Infopaedia
JF-Expert Member
- Oct 28, 2011
- 1,231
- 1,489
Ilikuwa ni research ndogo. Nipo kazini mida ya saa tano. Nachukua simu yangu ya kiganjani naandika ujumbe...'Hi baby, niko busy sana, naomba saa saba unishtue niende lunch. Mis u already'. Baada ya kuandika hivyo, natuma ujumbe huu kwenda kwenye number mbili. Moja ya wife, ya pili ni mchepuko. Guess what!!!!! Saa saba on dot, simu inaita. Kuangalia ni mchepuko. Nikapokea nikaambiwa nikale. Naenda kula huku attention yote ikiwa kwenye simu, nijue my wife wangu kachelewa kwa dakika ngapi. Nimekula, nimemaliza, nimerudi ofisini naanza kazi, still attention ipo kwenye simu. Saa nane na nusu inainggia msg.....'umeshakula?'. Wakezetu badilikeni jamani.