Kwa wale tuliowahi kwenda kwa waganga wa kienyeji, tukutane hapa

Mjina Mrefu

JF-Expert Member
Dec 6, 2016
3,030
3,324
Kila mtu huwa ana imani yake

Kila mtu ana mbinu zake za kutatua matatizo yake.

Wapo ambao wakipata shida kidogo tu ni kwa babu sangoma wanakimbilia.

Tujuzane, vipi gharama huko? Shida zinatatulika? Permanently or temporarily?

Na pia nasikia every dark magic comes with a price, ni kweli..? Ni price zipi mnalipa kupata magic nyeusi hizo

Tujuzane

Binafsi mimi sijawahi kukanyaga kwa sangoma na sitakaa nikanyage huko
 
Kama ni kweli hujawahi kukanyaga huko ni vizuri sana! Endelea kushikilia msimamo huohuo ila maisha hayana formula na hujafa hujaumbika
 
Jirani yetu binti wao alisumbuliwa na maradhi, walihangaika hospitali zote , yule dada ilikuwa akisafiri to the moon ni ugonjwa wakupoteza fahamu.

Mmoja wa Sangoma alisema binti analogwa na wazazi wake. Wazazi wenyewe waliblow mapigo .
 
Msema kweli mpenzi wa mungu.nilishakwenda kwa mganga.kwa ajili ya demu.tulikuwa wapenzi ghafla aka badilika.akawa mgumu kinomaaa.hanipendi tena.niliumia.kuna rafiki yangu yeye ni mganga nikamueleza akasema tulia atarudi.
Tukafanya Mandingo mixer kuoga njia panda usiku.kuchoma sana UDI.kupasua Nazi n.k
Kiukweli demu alianza kubadilika na kuanza kuongea na Mimi.Mara salam n.k.
Siku zikapita tukarudi tena kwenye penzi.ila hatukudumu tuliachana.
Ushauri kama MTU hakupendi ACHANA NAE.MADAWA HUISHA NGUVU.
 
Hiyo tamati ndio UKWELI japo mchungu
 
Jirani yetu binti wao alisumbuliwa na maradhi, walihangaika hospitali zote , yule dada ilikuwa akisafiri to the moon ni ugonjwa wakupoteza fahamu.

Mmoja wa Sangoma alisema binti analogwa na wazazi wake. Wazazi wenyewe waliblow mapigo .
How sasa.? Wazazi wake wamloge ili iweje?
 
Niliwakuta wanafanya mazingaombwe mara wakatupaka dawa ili tuone miujiza yao. Hapo niko kidato cha tatu.
Hawakufanya tuone kitu badala yake wakasema kila aliyepakwa dawa awafuate au wakivimba mikono baadae wasijelaumu.
Mie huyoo nikaunga tela kuwafuata huko uchochoroni ngarenaro hadi walipokuwa wana 'ofisi' yao.

Kuna dada akaingia nikasikia analalamika yeye ni housegirl na bosi anamnyanyasa hivyo anaomba bosi atengenezwe.

Kuna mzee akaingia nikasikia analalamika amezulumiwa shamba hivyo waliomzulumu watengenezwe.

Wakaendelea watu wengi mie bado naogopa.

Ikafika ndo nimebaki wa mwisho nikaingia. Nikakuta jamaa amekaa kitandani kumejaa maburungutu ya hela na matungyli na hirizi kadhaa. Akaniuliza nataka nini nikamwambia sina shida yeyote ila kwa kuwa wamesema aliyepakwa dawa aende na mie ndo nimefika.

Akanihoji endapo ningetaka fedha kwa ajili ya shule. Nikamwambia sihitaji maana sitakuwa na jibu la kuwapa wazazi kuhusu nilipotoa. Akaniambia niweke sikio kwenye moja ya tunguli nisikilize mizimu inasemaje. Nikatega sikio huku kichwa kimemuelekea yeye hivyo siwezi kumuona. Mara nikasikia sauti zisizoeleweka nikataka kutoa sikio akanishikilia kichwa. Nikawa nahojiwa na mizimu kama inisaidie kufaulu n.k kisha nikasikia kama inasema niweke hela niliyo nayo pale. Nikageuka kwa kasi nikakuta jamaa ana microphone mdomoni ikabidi niipotezre kama sijaona kitu maana kwa watu pale. Ikabidi niseme sina hela isipokuwa mia mbili tuu. Basi nikaiweka hiyo miambili na kusepa.

Hadi leo siamini katika uganga.
 
Hahahahahahaha!! Waganga wengi ni wahuni tu
 
Jirani yetu binti wao alisumbuliwa na maradhi, walihangaika hospitali zote , yule dada ilikuwa akisafiri to the moon ni ugonjwa wakupoteza fahamu.

Mmoja wa Sangoma alisema binti analogwa na wazazi wake. Wazazi wenyewe waliblow mapigo .
haahaahaa uwiii..
ila nahisi huyo binti alikua anasumbuliwa na endometriosis
 
Back
Top Bottom