Jinsi unavyoweza kuhatarisha maisha yako marafiki zako na jamaa zako kwa kutumia mitandao ya kijamii

ikindo

Senior Member
Nov 29, 2011
132
110
Mitandao ya kijamii kama facebook, instagram, badoo nk ni mitandao amabayo imejipatia umaarufu mkubwa sana hasa katika nchi za dunia ya tatu kwa siku za hivi karibuni.Umaarufu wa mitandao hii umetokana na tabia ya asili ya umbea ya wakazi wanoishi kwenye dunia ya tatu na kujikuta wakipost vitu ambavyo vimekua vikiwaharibia maisha yao kwa kiasi kikubwa bila wao kufahamu na kupata madhara ya muda mrefu yanayoweza kupelekea matatizo ya kisaikolojia ama hata kifo. Sababu ya pili iliyofanya mitandao hii kuwa maarufu zaidi ni kushuka kwa bei ya simu janja (SMART PHONES) hivyo kupelekea upatikanaji wake kuwa rahisi zaidi na kupelekea watumiaji wengi kuweza kumiliki simu hizo na kujiunga kwenye mitandao hiyo ya kijamii bila kuwa na elimu sahihi juu ya malengo na madhumuni ya kuwepo kwake hivyo kujikuta wakipost vitu ambavyo sio tu vinawafunua wao binafsi bali pia jamaa zao na mataifa yao kwa ujumla na hivyo kupelekea mmomonyoko wa maadili Machafuko, Utekwaji, na udahalilishaji katika taifa. Kwa mfano ni jambo la kawaida siku za hivi karibuni kumkuta mtu amepiga picha ya utupu, ama nusu uchi ama kaburi kwenye hizi nchi za jumuia ya tatu na kuandika status kwenye mtandao wa kijamii guu la bia, kiuno nyigu ama ndo tunazika sasa, ama mtu anampongeza mke wake, mume wake ama motto wake anaekaa nae nyumba moja kwenye mtandao wa kijamii, ama mtu anamtukana jirani yake kwenye mtandao wa kijamii, ama mtu anakula chakula cha jioni halafu anaandika status inatokea sasa hivi (It is happening now) na mambo kadhaa ya kushangaza bila kujua kuwa hayo ni mambo yake binafsi na yalitakiwa kuendelea kuwa binafsi.

Mimi nadhani matumizi bora ya mitandao ya kijamii ni kama kutangaza biashara ama ujuzi wako ili uweze kufahamika na labda ikuletee tija.

Ushauri wangu ni kuwa jamii yetu pamoja na utamaduni wetu wakutopenda kufanya kazi na kujikita zaidi kwenye mambo ya umbea ni lazima tutambue kuwa unapoweka kitu kwenye mtandao inamaana umekiweka ili kila mtumiaji akione hata kama ni chako binafsi wazungu wanasema (Once online it is there to stay) ina maana mtoto wako ambaye hata bado hajazaliwa siku akikua hata kama wewe umefariki anaweza kuona vitu vya hovyo ulivyokua unaposti. Mimi nikiamua kuwa mwizi na kwakutumia taaluma yangu ya kuzifahamu tekinolojia mbalimbali za mawasiliano ninaweza kukuibia kutokana na information zako unazoziweka mtandaoni kwa kutumia ukandarasi wa kijamii ama (Social engineering), mtekaji anaweza kukuteka, Majasusi na watu wenye husda ni rahisi kuifanyie nchi yetu ujasusi kwa kutumia taarifa tunazopost kwenye mitandao ya kijamii kwa kutumia teknolojia ya (big data mining) na kizifanya nchi zetu zisiendelee kiuchumi kwa sababu ni rahisi kukusanya taarifa za uelewa wa watu wan chi fulani kwa kuanza kukusanya taarifa zao kwenye mitandao ya kijamii ka facebook, instagram, watsapp, badoo n.k

Pia ningependekeza serikali iongeze maradufu kodi za simu janja (smart phones) ili zisiwafikie watu wengi zaidi na kuleta matatizo kama hayo niliyoyataja hapo juu.
 
Lakini mbona Hata kwa wale wa ulimwengu wa 1 sijui Ndio walio endelea mbona na wao wanafanya mambo Kama hayo?? Utaona status sick,angalia anachokifanya Dj khaaled...kafungua Acc ya mtoto wake anaiendesha yeye mwenyewe and anaandika Yale maneno ambayo as if yamesemwa au kuandikwa na mtoto mwenyewe. Beyonce katuonyesha Picha za ujauzito wake,tunajua wapenzi wapya wa celebrates and superstars kupitia social networks and a lot of things,so.mi naona tuache ushamba na tuelewe hii dhana ya utandawazi. That's all
 
Eti nashauri Serikali ipandishe kodi zaidi ili smart phones zisiwafikie watu wengi, huyu jamaa sijui katokea wapi
amesahau kwamba hizi simu zimekua kama ofisi kwa wengine


watu wanafanya biashara online kupitia hizi simu

mleta mada kila kitu kina hasara na faida

usiangalie upande mmoja wa hasara tu
 
Nimependa tahadhari yako kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii ila kumbuka kuwa mitandao ya kijamii ina faida zake pia. Hivyo badala ya kudhibiti matumizi yake ni vyema watumiaji waelimishwe matumizi sahihi ya mitandao hii.
 
hapo mwisho umeharibu,yani kwakuwa magari yanasababisha ajali sana basi yatozwe kodi kubwa ili watu washindwe kuyanunua?au barabara za lami zisijengwe kwasababu wenye magari watapita kwa kasi na kusababisha ajali?
 
Isitafutwe sababu tu hata ndogo ikawa ndio justification ya kukamilisha agenda Fulani.

Hii mitandao ya kijamii ni taswira ya maisha yetu. Hii mitandao ni nyenzo tu ya kuoneshea huu uharibifu wa maadili. Kufungia mitandao au monitoring hakutasaidia kutufunza uzalendo,uadilifu wala maadili na utamaduni wetu.

Watu wabadikike ki fikra,nguvu inayotumika kwenye kufungia mitandao ielekezwe kwenye kutoa elimu ya namna bora ya kutumia mitandao na tehema kwa ujumla kama njia ya kupata elimu na habari.
 
Hiyo aya yako ya mwisho naomba uitoe.

Kwakuwa ulichoshauri hapo sio suluhisho la matatizo uliyoainisha huko juu kwenye aya nyingine.
 
Mimi nadhani matumizi bora ya mitandao ya kijamii ni kama kutangaza biashara ama ujuzi wako ili uweze kufahamika na labda ikuletee tija.

Hapa uko sahihi kabisa, nadhani ndilo kusudi kubwa la mitandao.
 
Ni kweli unachoongelea ila hakuna maendeleo yatakayokuja bila kuwepo kwa changamoto, kwahiyo just embrace the benefits na hizo changamoto zifanyie kazi kwa namna ya uelewa wako. Huwezi zuia kila kitu,hiyo ipo tangu na tangu.
 
Back
Top Bottom