba uchungu unao sana we are at the same block but l wonder hujui stress tulizonazo teachers usiangalie upande mmoja imetokea accidentally kwani adhabu alianzia kwa uyo mwanafunzi ni wengi sema day ilifika tu imagine wingi na usumbufu plus mambo ambayo serikali haijamtimizia,mambo ya familia ni pasua kichwa sema mtoa thread nakupongeza umeongea kama ni mtu wa kada na mkosaji salute to you

Sent using Jamii Forums mobile app
Stress zikufanye uue? U are not serious mkuu. Mwache nae akafilie huko mbele
 
ZionGate

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
5,541
2,000
Kwani ukimpa mtoto adhabu inayotambulika kisheria unapungua nn, yaani unataka kuhalalisha hayo mauaji. Inauma mtoto katoka home mzima alafu unaletewa taarifa kapewa adhabu hadi mauti imemkuta weeee ntakuferemenda we mwl. yaani sikuachi hata kwa dawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
FPT

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
952
1,000
Eti acha wafeli,acha wabebe mimba nk nk......

Mkuu una watoto kweli? Je inamaana kwamba njia pekee ya kumnyoosha mtoto ni kipigo tu?
Tatizo hapa mimi naona ni kutoa adhabu kwa mihemko, hii sio kwa walimu tu bali hata kwa wazazi pia. Tuwasikilize watoto, kisha tufanye ufuatiliaji(hii pia inapunguza mihemko maana hadi ufuatilie na uthibitishe na hasira zitakuwa zimepungua hivyo utatoa adhabu stahiki)
Sheria na miongozo iko wazi ya aina za adhabu zinazopaswa kutolewa kwa wanafunzi, tuzifuate hizo na hatutokuwa na madhara yoyote.

Pia tusipende zaidi adhabu za kipigo as most of times hazijengi zaidi ya kumjengea mtoto uoga na kumfanya kuwa na heshima ya kuigiza awapo machoni pako tu kwa kuogopa adhabu. Tuelekeze zaidi kwa upendo, hiki ni kitu kinachokosekana sana majumbani na shuleni kwa ujumla.
hawa inabidi waambiwe kwa upole maana watanyongwa wengi sana wasipoangalia. sifa mbaya sana , yote hiyo ilikuwa ni kutafuta sifa. hata kama kweli alikuwa kaiba ndio umpige vile? hata mtaani mwizi anapokamatwa wanaopiga wakiona polis wanatawanyika wanajua ni kosa sembuse huyo mwalimu anaua akiwa peke yake na bila ushihidi? Mungu wangu epushia mbali ila hili liwe funzo kabisa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom