Wale tuliowahi kuingilia ugomvi wa wapendanao kwa lengo la kusuluhisha tukutane hapa. Nini kilijiri baadae?

MFALME WETU

JF-Expert Member
Feb 1, 2021
2,582
6,166
Nawasalimu kwa jina la mmu..

Kuna kisa kimoja cha mwisho kati ya vingi ambavyo nmewahi kukumbana navyo ningependa kuwashirikisha.. kilinitokea miaka miwili nyuma kipindi bado nipo chuo ambacho kilipelekea mpaka leo sitaki kuingilia ugomvi wa "wapenzi" hata nikikuta wanauana.

Kuna shemeji yangu mmoja [rafiki wa mpenzi wangu] alikua na mpenzi wake wa apoapo chuo, yeye alikua kamtangulia jamaa miaka miwili (manzi 3rd year, jamaa 1st year) ila diploma walisoma na kumaliza pamoja.

Sasa iko kijamaa kilikua ni kilevi cha kupindukia sana, kunywa pombe kali na bangi ndo ilikua pigo zake kila siku. Alikua na uwezo wa kukalisha Kvant au Konyagi Mbili Kubwa na Bangi pembeni peke yake.

Sasa huyo shemeji yangu alizama kwa jamaa ile mbaya, alikua anampost status kila dakika kila saa na vikapsheni motomoto vya mahaba kuonesha ni jinsi gani kakolea. ilifikia hatua akaamia kwa alipokua anakaa huyo bwanake na mazaga yake yote ya geto.

...........................................

Kuna weekend moja tumezamia Lounge usiku sana around 23:00hrs, muda naingia nikawapita wamesimama meza moja wanapiga vyombo nikawapa hi tukapiga stori mbili tatu nikawaacha nikaenda kukaa kwenye meza moja ivi ambayo huwa napenda kukaa siku zote nikiingia apo ipo angle flani ivi ukikaa unaona kila mtu anaeingia na kutoka pale ndani huku nikiwa navizia sleepover.

Bhana ee, nikiwa nmesimama pale nikisubiria B&W yangu nlokua nmeagiza wakati huo nmemkodolea macho denti mmoja ivi alietokea kunivutia nilitahamaki baada ya mshikaji mmoja alokua amekaa pembeni yangu kunishtua na kuninyooshea kidole kuashiria kuna taharuki imetokea upande huo kucheki nakuta ni couple nayoijua ikabidi kusogea eneo la tukio haraka sana.

Kufika pale nikajaribu kuwaachanisha na kuwacalm down kijamaa kimelewa chakari hakielewi kitu ikabidi Mabaunsa waitwe wamuondoe pale ndani. Nilimpatia shemeji yangu pullover nlokua nmevaa ili kumsitiri maana nilimkuta yuko almost kifua wazi kachaniwa nguo zote za juu nyonyo zinaning'inia nje.

Nilimtoa pale kwenye eneo la tukio nikamweka kwenye gari tulokua tumeenda nayo ya mshikaji wangu mmoja ivi chapombe sana alikua anapenda kunichukua nimdrive akienda kulewa.

Shemeji alikua amepanic sana huku kichwani nikiwa nawaza nampeleka kulala wapi nikapata wazo la kumpeleka kwa rafiki yake (mpenzi wangu) nikampigia simu akawa hapokei.. ilikua around sa 7 usiku, mawazo ya kishetani yakaniingia nikasema ngoja nimpeleke getoni kwangu.

Tukafika nilipokua nakaa tukashuka nikamwambia kwa leo utalala kwangu mimi ntaenda kulala kwa mshikaji wangu yule nlokua nmeondoka na gari yake akawa anaogopa akasema nisimuache peke yake nikamwambia basi ngoja nikamsubiri jamaa angu wa gari mpaka atakapotoka nimpeleke kwake ndo nirudi pia akakataa akadai kama ndo ivo turudi tukamsubiri wote then turudi wote geto maana alikua anaogopa kubaki mwenyewe nikasema poa.

Kufupisha story shemeji alilala kwangu kwa muda wa siku 3 pasipo mpenzi wangu kujua, nilimuuliza chanzo cha ugomvi wao pale Lounge akanambia kuwa alimkataza kunywa pombe nyingi maana jamaa alianza kunywa kuanzia asubuhi kitu ambacho kilipelekea jamaa kumtamkia shemeji maneno machafu kuwa ni "malaya na ana Ukimwi" ndo ugomvi ukaanzia apo.

Kwenye izo siku alizokua analala kwangu, alikua anapanga namna ya kwenda kuchukua vitu vyake kwa jamaa maana alikua anaogopa mshikaji anaweza kuvikatalia au kuchezea tena kichapo ikabidi nimuunganishe na jamaa angu mmoja yupo FFU pale wilayani tulisoma wote chuo kimoja ila alinitangulia mwaka mmoja nikampatia namba ya shemeji yangu kesho yake wakaenda wakachukua vitu bila shida yoyote akavihamishia kwa rafiki yake.

............……................…...........

Ukistaajabu ya musa utayaona ya firauni.

Baada ya ule mkasa haikupita ata wiki mbili kuna siku naview status nikakuta kampost huyo alokua Bwanake nikaduwaa sikutaka kumuuliza nikaamua kukausha badae rasmi nikasikia kwa mpenzi wangu kuwa wamesameheana na wamerudiana aisee nilishangaa sana.

Tulivomaliza chuo siku ya graduation pia naskia waligombana Manzi kioo cha iPhone 11 pro yake kikapasuliwa hadi leo hii hayupo online lakini naskia wanakaa wote mpaka sasa na manzi anabugia bangi na pombe kali mbaya mbovu.

Since then niliapa siwezi kuingilia mambo ya watu ambao washaonana nyuchi zao / wanajifunika duvet moja. Never.!!

Poleni kwa gazeti japo nimejitahidi sana kufupisha.

Tupe experience yako ilikuaje
 
........na ushukuru Mungu kama shemeji yako hakumuadithia Jamaa yake kwamba wewe ulihusika kuwaachanisha Kwa kutoa sapoti ya polisi kuchkua vitu Kwa Jamaa.....
 
nmefupisha tu stori mkuu ingawa shemeji hakumwambia direct ila jamaa alivoona mambo ya polisi alijua tu ninahusika, alinitafuta kunambia nilvofanya sio poa nikamwambia mimi nilitoa tu namba pasipokujua lengo la shemeji.

Sirudii tena
 
Nimesoma hapo Tupe experience yako. Ilikuaje

Ningeandika ila sijui experience ya nini
 
Back
Top Bottom