Kwa utapeli huu tuwe makini katika kutuma pesa

Kwa utapeli huu tuwe makini katika kutuma pesa

Alikuja kavaa Jeans... sasa huo si ukosefu wa adabu? Kibaya zaidi alikaidi agizo langu la kunisaidia kushika mkongojo wangu...
Pole Babu, tutamuhoji kwenye kamati yetu ya maadili kwa jambo hilo alilolifanya na sheria itachukua mkondo wa bahari yake
 
juzi wamenipigia matapeli wengine wakisema wanauza matrekta na wanataka waniunganishe,mara baada ya kupokea simu nikawa nimeshatambua ni watu wa aina gani,nilivyowapiga logical questions wakakata simu haraka sana,hawa wanawaweza watu ambao hawana huelewa na technologia na uelewa wa ujumla kuhusu maswala ya money transactions,cha msingi tuwe makini sana,na kwa kuwa hapa jf watu wengi huwa wanatoa hushuuda ni rahisi kujifunza zaidi kwani jf ni darasa zuri zaidi.
 
Cha kujiuliza.
1. Wakala anajulikana kwa namba ya uwakala, na si yenye mpangilio kama wa namba yako wako.
2. Utaambiwaje utume pesa kwa "wakala" usiyemjua? Kwanini asikuambie uende kwa wakata ufanye kama unatoa hela?
3. Umetumiwa hela, OBVIOUS ni kwamba ulikuwa na ahadi na mtu au kuna mtu unamdai utaanzaje kutuma hela kwenda namba usiyoijua? Kama kuna mtu akatuma kimakosa,
Mtandao husika ndo huwa unatoa hela kwenye akaunti yako na kuiwekwa kwa aliyekosea.


Tuwe makini
Ninakutafuta were ulipoteleawapi
 
Pole sana kwa hilo sekeseke ilaa siku hizi wamejaa sana,wapo na walikuwepo inanirudisha enzi nipo sekondari nilipigwaga changa na haoo watu toka siku hiyo mimi nikawa mchangamfu mno upole tupa kuleee nikiwa barabarani
 
Mie bado sijaelewa huyo tapeli anajuaje Kama umeingiziwa pesa
 
Hawa ngedere wanatoa wapi namba zetu

IMG_20180420_094223_548.jpg
 
Ni wajinga ndio huweza kutapeliwa kizembe hivi hata mie nilipokea Ujumbe kama huo nikaupuuzia, maana Hata huo mwandiko
Screenshot_20180420-083833.jpg
 
Habari,wanajamii jana kuna suala ambalo limenigusa sana na si mara moja kutokea bali ni mara ya pili juzi kuna ndugu yangu alitumiwa pesa kwenye mtandao fulani wa simu alipoipokea ile pesa haukupita muda alitumiwa meseji nyingine iliyomtaka arudishe pesa kwa wakala maana ilitumwa kimakosa,yeye hakuirudisha ile hela ila ilipofika jioni alianza kupigia simu watu wake wote ambao alikuwa na ahadi nao ya kulipana hela ndipo kuna mmoja akamwambia nilikutumia kiasi fulani asubuhi.

Hapo ndipo jamaa aliposhtuka kama ule ulikuwa ni utapeli Jana mimi nilitumiwa pesa kwenye mtando uleule kama anaotumia ndugu yangu ambapo baada ya kutumiwa pesa nikapokea meseji nyingine inayonitaka nirudishe pesa kwa wakala haraka maana namba ilikosewa kwasababu nilifahamu huu ni utapeli nilipiga namba ya huduma kwa wateja na keeleza yaliyonisibu kwakifupi waliniambia pole sana na siku nyingine niwemakini.

Swali nililojiuliza je,kama ningetapeliwa kweli fedha zangu zingerudi na kama wangenitapeli hawa watu ni untouchable na si rahisi kuwapata? Namba zinazoonekana kwenye hiyo picha ni namba za hao matapeli na hiyo meseji walionitumia msaada kwa wataalamu wa mambo View attachment 750502
Huyo tapeli ni mwanaume wa Dar
 
nikishagundua hivyo hela naitoa chap chap, hamna kuwasiliana nao tena
 
yaani hawa matapeli ni wajanja na katili hata 5,000 wanaikomba wao hawajali ni ndogo au kubwa. Tuwe makini jamani
 
zingine zinakuja kwa mtindo huu

halafu wanategea ukiwa una mtu anakudai pia,sasa nikawapigia wote wanaonidai wanakataa sio wao nikaona
 

Attachments

  • 0B1835FE-10FA-452E-898D-493A873EA517.png
    0B1835FE-10FA-452E-898D-493A873EA517.png
    23.5 KB · Views: 30
Tupeane elimu wakuu.

Endapo angeituma hiyo hela jinsi alivyotakiwa kuirejesha, angeingizwaje mjini zaidi?
Pengine in reality hakuna hela iliyotumwa kwake,
bali ni sms ya kawaida tu so ukiwarudishia means unatuma zako wewe
 
hata mm nimetumiwa huo kwa namba tofauti na hizo,nihii inatokea mara tu ukiingiza hela kwa sim na nimtandao wa voda
 
Juzi kati, jamaa yangu kakwapuliwa simu, ilikua kipindi cha pasaka then mi nikiwa sijui, jamaa akani text na kuniuliza nilipo, nikamwambia mahali nilipo knowing nina chati na mshkaji wangu; akanambia hivi; "kuna biashara nataka nikuunganishie, inalipa balaa but please usinisahau" Mi nikamwambia poa, nipo mchongo, kanitumia namba Fulani hivi then nikampigia huyo jamaa, akanieleza vizuri sana kuhusu mambo ya madawa ya maji sijui kuondoa TOPE kwenye maji ili maji yatumike na binadamu; the way alivyo kua ananielekeza nikamstukia kwasababu 2, moja hiyo biashara niliisha wahi sikia watu wamelizwa but pili ni hivi, mi mwenyewe mtaalamu mzuri tu wa kuyafanya maji kua hivyo alivyo kua anasema na sikuona kama ni deal kiviile (kwa mujibu wa utalaamu wangu) then nikaona nimpe ushirikiano vizuri but again nikamrudia jamaa yangu (hapa sasa ni yule aliyekwapua simu) nikaona nimpigie; hakupokea badala yake akani text message Fulani hivi, kwamba yupo sehemu Fulani, huyu jamaa yangu namjua in and out, yeye sehemu hizo sio mwendaji hata kidogo ndio nilipo confirm kwamba nimekutana na matapeli, aise, jamaa walikua na bonge la msururu wa watu na yaelekea wana mtu kila mkoa hadi noma, yaani simu imeibiwa Dar but jamaa wana connection Kigoma, Tabora, Mbeya, Iringa na Dar yenyewe; well nisingekua busy I could catch somebody but mwishoni niwaambia tu ukweli.
 
Back
Top Bottom