Kwa sasa tutajua weledi na nguvu za January Makamba kwenye siasa nchini!

Ni vigumu sana kufurukuta
Jamaa ana vimeo.vingi sana tutammaliza within seconds!
Ana mkopo wa Bilioni moja kajichota Nssf,hajatoa maelezo zaidi ya kusema Musiba chizi
Ana NGO anajifanya ni kwa ajili ya masndeleo ya bumbuli,kumbe ni kichaka cha kutakatisha mabilioni ya pesa ambayo hayawafikii walengwa
Mkuu;
Tatizo la siasa za Tanzania huwezi kuchukua ni kweli kwa yote yanayosemwa.

Sikatai kuwa inawezekana unayosema ni kweli lakini kumbuka pia historia ina bainisha kuwa mengi yanayosemwa kuhusu wanasiasa wa Tanzania huwa sio kweli.

Nakumbuka kuna kipindi tulikuwa tunaambiwa kila jengo lefu nchini lilikuwa la Ridhiwani Kikwete. Kwa sasa husikii tena bali hoja zimehamishiwa kwa Makonda.

It's worth taking with a pinch of salt!
 
Embu muacheni kijana wa watu.. bora zimwi likuepukalo.! Kufanya kazi na Jiwe ni ngumu sana. Sasa atarelax na kujipanga vizuri.
Mkuu;
Sisi ni wapiga porojo tu!

Hatuna uwezo wowote kisiasa, kiuchumi na kijamii!

Kumbuka kama anataka a relax basi atangaze amechana na siasa kwa sababu mwanasiasa anategemea hisani ya wananchi ambao wana haki ya kumjadili.
 
Mimi sijawahi kabisa kumwona huyo jamaa kuwa ni mtu mwenye uwezo mkubwa. Kinyume kabisa na watu wengine wanavyomwona.

Namwonaga ni mtu mwenye uwezo wa kawaida tu kama tulivyo wengi.
Mkuu;
Kwa sasa ndio tutajua uwezo wake hasa kwenye mazingira ya siasa za sasa.

Kuna baadhi ya watu hawakubaliani na angalizo lako ndio maana nimeweka link ya thread ya Mdau akitoa sifa kwenye mada yangu ya kwanza.
 
Mkuu;
Hoja yako inataka tuamini kuwa Nape Nnauye ndiye mnasihi wa Makamba Jr!

Siamini kama ni kweli.
Nape anachokifanya sasa ni kushawishi wengine ili ionekane alionewa.Kuna siku alishawahi kutweet maneno yanayoashiria bila kundi lake CCM haitasimama.Kama umesikiliza kwa makini clip utagundua yeye ndiye "architect" na mratibu mkuu waraka,mara baada ya ajasambaza picha zake akiwa Mtama akicheza na "shangazi" zake
 
Ila amekosea sana kutoroka uapishwaji wa anaye chukua cheo chake.

Mwanaume angetia timu na misuti ya kiwaziri.. kaa mbele kabisa..

Ukipewa nafasi toa pongezi na shukrani na sifia sana.

Baada ya hapo unaendelea na mishe zako.

Ajifunze siasa za kina lowassa na kina mbowe.

Wanatukanwa sana lakini ukionana nao utadhani wamepoteza kumbukumbu.


Makambe usikimbie tatizo.. mwanaume anakabiliana na matatizo.
Hao ni watu soft sanaa huwezi kuwalinganisha na watu waliopitia nyakati ngumu km mbowe na lowasa.
 
Masumbuko lamwai, lawrence masha, kagasheki, mkama......... . ongeza wengine waliowekwa pembeni na siasa wakasahaulika kabisa kisha malizia na J makamba,Nape na sasa ongeza na wastaafu watakaopata tabu sana hahaaaaa Kinana,Makamba........ . Uroho wa madaraka uliopitiliza ndo unawaponza.
 
Nape anachokifanya sasa ni kushawishi wengine ili ionekane alionewa.Kuna siku alishawahi kutweet maneno yanayoashiria bila kundi lake CCM haitasimama.Kama umesikiliza kwa makini clip utagundua yeye ndiye "architect" na mratibu mkuu waraka,mara baada ya ajasambaza picha zake akiwa Mtama akicheza na "shangazi" zake
Mkuu;
Hoja yangu sio kushawishi kwa sababu suala la kushawishi kila mtu hushawishiwa bali wanaoshawishiwa wanakubali?

Vishawishi na washawishi wapo tu lakini la msingi ni kukubali au kukataa,
 
Nimeeleza ninachoona kinawezekana, na kuweka mipaka ya uwezo wangu kutabiri kwa uhakika, kwamba, pamoja na maoni yangu haya, usiende ku bet kwa maoni haya, halafu Makamba akafukuzwa uanachama, halafu ukamlaumu Kiranga.

Kwa sababu Magufuli haeleweki anataka nini, na hata sina hakika kama yeye mwenyewe anaelewa anataka nini.

Nimekuwa muangalifu baada ya kusema Bashe atachezea backbench sana bila appointment kwa kuwa ni "team Lowassa" mjuaji, lakini ikawa kama vile Magu kanisoma halafu kataka kunionesha hatabiriki, akamteua Bashe aondoke backbenchers za Bunge aingie serikalini.
Hahahaaa...eti Magufuli kakusoma kwa Bashe!
 
Mkuu nakupongeza kwa uchambuzi nzuri. Pia nakubaliana na ukweli kwamba samaki nje ya maji ndio mwisho wake na hii imethibiti kwa Lowassa na timu yake.

Lakini licha ya ukweli Huu, bado Kuna tofauti kubwa sana kufananisha tukio la Lowassa na tukio la January dhidi ya CCM. Vile vile Kuna tofauti kubwa Kati ya CCM ya Kikwete iliyomkabili Lowassa na CCM hii ya Magufuli iliyodhamiria kumkabili January.

Kwanza kabisa tukumbuke kuwa ingawa Napa alionesha kusudio la kumtoa Lowassa (samaki) ndani ya CCM (maji), bado Lowassa aliendelea na harakati zake ndani ya chama hicho mpaka alipoamua mwenyewe kukihama. Lakini Kuna Jambo la mazingatio hapa; kwanini tukio la kumfukuza Lowassa halikutimia Kama alivyotanabaisha Nape?

Kumfukuza Lowassa kwa kutumia "style" ya kumsukumia samaki nje ya maji Kama ilivyopeneekezwa na Nape isingeiacha CCM salama.

"Ku-deal" na Lowassa kulihitaji "akili kubwa" kutoka kwa magwiji wa siasa na si akili ya Nape ambaye alikuwa bado mchanga katika siasa. CCM ya Kikwete haikufanya papara na kutumia nguvu kubwa kupambana na Lowassa. Bali kwa kutumia ujuzi na uzeofu walionao kwenye siasa, 'walifanza subra" kumruhusu Lowassa atanye harakati zake huku wakijua wataweza kumkwamisha mahali Fulani tena mwishooooni kabisa Kama ilivyotokea kwa kutolipitisha jina lake kwenye mchakato wa Kura zamaoni. Lowassa hakuvuliwa uwanachama, Bali mwenyewe ndo alizira na kukimbilia upinzani akiwa na kadi yake ya CCM mfukoni.

Mbinu hii ya kumkwamisha Lowassa "dakika za lala salama" ilikuwa na UFANISI mkubwa kwa "usalama" wa CCM. Vinginevyo wangefanya papara kumfukuza uwanachama miaka hiyo ya 2012, kungempa wasaa Lowassa kujijenga dhidi ya CCM.

Ushindi Huu wa CCM dhidi ya Lowassa ilidhihirisha uwezo mkubwa walionao viongozi wake namna ya ku-deal na watu wasiotakiwa ndani ya chama.

Tunapoangazia CCM ya Sasa ya Magufuli na siasa zake dhidi ya wale wasiotakiwa tunaona ni tofauti kabisa na ilivyokuwa enzi za Kikwete.

Kwanza kabisa, Kikwete Kama Mwenyekiti wa chama hakuwahi kutoa kauli ya kudhihirisha kuwa Yuko "against" Timu Lowassa waliokuwa wanafanya harakati zao kushika hatam. Kikwete ni muumini wa demokrasia; si nje tu Bali Hadi ndani ya chama. Kikwete aliamini kwenye siasa za ushindani, kila mtu ana haki ya kufanya harakati ili ashinde.

Tofauti na Kikwete, Magufuli Kama Mwenyekiti wa chama hayuko tayari kuona mtu au kikundi cha watu wanafanya harakati za siasa dhidi yake. Watu wanafanya hivyo yeye anawachukulia kuwa wanamhujumu na mbinu pekee aliyonayo ya kushughulika nao si kufanya subira na kuwakwamisha mwishoni, bali ni kuwachafua, kuwasemanga waziwazi na kuwatema kwenye teuzi zake. Kiufupi Magufuli Hana uvumilivu, bali anadhihirisha chuki zake dhidi ya wapinzani wake.

Hayo yote tisa, udhaifu mkubwa wa Mwenyekiti huyu ni Ile hulka ya kujipa hati miliki ya chama. Yaani hana muda wa kukaa na wenzie ndani ya chama na kushauriana kufanya maamuzi ya mambo makubwa kwa usalama.wa chama. Badala yake anafanya maazi ya kukurupuka. Kiufupi jamaa anajitenga na mila na desturi za chama, bali anatumia nguvu ya cheo cha urais wake ku-dictate mambo ya chama.

Kutokana na utofauti Huu wa siasa za CCM ya Kikwete dhidi ya harakati za Lowassa na hii ya Magufuli dhidi ya akina Makamba, Nape, Kinana na Membe, ni vigumu kutarajia matokeo Yale ya samaki (Lowassa) kukosa nguvu nje ya maji yatokee kwa "game" ya sasa. Hofu yangu ni kwamba katika "game" ya sasa ambayo imeanza pamema, Magufuli ana "samaki" wengi wa kuwatoa "majini" nai wanaweza kumzidi nguvu ukizingatia Wana muda mwingi wa kujiandaa dhidi yake kuekea 2020.
 
Masumbuko lamwai, lawrence masha, kagasheki, mkama......... . ongeza wengine waliowekwa pembeni na siasa wakasahaulika kabisa kisha malizia na J makamba,Nape na sasa ongeza na wastaafu watakaopata tabu sana hahaaaaa Kinana,Makamba........ . Uroho wa madaraka uliopitiliza ndo unawaponza.
Mkuu;
Jaribu kuangalia kesi kwa kesi.

Unaweza kuwa ulichokisema kinaweza kutokea kwa Makamba Jr au kisiweze kutokea.

Kwa sasa tutajua ukweli wake.
 
H

Huyu dogo is not a political genius kama watu wanavyotaka kum-potray. Alibahatika kuzaliwa kwenye familia yenye connections ndio zimemfikisha hapo. Hana ujanja kama wa kina Mwigulu na Kigwangala. Hatapona nje mfumo.
Hawa wote wametembelea nyota za wazazi wao hawana uwezo wa kusimama peke yao.
 
H

Huyu dogo is not a political genius kama watu wanavyotaka kum-potray. Alibahatika kuzaliwa kwenye familia yenye connections ndio zimemfikisha hapo. Hana ujanja kama wa kina Mwigulu na Kigwangala. Hatapona nje mfumo.
Mkuu;
Nadhani angalizo lako litapata jibu sahihi sio muda mrefu.
 
Nguvu ya ccm iko ndani ya madaraka ya urais ambapo cheo cha mwenyekiti wake huwa na kofia ya amiri jeshi mkuu. Hapo ndio nguvu pekee ya wanaccm wote. Ukimtoa mwana CM yoyote ndani ya ccm ni nadra sana kufanya siasa akafanikiwa hasa hawa waliozaliwa 70s kwenda mbele. Huyo Januari hawezi siasa zozote nje ya siasa za mbeleko ya vyombo vya dola, na anaogopa jela kuliko hata kifo. Leo hii ccm ikitoka madarakani, wanaccm karibia wote watahamia chama kilichoko madarakani ambapo mbeleko ya vyombo vya dola itaendelea kuwa mbele yao.
Inawezekana Kuna ukweli kwamba dola no kimbilio. Mbowe anasimulia kwamba baada ya EL kuitwa aende polisi alimpigia Mbowe kwamba nifanyeje, Mbowe akasema tumeshayazoea we nenda tu, mzee alitetemeka. Hizi influence za familia pamoja na mbeleko zikidhibitiwa tunaweza kupata viongozi halisi.
 
Umenichekesha sana kwenye aya ya mwisho.

Kwamba jamaa amekusoma halafu akajisemea ngoja nimuoneshe huyu anayedhani ananijua.

Mimi nilianza kujaribu kumsoma mwanzoni ili nipate mwelekeo/mpangilio wake kiutendaji lakini baadaye nikaacha kutokana na moja ya sababu ulizozisema.

Ninachojua tu ni kuwa ukitaka kupambana naye basi lazima uelewe kuwa hawezi kukaa kimya lazima atajibu mapigo kwa maneno au vitendo, Hoja ya msingi ni mapigo gani atajibu.
Bashe kapewa mtihani mkubwa kutuonesha kwamba yale aliyokuwa anayasema Bungeni si nadharia tu ambazo zikipewa mtihani ambao Kiingereza unaitwa "realpolitik", zitashindwa kutekelezeka.

Magufuli kamuona Bashe mchawi anamuwangia kwa kuisema sana serikali yake.

Akafanya kama Waswahili walivyosema.

Mchawi mpe mwana alee.

Yani kasema wewe Bashe si una ideas nyingi sana za kukosoa serikali? Chukua kiti fanya kazi tuone.

Sasa hapo ndipo utakapoona kama serikali inahitaji mtu mwenye ideas nzuri tu, au zaidi?
 
Back
Top Bottom