KWA UFUPI: Gwantanamo bay Cuba.

The Certified

JF-Expert Member
Feb 10, 2016
910
773
d8ad7de0e1e3efb2cfedb83c4d30d0e9.jpg

Ramani ya Guantánamo Bay
Wafungwa walipofika mwaka 2002
Guantanamo Bay au Hori ya Guantanamo (kwa Kihispania Bahía de Guantánamo) ni hori ya Bahari ya Karibi inayoingia kusini mwa kisiwa cha Kuba yenye upana wa km 20 na urefu wa km 8.
Kituo cha Kijeshi cha Marekani
Historia ya kituo
Ni pia jina la kituo cha kijeshi cha Marekani chenye eneo la km² 117,6 kilichopo kwenye kisiwa cha Kuba. Eneo hili lilikodishwa na Kuba kwa Marekani mwaka 1903 kwa muda wa miaka 99. Wakati ule Kuba ilitwaliwa na wanajeshi Wamarekani baada ya Vita ya Marekani dhidi Hispania ya 1898. Marekani ilidai kibali cha Kuba kwa utawala kwake juu ya Guantanamo Bay kama sharti kabla ya kuondoa jeshi lake.
Kwa sababu hiyo serikali ya Kuba ya mapinduzi ya 1958 haikutambua tena mapatano haya kwa sababu inadai Kuba ililazimishwa kijeshi kukubali.
Matumizi ya kituo
Marekani imejenga bandari ya kijeshi pamoja na uwanja wa ndege na huwa na kikosi cha askari 9,500. Kuna ukuta na fensi ya kutenganisha kituo na maeneo chini ya serikali ya Kuba.
Kambi ya wafungwa maalumu tangu 2001
Tangu mwaka 2001 kambi la wafungwa limejengwa kituoni lenye mnamno wafungwa 1,000 hasa kutoka Afghanistan waliokamatwa baada ya mashambulio ya kigaidi ya 11 Septemba 2001 katika Marekani na vita katika Afghanistan iliyofuata. Marekani ilipeleka hapa watu waliokamatwa Afghanistan na penginepo duniani wanaoshtakiwa kuwa magaidi wa Al-Qaida au Taliban lakini ambao hawakuwa bado na kesi mbele ya mahakama.
Utaratibu huu ni nje ya sheria za Marekani na haulingani na sheria za kimataifa kuhusu kuwatendea wafungwa wa vitani.
Nchi nyingi dunani zimepinga kuwepo kwa makambi haya na kudai wafungwa watendewe ama kama wafungwa wa vita au kupelekwa mahakamani kama magaidi.
Mwaka 2007 ni bado zaidi ya wafungwa 500 kambini.
Donald Trump asema wafungwa hawafai kuachiliwa Guantanamo Bay
Rais mteule wa Marekani Donald Trump amesema wafungwa zaidi hawafai kuachiliwa kutoka kwa gereza la Marekani la Guantanamo Bay, Cuba.
Amesema wafungwa waliosalia gerezani humo ni "watu hatari sana na hawafai kuruhusiwa kurejea kwenye uwanja wa mapigano tena".
Rais Barack Obama alikuwa ameapa kuwa
angefunga jela hiyo kabla ya kuondoka madarakani na amewahamisha wengi wa wafungwa waliokuwa wakizuiliwa humo.
Kwa sasa, wafungwa 60 wamesalia gerezani na ikulu ya White House ilisema baadaye Jumanne kwamba inapanga kuwahamisha wafungwa hao kabla ya tarehe 20 Januari.
Bw Trump alikuwa amepinga mpango wa Obama wa kufunga jela hiyo wakati wa kampeni.
Mwezi Februari alisema: "Asubuhi hii, nimemtazama Rais Obama akiongea kuhusu Gitmo, sawa, Guantanamo Bay, ambayo kusema kweli, ambayo kusema kweli, hatutaifunga.
"Tuaicha iendelee kutumika... na tutawarundika watu wale wabaya huko, niamini mimi, tutawaweka watu wengi huko."
Mnamo 17 Desemba, vyombo vya habari Marekani viliripoti kwamba Pentagon inapanga kuwahamisha wafungwa wengine 17 siku chache zijazo.
Bw Obama ameidhinisha kuhamishwa kwa wafungwa lakini Bunge la Congress ambalo linadhibitiwa na chama cha Republican limewekwa masharti mengi.
Bunge hilo linaitaka wizara ya ulinzi kutoa taarifa kuthibitisha viwango vya kiusalama vimetimishwa angalau siku 30 kabla ya hatua kama hiyo kuchukuliwa.
Nchi kadha zimewapokea wafungwa wa zamani wa Guantanamo, zikiwemo Ghana, Senegal, Umoja wa Milki za Kiarabu (UAE), Uganda na Cape Verde.
Watu 780 walizuiliwa Guantano tangu 2002, lakini kwa sasa ni 105 pekee waliosalia gerezani. Hamsini kati ya hao wameidhinishwa kuachiliwa huru.
Jela hilo ilijengwa na Marekani baada ya mashambulio ya tarehe 11 Septemba mwaka 2001 na hutumiwa na Washington kuwazuilia "wapiganaji maadui".
Gereza hilo hugharimu Marekani $445m (£316m) kila mwaka
Wafungwa wawili waliokuwa wakizuiliwa katika gereza la Guantanamo Bay, Cuba, wamehamishiwa Ghana.
Wizara ya Ulinzi ya Marekani imesema idhini ilitolewa kwa Khalid al-Dhuby kuachiliwa huru 2006 na kwa Mahmoud Omar Bin Atef mwaka 2009.
Wawili hao, wanaotoka Yemen, wamezuiliwa kwa zaidi ya mwongo mmoja na hawajawahi kufunguliwa mashtaka.
Ghana imetoa idhini kwa wawili hao kukaa nchini huko kwa miaka miwili, waziri wa mashauri ya kigeni wa Ghana Hanna Tetteh amesema.
Kwa mujibu wa stakabadhi za jeshi la Marekani, Mahmoud Omar Bin Atef ni raia wa Yemen aliyezaliwa Saudi Arabia mwaka 1979 .
Alikamatwa nchini Afghanistan 2001.
 
guantanamo imejengwa under alliens technoly..
ni technolojia kubqa sna...ndo mna mpka sasa maenjinia wengi dunia wnashindwa kuijui ramani kamaili ya Guantanamo Bay
 
mkuu mi binafsi nimeisoma yote lakini naona kama kiswahili hakijakaa vizuri... Kuna mistari unaandika bila kuhusisha ulipoishia..

Na kuna sehemu hazieleweki kabisa... Ol in ol thank you
Guugo.
 
Back
Top Bottom