Kwa wale introverts, anti social, na shy people maisha yako ya chuo yalikuwaje? Vipi mtaani kukoje?

Mimi ni kama introvet lakini wa aina yake

Kwanza naishi na watu, wasipokuwa wananiongelesha na mimi siongei, ila kama ni waongeaji na mimi nakuwa muongeaji hadi basi

Nikiwa sina hela nyingi kuliko majirani au marafiki zangu huwa sijiamini mbele yao, napenda kuwa na marafiki ambao nawazidi uwezo au angalau tuliolingana,ndio nakuwa comfortable

Siboreki kuwa na watu as long as hao watu watakuwa na story na interest ambazo nazipenda pia, mfano burudani zetu zinaendana, mitazamo kuhusu uchumi, biashara, siasa, Dini, malezi, mahusiano n.k au angalau awe intellectual ambaye tukitofautiana mitazamo tunaweza ki argue kwa fact za kisomi

Watu wanaopiga story za mara Diamond, Harmonize, wema, wasafi, demu yule nimetembea nae n.k, huwa siendani nao,

Napenda sana kufanya kazi muda mwingi na kuingiza hela, kuliko kuzitumia

Nyimbo hii ya G-Eazy& Bebe Rexa ya Me, Myself and I niiliipenda kweli, iliendana na life langu sana
Nai dedicate kwa ma introverts woote wa JF


 
Mimi ni introvert lakini kwenye ulazima naweza kujichanganya na kundi la watu. Kwenye discussion sipendi kuwepo ila ikinibidi basi nitahakikisha nashiriki kikamilifu sababu sipendi kukaa kivivu. Naweza sema wakati mwingine nakuwa kama extrovert.

Katika kutaka kujifahamu zaidi nilifanya personality test ya Myers & Briggs na nikaangukia kwenye INFJ-T. Kwa sehemu kubwa sifa zake ndizo ambazo ninazo. Napenda jinsi nilivyo ingawa kuna mambo ambayo yananiwia vigumu sana kuyafanya vinginevyo nijilazimishe.
 
Wewe umetisha

Unataka kuwa Bora kuliko wenzako utao wazunguka

Unaishi maisha ya tabu sana.

Sasa hela unamjuaje mwenzio hana hela kuliko wewe?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mzee siishi maisha ya tabu kwa kuwa kipato changu pia ni above average ya watu wengi mjini, hii ni moja ya vitu vinavyonisukuma kuwekeza zaidi

Nilivyokuwa nasoma nilikuwa hivi hivi, moja ya vilivyonifanya kuwa wa juu darasani mara nyingi
Mtu sio lazima awe nimemzidi exactly, ila hata tukilingana tu poa
Mi sioni poa kuishi na watu wanaobadili magari mara kwa mara halafu ukute mimi uwezo wa kumiliki baiskeli sina, hawa unakuta nina uhusiano nao wa kikazi ila sio close sana
 
Yaani huyu Ni Mimi.
I'm enjoying staying myself rather than being with people (friends)

Sent using Jamii Forums mobile app
kama mm tu rafiki ninao wachache na tena wakianza kuniseng'enya na kunipiga majungu ndo najitenga nao kabisa.
NB.Nainteract na watu tunaoendena interest mf siasa,muziki au misimamo ya dini.

God doesn't require us to succeed,he only requires that you try
 
Mimi binafsi nateseka sana nikikaa sehemu zenye watu wengi, nilikuwa nafanya kazi sehemu, asilimia kubwa ya watu walikuwa extrovert basi nilipata tabu sana,maana walikuwa wananisema,wanahisi nina stress, wengine mpaka wakishauri labda niende kwa psychologist...
hali usipoizoea inatesa sana hasa ukiwa unaishi au unafanya kazi sehemu yenye muingiliano wa watu wengi
 
KING 360, Mimi tangu primary hadi namaliza chuo life style ilikuwa ni rafiki mmoja au wawili tu shule nzima au chuo kizima nilikuwa mkimya mno hadi nikabatizwa "tabasam adimu" maana ilikuwa nadra sana kuniona nikitabasamu...

Mbaya zaidi ilikuwa naweza kaa hata mwezi mzima sijaongea na mtu yeyote darasani!....

Maisha yangu social kitaa ni mimi na chumbani, chumbani na mimi tu mara nyingi sana mtaani wengi hawanijui maana kuonekana ni nadra sana...

Ili tuongee basi hapo labda uanze mwenyewe kunisemesha ama niwe na shida kubwa vinginevyo navunga.

Nachelea kusema huenda tabia ya kujitenga na kutopenda kusocialize ilichochewa zaidi na changamoto ya kusikia niliyoipata nikiwa darasa la tano..

Kimahusiano nilifanikiwa kupata mchumba ambaye alijitoa kwenda na mimi hivyohivyo ingawaje haikuwa ridhiki kazalishwa kwingine na anaendelea na maisha yake mengine...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom