Mnyamahodzo
JF-Expert Member
- May 23, 2008
- 1,932
- 985
Ujenzi wa majiji ya Dar es salaam, Tanga na Mwanza unahistoria ndefu sana. Yalijengwa polepole mwaka kwa mwaka. Lakini lililo la muhimu zaidi ni ubora wa vifaa vya ujenzi vilivyotumika.
Majengo ya zamani kabisa katika Majiji ya Tanga na D'salaam yalijengwa kwa mawe na matumbawe na mengine kwa tofali za kuchoma huku nguzo na migamba ikiwa ni ya mikoko na mivinje iliyokomaa hasa.
Ulipokuja ujenzi wa kutumia tofali za simenti (blocks), tofali zake zilikuwa ni imara sana kutokana na aina ya sementi, kiasi cha mchanganyo wa sementi na mchanga na pia idadi ya siku tofali lilizolazwa katika maji. Majengo ya maghorofa yalijengwa kwa tofali bora pamoja na yale ya kawaida (ofisi na nyumba za viongozi).
Watu binafsi nao walipenda kuwa na tofali bora kama za MECCO au TACONA. Baada ya kipindi kigumu cha kiuchumi ndipo wananchi wakaanza kuchakachua vipimo vya sementi: mchanga na utiaji wa maji.
Ukiingia Tanga, Mwanza na Dar utaona majengo ya toka 1950 hadi 2000 yaliyo katika ubora wake.
Ninachokiona kwasasa Jiji Dodoma majengo mengi kujengwa kwa pupa. Tofali zinazotumika ni za ubora wa chini..hakuna kampuni rasmi yenye kuzalisha tofali bora. Nyingi ya tofali ukinyanyua usawa wa kiuno na kudondosha zinavunjika; ukisugua kwa kijiti zinapukutika upesi. Ni tofali zenye mchanganyiko mmbovu wa mchanga na sementi. Ni tofali zisizokunywa maji ya kutosha.
Majemgo mengi misingi yake ni mifupi bila kuzingatia kuwa mwamba wa maji (water table) wa Dodoma hauko chino sana. Matokeo yake, mwaka mmoja toka jengo lisimame utaona msingi unaanza kumong'ong'onyoka na sakafuyingi kutoa sauti tofauti tofauti unapokanyaga juu yake.
Kama TBA na Halmashauri ya Jiji la Dodoma hawatachukua njia za makusudi katika kudhibiti uzaloshajina utumiaji wa vifaa vya ujenzi vyenye ubora wa chini, iko hatari hatari hata maghorofa yanayojengwa sasa baada ya miaka miwili kuwa na nyufa na mengine kutakiwa kuvunjwa baada ya miaka 10 hivi.
Nawasilisha.
Kwa kuandika hivi haimaanishi katika kipindi cha miaka ya karibuni hakuna kabisa majengo yaliyojengwa kwa viwango.