Kwa wale wanaotaka kuwekeza kwenye mashamba ya miti

js52471224

Member
Oct 8, 2017
36
15
Wanaotaka kuwekeza kwenye miti wanaweza kuniona mashamba yapo Njombe Lugarawa Ugera.Nauza Shamba lenye miti sh.1,000,000 Kwa eka moja,shamba tupu lakupanda mwenyewe sh.600,000 karibu MAWASILIANO 0654889707
 
Wanaotaka kuwekeza kwenye miti wanaweza kuniona mashamba yapo Njombe Lugarawa Ugera.Nauza Shamba lenye miti sh.1,000,000 Kwa eka moja, shamba tupu lakupanda mwenyewe sh.600,000 karibu MAWASILIANO 0654889707
Kwa heka moja au??
 
Hakuna shamba tupu la Tsh 600,000/ kule Njombe na Iringa, labda pande za Tukuyu/Rungwe.
Wewe muuzaji utakuwa umedanganywa, mimi mwenyewe niko pande hizo hizo. Hatujafikia bei hiyo.
Jaribu kunifafanulia mkuu kabla sijamtafuta huyu jamaa bei, sifa za maeneo hayo na tahadhari za kuchukua kabla,wakati na baada ya kununua shamba.
 
Kuwa na busara kila BIASHARA sio lazima umaharibie Mwenzio na wewe tangaza yako
 
Hata wewe unawaharibia watu wanaotaka kuwekeza kwa sababu ya kuwaambia vitu ambavyo havipo. Unadhani ukishampiga mtu kwa bei hiyo na kesho yake akasikia jirani yake kanunua kwa laki na nusu eneo hilo hilo atajisikiaje? Au fikiria ndo wewe unapigwa na jamaa kienyeji utafanyaje?

Tuhurumiane jamani, gharama za uwekezaji zinapokuwa kubwa sana zinafanya wengine washindwe kuwekeza mkuu, matokeo yake wanabaki wachache kwenye sector hiyo.

Sitakaa kimyaa kama naweza kuzuia dhuruma iliyo ndani ya uwezo wangu kama hii yako.Potelea karibu hata kama utanichukia lakini nimesema ukweli.
 
Jaribu kunifafanulia mkuu kabla sijamtafuta huyu jamaa bei, sifa za maeneo hayo na tahadhari za kuchukua kabla,wakati na baada ya kununua shamba.

Bei za mashamba yaliyo karibu na mji wa Njombe labda 50/70 km bei yake iko kati ya 100,000/ mpaka 120,000/ pamoja na gharama ndogo ndogo. Ukienda umbali mpaka wa 100km unapata kwa 80,000/90,000/ kwa eka.Hilo ni shamba tupu. Maeneo ya Njombe mengi sana yanafikika kwa gari, yana mvua za kutosha, manpower skilled ipo.

Usinunue shamba la familia bila kuwashirikisha wote, hakikisha mwenyekiti wa Kitongoji na mwenyekiti wa kijiji wameshiriki zoezi Zima. Lipia malipo ya kijiji bila kukwepa, angalia usije ukauziwa maeneo ya mifugo. Kama shamba linauzwa na mmiliki wa pili, tafuta sababu kwa nini analiuza. Dalali aishie kukuonyesha mwenye shamba, baada ya hapo mengine fanya mwenyewe.

Baada ya kununua, hakikisha kijiji kinakupa mhitasari na nenda Njombe waje wakupimie kabisa. Nenda na mashahidi wako na kama huna omba viongozi wa kijiji wakusaidie kupata majirani wa shamba husika ili wasaidie kuonyesha mipaka.
 
Shukrani sana mkuu, umenifumbua macho nina uhitaji wa kununua shamba.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom