Kwa wakubwa tu: Kasheshe ya FUNZA kanda ya Magharibi

Inasemekana kwamba funza huendana na uchafu. Usipouweka mwili wako katika hali ya usafi ni rahisi kuvamiwa na funza. Uvivu wa kutoa funza nao huchangia funza hao kuzaliana mwilini mwako. Ukiwa na funza mmoja tu lazima utagundua kwa sababu atasababisha mwasho sehemu aliyojichimbia. Ukidharau na kumwacha basi nae anajua amepata msamaria mwema hivyo ataita na ndugu zake na kufanya makazi ya kudumu miguuni mwako. Wasamaria wema zaidi huwakaribisha vunza hata kwenye mikono yao! Viatu vinasaidia sana kuzuia funza kama ilivyoelezwa hapo juu, lakini muhimu zaidi ni usafi wa mwili, maana huwezi kuvaa viatu kama miguu yako ni michafu. Vile vile funza ni ugonjwa wenye tiba tena tiba rahisi, lakini baadhi yetu labda kwa sababu ya kubanwa sana na majukumu ya maisha, au ujinga au umasikini au vyote, tunapuuza kupata matibabu.

Nisahihishe kidogo tu kwamba funza si ugonjwa, kinachotokea ni kupata vijeraha unapowatoa funza mwilini, kama ni mmoja si tatizo ila ukiwaacha wakiwa wengi ndio unapata vidonda kwani unabaki na vishimo kila ulipotoa funza. Na kwa kweli hata ukiwa msafi unaweza kuingiwa na funza kwani huingia akiwa mdogo sana halafu anakuwa ndani ya ngozi, ukimwahi kumtoa si tatizo, ila ukiwaacha unaweza hata kulazwa hospitali.
 
Kuna baadhi ya maeneo hapa Tanzania ukienda na viatu unapewa uongozi fasta
Umenikumbusha shule ya msingi niliyosoma huku kijijini kwetu tulikuwa miguu peku shule nzima, basi siku nimevaa viatu mfululizo kama mwezi nikapewa ukiranja wa afya
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom