Kwa sasa tutajua weledi na nguvu za January Makamba kwenye siasa nchini!

Kuna watu mna hoja nzuri kweli.Very interesting kusoma.Kiukweli naona hapa kati siasa yetu imetiwa chachandu la hatar joto limepanda kama lile la kipind cha uchaguzi 2015.
Lets wait and see.Is he smart? or was just a lucky boy spoonfed by the system.
In Tanzania political locus, this is the million dollar question!

We're about to get a true answer!
 
Ina maana kukaa serikalini na kushika nafasi za uwaziri muda wote huo bado hana pesa anategemea wafanyabiashara wampe pesa?kweli mswahili ni mswahili tu.
Hizo nafasi tuna zitamani tuzikamate angalau kwa miezi 6 tu.hatukamatiki tena

Ana hela kweli hilo halina mjadala, ila sio mfanyabiashara useme anaweza kuzichanga. Sana sana kama ana nyumba za kupangisha wangalau. Lakini akilogwa akafungua biashara bila mshahara wa serekali lazima changamoto zimuangushe. Saa hii huyo dogo ataenda kwa waganga wa kila aina ili arudi kwenye madaraka. Hana ujanja wowote nje ya vyeo vya upendeleo.
 
Ila amekosea sana kutoroka uapishwaji wa anaye chukua cheo chake.

Mwanaume angetia timu na misuti ya kiwaziri.. kaa mbele kabisa..

Ukipewa nafasi toa pongezi na shukrani na sifia sana.

Baada ya hapo unaendelea na mishe zako.

Ajifunze siasa za kina lowassa na kina mbowe.

Wanatukanwa sana lakini ukionana nao utadhani wamepoteza kumbukumbu.

Makambe usikimbie tatizo.. mwanaume anakabiliana na matatizo.
 
Ng'wamapalala, Kwakuwa hata Baba yake hayupo madarakani,hata yeye kusimama ni ngumu inatakiwa abadilike ili JPM aamini kabadilisha.Kinyongo cha Nape kimemponza January,Nape anataka atengeneza hali fulani kuwa mambo hayako sawa ili apate wafuasi kwenda nao
 
Makamba amerithishwa cheo gani?
Amekuwa mbunge kwa kuchaguliwa na wananchi,amekuwa waziri Kwa kuchaguliwa na marais wawili tofauti.
Watoto wa Nyerere walitaka kurithishwa Urais wa baba yao?
Kuna mahali Nyerere amewahi kuzungumzia kwa nini watoto wake hawajafanikiwa sana pamoja na wao kujihusisha nazo na kuendelea nazo mpaka sasa?
Kuzaliwa na "a political silver spoon" ni tatizo? Watoto wa viongozi nao hawaruhusiwi kuwa viongozi?
Nop. Nyerere hakutaka kuwarithisha watoto wake vyeo. Ingawa Butiku, Bonka Munanke, Musuguri and the rest, walitaka Nyerere aendelee kutawala. Nyerere alihisi Kamba imekatika na jiwe, akakaa pembeni
 
Nimeeleza ninachoona kinawezekana, na kuweka mipaka ya uwezo wangu kutabiri kwa uhakika, kwamba, pamoja na maoni yangu haya, usiende ku bet kwa maoni haya, halafu Makamba akafukuzwa uanachama, halafu ukamlaumu Kiranga.

Kwa sababu Magufuli haeleweki anataka nini, na hata sina hakika kama yeye mwenyewe anaelewa anataka nini.

Nimekuwa muangalifu baada ya kusema Bashe atachezea backbench sana bila appointment kwa kuwa ni "team Lowassa" mjuaji, lakini ikawa kama vile Magu kanisoma halafu kataka kunionesha hatabiriki, akamteua Bashe aondoke backbenchers za Bunge aingie serikalini.
Umenichekesha sana kwenye aya ya mwisho.

Kwamba jamaa amekusoma halafu akajisemea ngoja nimuoneshe huyu anayedhani ananijua.

Mimi nilianza kujaribu kumsoma mwanzoni ili nipate mwelekeo/mpangilio wake kiutendaji lakini baadaye nikaacha kutokana na moja ya sababu ulizozisema.

Ninachojua tu ni kuwa ukitaka kupambana naye basi lazima uelewe kuwa hawezi kukaa kimya lazima atajibu mapigo kwa maneno au vitendo, Hoja ya msingi ni mapigo gani atajibu.
 
Ila amekosea sana kutoroka uapishwaji wa anaye chukua cheo chake.

Mwanaume angetia timu na misuti ya kiwaziri.. kaa mbele kabisa..

Ukipewa nafasi toa pongezi na shukrani na sifia sana.

Baada ya hapo unaendelea na mishe zako.

Ajifunze siasa za kina lowassa na kina mbowe.

Wanatukanwa sana lakini ukionana nao utadhani wamepoteza kumbukumbu.

Makambe usikimbie tatizo.. mwanaume anakabiliana na matatizo.
Mkuu;
Ninakubaliana na angalizo lako.

Kama nilivyosema, hii ni ishara moja kuwa bado ni mchanga kisiasa.
 
Kwakuwa hata Baba yake hayupo madarakani,hata yeye kusimama ni ngumu inatakiwa abadilike ili JPM aamini kabadilisha.Kinyongo cha Nape kimemponza January,Nape anataka atengeneza hali fulani kuwa mambo hayako sawa ili apate wafuasi kwenda nao
Mkuu;
Hoja yako inataka tuamini kuwa Nape Nnauye ndiye mnasihi wa Makamba Jr!

Siamini kama ni kweli.
 
Nachoweza kusema kuhusu January ni mtu charismatic, anajua ni nini cha kuongea na wapi aongee pasipo kuharibu. Ni moja Kati ya viongozi wanaoweza command presence yao pasipo kutumia nguvu nyingi. Hili nimeliona mwenyewe maana niliwahi hudhuria conference moja ambayo alikuwa ni moja ya panelist lakini si yule aliyesubiriwa kwa hamu lakini baada ya kukubidhiwa mic, Kila mtu alifurahia pengine zaidi ya wale waliotegemewa.

Kuhusu uwezo wake binafsi ukiitoa hiyo quality siwezi sema Sana maana success yake kubwa ni kuondoa mifuko ya plastic ambayo kiukweli lilikuwa si suala jipya na pia lilihusisha mass conciousness ambayo ililifanya kuwa rahisi zaidi. I wish him all the best lakini
 
Makamba JR amezidi kujipalia tu kaa la moto kwa kutotokea ktk hio hafla wacha ngonsha amnyooshe kweli sasa tuond io influence aliyotumia kukabiliana na swala la mifuko kama itakuwa applicable kwa sasa.
 
Si makamba tu, hakuna mwanaccm yoyote mwenye nguvu au ushawishi bila mbeleko ya tiss na policeccm.
Mkuu;
Hoja yako inaweza kuwa ni kweli lakini mimi siamini.

Sidhani kama umeiangalia CCM kwa upana wake na unaijua historia yake.

Nadhani unadhani CCM imeanzia kwenye kizazi cha UVCCM wa sasa na viongozi walioko madarakani.

Hujui kuwa kuna viongozi kama Mwl. Nyerere alikuwa mwanaCCM?
 
Mkuu;
Huezi kuhitimisha tu kwisha habari yake wakati hutujui yajayo akiwa nje ya kuta za watalawa.
Ni vigumu sana kufurukuta
Jamaa ana vimeo.vingi sana tutammaliza within seconds!
Ana mkopo wa Bilioni moja kajichota Nssf,hajatoa maelezo zaidi ya kusema Musiba chizi
Ana NGO anajifanya ni kwa ajili ya masndeleo ya bumbuli,kumbe ni kichaka cha kutakatisha mabilioni ya pesa ambayo hayawafikii walengwa
 
Nachoweza kusema kuhusu January ni mtu charismatic, anajua ni nini cha kuongea na wapi aongee pasipo kuharibu. Ni moja Kati ya viongozi wanaoweza command presence yao pasipo kutumia nguvu nyingi. Hili nimeliona mwenyewe maana niliwahi hudhuria conference moja ambayo alikuwa ni moja ya panelist lakini si yule aliyesubiriwa kwa hamu lakini baada ya kukubidhiwa mic, Kila mtu alifurahia pengine zaidi ya wale waliotegemewa.

Kuhusu uwezo wake binafsi ukiitoa hiyo quality siwezi sema Sana maana success yake kubwa ni kuondoa mifuko ya plastic ambayo kiukweli lilikuwa si suala jipya na pia lilihusisha mass conciousness ambayo ililifanya kuwa rahisi zaidi. I wish him all the best lakini
Mkuu;
Nadhani unafanya kosa kwa kumpima kiongozi kwa kutumia eneo moja halafu ukahitimisha kuwa ana haiba kubwa (Charisma).

Mfano mdogo, charisimatic person must be influential and authentic. Je makamba Jr ni authentic? Nope. Hili eneo dogo tu linamtoa nje,
 
Makamba JR amezidi kujipalia tu kaa la moto kwa kutotokea ktk hio hafla wacha ngonsha amnyooshe kweli sasa tuond io influence aliyotumia kukabiliana na swala la mifuko kama itakuwa applicable kwa sasa.
Mkuu;
Mimi inanishangaza kidogo kuona mwanasiasa aliyekuwa serikalini tokea kwenye utawala wa Rais Kikwete anapongezwa kwa kufanikisha suala moja tu!

Hii kwangu sio ushindi bali ni kushindwa hasa ukichukulia kuwa nchi yetu ina matatizo na changamongo nyingi wakati huo huo alikuwa ni privileged class!
 
Back
Top Bottom