Hatua za kisheria ili kumrudisha mtoto shuleni aliyesimamishwa masomo kwa utashi wa waalimu na si utashi wa Sheria za shule!

Weakman

JF-Expert Member
Jul 23, 2021
861
1,384
Kuna dogo mmoja Ni ndugu yangu wa mbali!

Amepatwa na hekaheka ya kutotakiwa shuleni pamoja na wenzake kadhaa!

Msimamo wa mkuu wa shule ni kwamba hawawahitaji wanafunzi hao shuleni kwake, hivyo wazazi wawatafutie shule zingine

Hii ni shule ya serikali ambayo miongozo ya kuwasimamisha wanafunzi shule imewekwa, na haijafuatwa

Hawa wanafunzi wote ni kidato Cha nne, ktk shule hii ya kata, na hoja ya msingi ya mkuu wa shule ni kuwa wanafunzi Hawa hawana mahudhurio mazuri, hivyo watashindwa kuendana na kasi ya shule yake ktk mchakato wa kuboresha taaluma na kutoa matokeo Bora kidato Cha nne!

Hoja hii imefikishwa kwa Afisa Elimu, na akaahidi atafuatilia Ila Kuna ukimya unaendelea unaoashiria kuwa hoja imepuuzwa.

Huenda ni ajenda ambayo Afisa Elimu anaitambua pia

Hivyo naomba kuelimishwa Ni njia gani sahihi ya kisheria inaweza kutumika kumrudisha mtoto shuleni aweze kufanya mtihani wake kidato Cha nne!!

Naomba kuwasilisha!
 
nafikiri ni busara kurudi kuzungumza na Mkuu wa shule pamoja na Mwalimu wa Taaluma pia ikiwezekana jaribu kudodosa kutoka kwa wanafunzi wenzake ili kupata picha ya tukio zima,nafikiri Mkuu wa Shule amefanya hivyo ili kwa sababu za kiutawalakwa miongoni mwa majukumu yake naimnai ni kusimmaia na kuhakikisha shule yake inafanya vizuri na wanafunzi kupata matokeo mazuri,hivyo kama wanafunzi wako wamekuwa na tabia za utoro uliokidhiri kiasi cha kuathiri masomo yao nafikiri kwa wakati ule aliotoa maamuzi alikuwa sahihi ili sasa wazazi waweze kufanya ufuatiliaji juu ya mahudhurio pamoja na mwendo wa wanafunzi wao shuleni,na pengine wanafunzi husika wanaweza kuwa walishapewa taarifa ya kuwaita wazazi au walezi shuleni na hawakuweza kutoa taarifa mahali husika,ulifikiri ni hatua gani mwalimu Mkuu alipaswa kufanya?kulinganisha na muda uliobaki wa kujiandaa na mitihani ya Kidato cha nne? Nashauri utafute muda wa kuonana na uongozi wa Shule husika kutatua changamoto hiyo,maana hata kama amewsimamisha alipaswa kusema ni kwa muda gani? ili kuruhusu taratibu zingine ziwe kuendelea ya kuwapa vijana hao muda wa kujiandaa na mitihani yao ya mwisho
 
Kwani huyo kijana anataka shule? Maana inaonyesha hahitaji ila nyie ndo mnamlazimisha
 
Hajawasimamisha,bali amewafukuza shule kwa kuwaambia wakatafute shule nyingine yeye hataki kuwaona shuleni kwake! Safi sana Mwalimu Mkuu Mwanafunzi mtoro hana nafasi labda utoro wake uwe na sababu za msingi za kibinaadamu,tunaweza peana ushauri!!
 
Swali ni kwamba tuhuma alizonazo mwanao na hao wengine ni za kweli ama uongo?

Kama ni za kweli, utasemaje ni utashi wa walimu?

Inavyoonekana huyo mtoto amejiingiza kwenye makundi, na perfomance yake darasani ni mbovu sana.

Walimu huwa hawawafukuzi wanafunzi ovyo ovyo, ukiona mwanafunzi amefukuzwa, tena shule ya serikali basi ujue amekubuhu..

Cha kufanya hapo usianze kupambana na walimu, pambana na mwanao..
 
Wazazi/walezi mnashida sana mtoto ni mtoro kwa maana nyingine hataki shule hapo mkuu kosa lake ni lipi.
Mtafutie shule nyingine
 
Ukiona umefukuzwa Gvt jua umekubuhu sanaaaa,
Kama walezi wa huyo kijana mmefeli sana kumsimamia,
Cha kufanya, muhamisheni ila hakikishen sasa mnamfuatilia kwa ukaribu, msipambane na walimu,
Wanaweza warudisha then wakawatafutia kosa wakawafuta jumla sasa,
Mana kwa story hio huyo dogo ni nunda, so kumtafutia kosa la kumfuta shule kisheria sio kazi kubwa kabisa
 
Kwa kulisoma andishi lako naona kuwa unaamini mwanao kaonewa. Kwenye shule za serikali, mpaka uongozi wa shule unamwambia hivyo huyo kijana, ni kwamba wamejaribu alternative zote za kumuokoa bilamafanikio. Hivyo usiende na mtazamo wa kupambana na walimu, bali uende kutafuta suluhu hasa lengo likiwa kmsaidia mtoto.
 
Ili kutokomeza zerooooo watoto na watukutu wote ni kuwalamba stiki Kila wakionekana anga za shule.
 
  • Kicheko
Reactions: K11
Kwani huyo kijana anataka shule? Maana inaonyesha hahitaji ila nyie ndo mnamlazimisha
tatizo linaanzia hapa

Wazazi sometime wanakera, sioni tatizo la mwalimu mkuu, tatizo lipo kwa wazazi na watoto wao

Halafu kama mzazi unashindwaje kuongea na mtu mzima mwenzako(headmaster) mpaka akakuelewa?

Ama na wao watakuwa walitumia jazba badala ya kujishusha ili kufanikisha lengo?

Maana walimu walio wengi hawanaga sifa ya roho mbaya
 
Tatizo wazazi wengi ni hamnazo
 
Sheria inasema akiwa mtoro Kwa siku 90 mfululizo anakua amejifukuzisha Shule. Kama mtoto hataki kusoma msaidieni Kwa kumpa ujuzi wa kujiajiri, mnaweza kumpeleka veta na akajimudu maisha vikevile sio lazma asome Sekondari, Watu wanamaliza chuo maelfu na maelfu na ajira hakuna. Anaweza kujifunza ujuzi wa kujiajiri vzr tu
 
  • Thanks
Reactions: K11
nafikiri ni busara kurudi kuzungumza na Mkuu wa shule pamoja na Mwalimu wa Taaluma pia ikiwezekana jaribu kudodosa kutoka kwa wanafunzi wenzake ili kupata picha ya tukio zima,nafikiri Mkuu wa Shule amefanya hivyo ili kwa sababu za kiutawalakwa miongoni mwa majukumu yake naimnai ni kusimmaia na kuhakikisha shule yake inafanya vizuri na wanafunzi kupata matokeo mazuri,hivyo kama wanafunzi wako wamekuwa na tabia za utoro uliokidhiri kiasi cha kuathiri masomo yao nafikiri kwa wakati ule aliotoa maamuzi alikuwa sahihi ili sasa wazazi waweze kufanya ufuatiliaji juu ya mahudhurio pamoja na mwendo wa wanafunzi wao shuleni,na pengine wanafunzi husika wanaweza kuwa walishapewa taarifa ya kuwaita wazazi au walezi shuleni na hawakuweza kutoa taarifa mahali husika,ulifikiri ni hatua gani mwalimu Mkuu alipaswa kufanya?kulinganisha na muda uliobaki wa kujiandaa na mitihani ya Kidato cha nne? Nashauri utafute muda wa kuonana na uongozi wa Shule husika kutatua changamoto hiyo,maana hata kama amewsimamisha alipaswa kusema ni kwa muda gani? ili kuruhusu taratibu zingine ziwe kuendelea ya kuwapa vijana hao muda wa kujiandaa na mitihani yao ya mwisho
Pamoja na yote hayo Mkuu wa shule hana mamlaka ya kumnyima haki ya elimu mtoto kwasababu nyepesi kama hizo.

Ni vema wazazi wa huyo mtoto waende haki ngazi ya mkoa kwa afisa elimu mkoa then wakiona kimya basi wafike hadi wizara ya elimu/Tamisemi.
 
Nimesoma Andiko lako lote, inaonekan unatoa hukum kwa shule (walimu) pasipo kuelezea kwa undan mtoto ana utoro wa kiasi gan, haiwezekan awe mtoro siku tatu akafukuzwa, ukiona mtoto anafukuzwa gvt ujue Kuna shida, gvt kamwe haifukuz watoto ovyo km private,

Kuna scenario kama hiyo iliwahi to kea, Mtoto wa OCD wilaya fulan alifukuzwa shule kwa utoro, OCD akapiga sim kwa afisa elimu ili suala liishe, afisa elimu akapiga kwa mkuu wa shule ili walimalize lkn mkuu wa shule akakataa akasema yule hatumtaki ni mkorof na mtoto tunavoongea muda si mrefu ametoka kuwatisha walimu na ameenda porin kuvuta bangi, bas afisa elimu aliposikia akamrudia OCD na kumpa ripot kamili, baada ya hapo OCD akatuma vijana wake waemde shulen ,vijana wakaelekezwa mtoto alipo wakamkuta dogo anavuta bang na wenzake ndo wakakamatwa, mwishon yule dogo alihamishwa shule

Ushauri

Ongea na mwanao kuhusu utoro wake, pengine anakuaga anaenda shule, kumbe akifika njian ana-diverge ww unajua kafika shule ikiwezekan omba mahudhirio yake ya darasan,

Halafu mwishon kabisaa jishushe kwa mkuu wa shule uwe mpole busara itumike, usitumie Sheria kwa suala hili utakaeumia ni wewe, kama mkuu atakubalia kishingo upande watam-disperate mtoto mwishowe atafeli tu
 
Kuna dogo mmoja Ni ndugu yangu wa mbali!

Amepatwa na hekaheka ya kutotakiwa shuleni pamoja na wenzake kadhaa!

Msimamo wa mkuu wa shule ni kwamba hawawahitaji wanafunzi hao shuleni kwake, hivyo wazazi wawatafutie shule zingine

Hii ni shule ya serikali ambayo miongozo ya kuwasimamisha wanafunzi shule imewekwa, na haijafuatwa

Hawa wanafunzi wote ni kidato Cha nne, ktk shule hii ya kata, na hoja ya msingi ya mkuu wa shule ni kuwa wanafunzi Hawa hawana mahudhurio mazuri, hivyo watashindwa kuendana na kasi ya shule yake ktk mchakato wa kuboresha taaluma na kutoa matokeo Bora kidato Cha nne!

Hoja hii imefikishwa kwa Afisa Elimu, na akaahidi atafuatilia Ila Kuna ukimya unaendelea unaoashiria kuwa hoja imepuuzwa.

Huenda ni ajenda ambayo Afisa Elimu anaitambua pia

Hivyo naomba kuelimishwa Ni njia gani sahihi ya kisheria inaweza kutumika kumrudisha mtoto shuleni aweze kufanya mtihani wake kidato Cha nne!!

Naomba kuwasilisha!
Kabla sijasema neno, ni kweli huyo mtoto ni mtoro?
 
Bodi ya shule ndio wamiliki wa shule na maamuzi ya kumfukuza mtoto shule yanatoka kwao. Katibu wa bodi na mwalimu mwakilishi wanaishia kwenye kumsimaimisha masomo mtoto hadi pale atakapoita boda na kumshtaki mtoto. Gharama za bodi ni jambo jingne.. Wakati nasoma mwanafunzi wenzetu alifukuzwa shule hali ya kuwa amesajiliwa kabisa ila alifukuzwa na mtihani tunanza kama kesho na maafari tulifanya wote. Kama umefanya makosa ya kufukuzwa shule utafukuzwa tu hasa kwa asiyesajiliwa na mitihani. Kwa aliyesajiliwa hadi atende kosa la jinai.
 
Back
Top Bottom