Kwa ukweli wake huu ' Kuntu ' kabisa Mwanadada na Msanii Shilole ananidai ' Zawadi ' yake

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
38,625
2,000
" Wasichana nawahusia msikimbilie wanaume wenye hela mkawakataa wasio nazo na kuwadharau. Pesa zinatafutwa pendaneni saidianeni kufikia mafanikio. Pengine wewe ndio mwenye ule ufunguo wa yeye kupata " Shilole.

Tokea nimfahamu huyu Dada sijawahi ' Kumchukia ' bali nimekuwa nikimpenda mara kwa mara kwakuwa hana Unafiki, ni Mkweli siku zote na haishi Maisha ya ' Video / Kaole / Kisanii ' bali anaishi Maisha yake halisia na pengine ndiyo maana hata Mwenyezi Mungu kila uchao anazidi kumnyooshea njia yake ya Mafanikio.

Kibinadamu anaweza akawa na mapungufu yake kama ambavyo Mimi na Wewe pia tunayo yetu ila ni mmoja wa Wanawake ambao nawapenda kwa Ukweli wao na nadhani ananidai ' Zawadi ' kubwa na ya thamani Siku na Mimi nikizichanga na ' Uchumi ' wangu kuwa mzuri.

Amemaliza kila Kitu na nadhani si vibaya sana kama Wanawake wote wakamuelewa kwa huo ukweli wake ulio ' Kuntu ' kabisa na kuanzia sasa wakabadilika na wayaishi hayo maneno ya Msanii wangu ' pendwa ' kabisa Shilole. Mwanaume ambaye anaishi na huyu Dada ( Shilole ) nampongeza na namuambia rasmi kuwa amepata Mke mwema, mpambanaji na mzuri kabisa hivyo asimtende bali ampende na amtunze vyema.

Mwenyezi Mungu akubariki sana na mno Dada yangu Msanii Shilole.

Nawasilisha.
 

Omulasil

JF-Expert Member
May 5, 2015
3,540
2,000
Zamani nilikuwa niweka verse zangu kama hizi walikuwa hawaruki lazima nibanjue siku hizi mashairi kama haya nimeyasahau maana najua hawa wenzetu ili umvue kale ka ndani (pichu) we msifie mbona unafungua tu kipochi.
Japo wameanza ujasiriamali wa maku

Sent using Jamii Forums mobile app
 

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
3,771
2,000
Maskini Shilole hakujua kuna siku angegenzwa punchinbag ya uchebe. Kupotea njia ndio kujua njia
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom