Kwa wale wanaotaka kuwekeza kwenye mashamba ya miti

Epukeni kama ukoma watu wa njombe ni matepeli wakishikirisha na ushirikina kila mara. Ni ushauri tu
 
Hakuna shamba tupu la Tsh 600,000/ kule Njombe na Iringa, labda pande za Tukuyu/Rungwe.
Wewe muuzaji utakuwa umedanganywa, mimi mwenyewe niko pande hizo hizo. Hatujafikia bei hiyo.
Mkuu hii ni nje ya mada

Mbegu za miti zinapatikana wapi? Zinauzwaje?

Inakua baada ya muda gani?
 
Mkuu hii ni nje ya mada

Mbegu za miti zinapatikana wapi? Zinauzwaje?

Inakua baada ya muda gani?
Mbegu za miti zinapatikana TTSA Iringa, au Morogoro au Lushoto au Arusha. Bei ya pines ni Tsh 90,000/ mpaka msimu uliopita, ila mbegu zilizoboreshwa kilo moja ni zaidi ya milioni moja.

Miche ya miti hupatikana kwenye vitalu na bei ya kawaida ni Tsh 80/ mpaka Tsh 100/ kwa mche. Kuna baadhi ya maeneo mpaka Tsh 50/. Kuna sehemu nyingine mpaka 150/. Miaka ya nyuma GRL walikuwa wanagawa bure kwa out growers.

Rotation period ya pines ni 23yrs, Cyprus 26yrs.
 
Hakuna shamba tupu la Tsh 600,000/ kule Njombe na Iringa, labda pande za Tukuyu/Rungwe.
Wewe muuzaji utakuwa umedanganywa, mimi mwenyewe niko pande hizo hizo. Hatujafikia bei hiyo.
BORA UMENIFUMBUA MACHO NAMI NAHITAJI SHAMBA UKO NJOMBE
 
Kuwa na busara kila BIASHARA sio lazima umaharibie Mwenzio na wewe tangaza yako
Boss samahani kwa nitakayoyasema,

Wazo la uzi wako ni zuri na umejitolea kuwasaidia wengi ila ulichokosea ni kusahau kuwa biashara yoyote ile inahitaji uaminifu yaani ukweli, bei sahihi hata ikiwa mteja haijuwi bei, kauli na kujituma pia.

Nina shida kabisa ya shamba na nimekuwa nikijaribu nashindwa kupata connection, namba zako nime copy ila nashindwa kukutafuta kwakuwa bei zako zinanipa mashaka.

Sasa mkuu nitoe hofu na uniambie hilo shamba la 600,000 tofauti ni ipi na hilo la 120,000??

Ila mwisho wa siku uaminifu wako ndiyo unafanya kupata wateja au kutokupata wateja.

Kumbuka:
Hayupo anayekuharibia biashara bali biashara yako unajiharibia mwenyewe kutokana na bei zako.

Note;
Nitatathimini kutokana na majibu yako.
 
Mbegu za miti zinapatikana TTSA Iringa, au Morogoro au Lushoto au Arusha. Bei ya pines ni Tsh 90,000/ mpaka msimu uliopita, ila mbegu zilizoboreshwa kilo moja ni zaidi ya milioni moja.

Miche ya miti hupatikana kwenye vitalu na bei ya kawaida ni Tsh 80/ mpaka Tsh 100/ kwa mche. Kuna baadhi ya maeneo mpaka Tsh 50/. Kuna sehemu nyingine mpaka 150/. Miaka ya nyuma GRL walikuwa wanagawa bure kwa out growers.

Rotation period ya pines ni 23yrs, Cyprus 26yrs.
Kilo moja inatosha hekari ngapi?
 
Wapi parachichi zinastawi sana na gharama zake zikoje kwa heka?
Sehemu kubwa ya ukanda wa nyanda za juu kusini ( Njombe/Iringa/Mby/Rukwa na some parts za Songea), Ukanda wa wilaya ya Hai kule kilimakyaro, Kigoma, Bukoba.
Bei ya ardhi inatofautiana toka kipande kimoja cha nchi mpaka kingine. Mfano Heru Juu ni kuzuri sana kwa Parachichi, ila ardhi ni ghari sana, 2016 nilichemsha. Klm/Mby ardhi ni ghari. Mufindi na Njombe ardhi ni cheap, bei zinacheza kwenye 90,000/ mpaka 150,000/ maxmum.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom