Kwa sasa tutajua weledi na nguvu za January Makamba kwenye siasa nchini!

Huyo Makamba wala sio smart kihiiivyo mnampamba tu, kilichombeba ni historia ya familia na platform alioipata, hata ungekua wewe ungepata hiyo platform ungeshangaza dunia
Mkuu;
Kwa sasa tutajua kama kweli historia ya familia na platform alizopata ndizo zilimbeba mpaka kufika hapa alipofika.

Tunakoelekea ambako sio mbali tutapata hard fact.
 
Bashe kapewa mtihani mkubwa kutuonesha kwamba yale aliyokuwa anayasema Bungeni si nadharia tu ambazo zikipewa mtihani ambao Kiingereza unaitwa "realpolitik", zitashindwa kutekelezeka.

Magufuli kamuona Bashe mchawi anamuwangia kwa kuisema sana serikali yake.

Akafanya kama Waswahili walivyosema.

Mchawi mpe mwana alee.

Yani kasema wewe Bashe si una ideas nyingi sana za kukosoa serikali? Chukua kiti fanya kazi tuone.

Sasa hapo ndipo utakapoona kama serikali inahitaji mtu mwenye ideas nzuri tu, au zaidi?
Ulichokiandika nakubaliana nacho.

Hata Rais Magufuli alichokuwa anamwambia kina maana ya hiki ulichokiandika.
 
Umenichekesha sana, kwa sababu sijamsikia alivyosema na huwa simsikilizi Magufuli siku hizi.

Nikimsikiliza muda mfupi tu ananichafua mawazo.
Mkuu;
Ni kweli kumsikiliza Rais Magufuli huku ukiwa makini sana ni kujipa kazi ya bure, lakini usiache kumsikiliza.

Achilia mbali Rais Magufuli, hata kichaa kuna wakati anaweza kusema maneno yenye mantiki kama utakuwa unamsikiliza!

Hata saa mbovu kwa siku husema kweli!
 
Mkuu;
Ni kweli kumsikiliza Rais Magufuli huku ukiwa makini sana ni kujipa kazi ya bure, lakini usiache kumsikiliza.

Achilia mbali Rais Magufuli, hata kichaa kuna wakati anaweza kusema maneno yenye mantiki kama utakuwa unamsikiliza!

Hata saa mbovu kwa siku husema kweli!
Sijamuweka kwenye ignore list bado. Rais wa nchi si rahisi kumpotezea hivyo.

Ila hayupo katika vipaumbele vyangu vya watu wa kuwasikiliza.
 
Umaarufu wa January ulitokana na kubebwa na watawala,si kwa juhudi binafsi

Nakubaliana na wewe...vijana wengi wamebebwa tu...they are not that much intelligent ..wana bahati ya kuzaliwa katika familia hizo, na sasa wamejaa majivuno na 'uhuni'...wewe umetumbuliwa halafu unapost picha ukiwa na mzee Mwinyi..what is the meaning of that ??!!!
 
Influence ya Makamba ni Twitter
Hili linaweza kuwa na ukweli kiasi, lakini zaidi ni kwa wabunge au wanasiasa wa CCM wanakuwa na wigo mdogo wa wao kujulikana katika jamii kubwa ya watanzania kutokana na uwoga na mtindo wa chama chao kutosemea sana ukweli wa hali za wananchi hasa kwenye mambo yanayoonyesha sura mbaya ya serikali.

Mfano watu kama Zitto, Mdee,Msigwa na wengine wanajulikana hadi nje ya majimbo yao(kitaifa) Nimefikiri zaidi bila hii mitandao ya kijamii hali ingekuwaje kwa wanasiasa wengi wa sasa?
 
Siamini km makamba ana nguvu na ushawishi, sitegemei muujiza wowote toka kwake km ikitokea akafukuzwa uanachama. Huyu mimi namwonaga ni km mwanasayansi flani na siyo mwanasiasa.

Anasoma sana vitabu, anafaham vitu vingi. Ni asset ya kutumiwa kwa manufaa sehemu flani,,,lkn yeye km yeye hajajengeka sana kisiasa wala hana algorithms za kisiasa kwa asilimia kubwa.
 
"ITS BETTER TO LEAD FROM BEHIND AND PUT OTHERS INFRONT ESPECIALLY WHEN YOU CELEBRATE A VICTORY WHEN NICE THING OCCUR. YOU TAKE THE FRONTLINE WHEN THERE IS A DANGER, THEN PEOPLE WILL APPRECIATE YOUR LEADERSHIP"

NELSON MANDELA
 
Back
Top Bottom