Ngombe bora wa maziwa Mbeya

tajiri12

New Member
Feb 4, 2023
1
1
#MBALIZI_FARMING_PROJECT
0752 652 249
0752 652 249
MAANDALIZI YA KUSTAWISHA MAJANI YA NG’OMBE
2.1 Majani ya ng’ombe wa maziwa

Chakula kikuu cha ng’ombe ni nyasi. Kwa hiyo, maandalizi makubwa ni kutayarisha mashamba ya majani. Ziko aina nyingi za majani. Majani haya yanaweza kugawanywa katika sehemu mbili kubwa:
a) Nyasi
b) Majani aina ya mikundekunde

Kuna mimea mingi sana kutoka kila aina iliyotajwa hapo juu. Hata hivyo, kwa kufugia ng’ombe ndani, wakulima wanashauriwa kustawisha aina chache kufuatana na:

i) Wingi wa mazao yanayozalishwa na nyasi au mikundekunde kwa eneo.
ii) Ubora wa nyasi au mikundekunde.
iii) Uvumilivu wa nyasi au mikundekunde kwa hali ya hewa na udongo wa shamba.

Kufuatana na uzoefu uliokwishapatikana, nyasi na mikundekunde ifuatayo inafaa ipandwe na wakulima:

i) Nyasi:
a) Matete/mabingobingo
b) Guatamala
c) Setaria
d) Gamba

ii) Mimea aina ya mikundekunde:
a) Leuceana
b) Desmodium
c) Calliandra
d) Gliricidia

iii) Nyasi na mikundekunde ya asili
Pamoja na nyasi na mikundekunde maalumu iliyotajwa hapo juu ambayo mkulima wa ng’ombe wa maziwa anapaswa kuwa nayo kwenye shamba lake la majani, mkulima pia anaweza akawa na shamba la nyasi na mikundekunde ya asili. Inashauriwa mifugo ya asili isichungwe kwenye shamba hili la majani ya asili kwani kwa kufanya hivyo wataeneza kupe kwenye shamba na watapunguza ubora wa majani ya asili kwa kuyala na
kuyakanyaga kanyaga ikiwezekana shamba la asili liwekewe wigo imara wa mimea ya asili au seng’eng’e.

Pia inashauriwa mkulima apande mikundekunde inayotambaa au ya miti ili kuboresha shamba lake la majani ya asili. Mkulima akate majani ambayo bado ni machanga kutoka shamba la asili kulisha mifugo yake.

2.2 Upandaji na Utunzaji wa baadhi ya nyasi na Mikundekunde muhimu
2.2.1 Matete au mabingobingo

(a) Sifa

Matete ni nyasi ambazo zinashauriwa kulisha ng’ombe wanaofugwa ndani kwa sababu zifuatazo:
  • Mazao yake kwa eneo ni makubwa.
  • Yakitunzwa vizuri yanavumilia kiangazi.
  • Ni rahisi kukatwa.
  • Yanatoa lishe bora kuliko aina nyingi za nyasi.

Kwa ukuaji mzuri, matete yanastawi vizuri sehemu zenye mvua ya kutosha (zaidi ya mm 700 kwa mwaka). Yanapendelea udongo ambao hautuamishi maji mengi. Hata hivyo yanaweza kustawishwa katika aina yoyote ya udongo.

(b) Aina za matete/mabingobingo
Ziko aina nyingi za matete. Kuna matete/mabingobingo ya asili na yale yaliyoletwa toka nje ya nchi. Matete/mabingobingo ya asili yameonekana kustahimili hali ya hewa na magonjwa ya majani.

(c) Jinsi ya kupanda matete/mabingobingo
Kabla ya kupanda matete, sharti shamba litayarishwe vizuri kwa kulimwa na kuondoa nyasi aina ya kwekwe na kupunguza kivuli. Pia wakati wa kulima ni vizuri kuchanganya udongo na samadi ili kupata mazao mengi na bora.

Muda mzuri wa kupanda ni mwanzoni mwa mvua. Sehemu zenye mvua misimu miwili katika mwaka inashauriwa kupanda mwanzoni mwa Oktoba na Machi/Aprili. Wakati wa kupanda:
  • Tumia shina lililokomaa, lenye pingili tatu au zaidi.
  • Panda katika safu ya upana wa futi 3 au sm 90 na shina liwe chini ya ardhi kwa sm 10.
Inashauriwa kupanda shamba la matete karibu na zizi ili kurahisisha kazi ya kubeba nyasi
pamoja na mbolea

MBALIZI FARMING PROJECT
(1) Tunao mitamba ambao awajapandwa ila waweza pandwa mda wowote bei ni kuanzia Tsh 1800000 adi 2000000 inategemea na mtamba wenyewe
(2) Pia mtamba mwenye mimba kuanzia miezi mitatu (3) adi miezi sita (6) ni Tsh2000000 adi 2500000
(3) PIA tunao ng'ombe walio zaa mara moja mara mbili na mara tatu ambao wanakamuliwa maziwa kuanizia liter 16 adi 22 inategemea na ng'ombe mwenyewe bei zao ni kuanizia Tsh 2300000 adi 2600000
(4) Na pia kwa wale wanao itaji ndama madume pamoja na majike wanapatikana kuanzia umri wa miezi minne adi sita kwa bei kuanzia Tsh 750000 adi 850000

KARIBU KWETU UNUNUE NGOMBE BORA KWA UZALISHAJI

wasiliana nasi kwa simu namba
0752 652 249
IMG-20230321-WA0000.jpg
IMG-20230321-WA0005.jpg


Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Je Hawa ng'ombe wanapatikana muda wote? Mnawazalisha ninyi wenyewe? Au nanyi ni mawakala (dalali). Nauliza hivi Ili Nije Moja kwa Moja ofisini kwenu na siyo kunipeleka kwa mkulima.
 
Back
Top Bottom