Kwa sasa tutajua weledi na nguvu za January Makamba kwenye siasa nchini!

nchi hii hata Joti anaweza kuwa powerful ilimradi tu mapolisi wakiwa upande wake!
Mkuu;
Hoja yako haina ubishi lakini hoja ya msingi ni pale baadhi ya watu wanaposema Makamba Jr ana nguvu za kisiasa hata nje ya nguvu za utawala.

Je, Makamba Jr atakuwa zaidi ya yule aliyekuwa ndani ya nyumba za utawala?
 
Hana nguvu yoyote walibebwa na wazazi wao,hata ww mzazi wako angekua yupo kwenye system kitambo ungeshakua umepata nafasi ya kiuongozi serikalini.
watoto wa masikini wenye elimu na uwezo mkubwa zaidi yao wapo wengi zaidi ya hao unaowaona ila wanakosa connection tu.
Mkuu;

Kumbuka kuna wengine wana hoja kuwa Majamba Jr hata asingetoka kwenye familia ya watawala angefika hapo alipo.

Kwa sasa ndio tutapima nguvu alizonazo pamoja na weledi wake.
 
Kwa uwezo wa kisiasa ktk kufikiri na kuchanganua mambo na sarakasi za ccm makamba siwezi kumlinganusha na Bashe, bashe yupo vizuri zaidi ktk pilika za siasa ya kiccm.
Mkuu;
Nadhani hoja hapa sio kulinganisha wanasiasa bali ni kumchambua Makamba Jr ukilinganisha na siasa za nchini.

Je, weledi na nguvu kuasi gani aliyonayo akiwa nje ya nyumba za utawala/CCM.
 
Mkuu umetoa overview nzuri sana. Waandishi wetu wa habari kina Pascal mayala wangekuwa na kazi ya kudadavua kama wenzao wa ulaya kwa kuangalia the Makamba family in totality, I'm sure wangekuja na story tamu sana. I believe is not about January but the Makamba syndrome including Snr, jnr, sister and even mother. There is a story to tell, very touching one.

Mkuu;
Katika hoja yangu nimejaribu kuchambua sehemu kuu mbili. Moja ndio umeiandika lakini pia sehemu ya pili ni wale wanaosema ana nguvu na weledi wa kisiasa.

Muda hutoa jibu sahihi. Tusubiri kwa sasa huo muda kutupa jibu sahihi.
 
Makamba mweupe tu hata kufanya mtiani wa form six alifanya manoeuver tu,
Kazi yenyewe foreign affair alipata kwa upendeleo hakufanya usaili wala nini.
Hata kusomeshwa kwake masters US was not by merit ilikuwa upendeleo dhahiri.
Mkuu;
Nadhani kwenye maisha yake nimeainisha. Najua Mzee Mkapa alimsaidia kwenye elimu yake nchini Marekani.

Hoja ya msingi kwa sasa, Je, ana nguvu na weledi tunaoambiwa akiwa nje ya mfumo wa watawala?
 
Sioni scenario ya January Makamba kuondolewa uanachama CCM. Na sioni kwamba Magufuli anataka kufanya hivyo.

Baada ya kusema hivyo, sioni hata kama Magufuli mwenyewe anajua kesho anataka kufanya nini, kwa hiyo anaweza kuamka na mzuka wowote.
Mkuu Kiranga

Nadhani andiko lako kama limejipinga lenyewe!

Umeandika huoni kama Makamba Jr anaweza kuondolewa uanachama wa CCM halafu hapo hapo ukasema inawezekana kwa sababu Rais Magufuli haeleweki!

Mimi ninakubaliana na wewe kwenye hoja ya Rais Magufuli kutoeleweka.

Rais Magufuli ana tatizo kwenye kufuata taratibu, kanuni na sheria zilizowekwa.

Siwezi kushangaa nikisikia Makamba Jr amefukuzwa ndani ya CCM kama zile sauti zilizofukuliwa zilikuwa kweli niza Makamba Jr.

Inawezekana zile sauti zimetolewa ili kuufahamisha umma kuwa kuna mengi zaidi watoa sauti wanayajua.
 
Kukaa ndani ya system ilikuwa ni malipo ya JK kwa baba yake, kwa mchango wake ndani ya mtandao. Na yeye alijiandaa kwa makubwa. Yes ana akili zake. Sio sawa na Nape ambaye sijui wanampendea nini maana kichwani ni kama sifuri kabisa
Mkuu;
Hoja ya msingi kwa sasa, Je, ana akili kiasi gani akiwa nje ya nyumba za watawala?
 
Sina cha kukosoa katika uwezo wa January katika siasa. Binafsi nampa A plus. Jambo la Msingi hapa la kujiuliza ni je,hakuyaona mazingira ya kisiasa yalivyomzunguka na kuwa makini zaidi katika ngwe hii? Aliweza kutabiri matokeo ya hizo harakati zake backstage na kuhakikisha kwamba matokeo yake yatakua positive kwenye ndoto zake za siasa? Katika hii game mpaka sasa amegain au amelose? Atagain au atalose?
Mkuu;
Unampa A plus kwa kutumia kigezo gani?

Je, hicho kigezo ulichotumia kitafanya kazi katika mazingira ya yeye kuwa nje ya kuta za watawala?
 
Kuna watu mna hoja nzuri kweli.Very interesting kusoma.Kiukweli naona hapa kati siasa yetu imetiwa chachandu la hatar joto limepanda kama lile la kipind cha uchaguzi 2015.
Lets wait and see.Is he smart? or was just a lucky boy spoonfed by the system.
 
Mkuu Kiranga

Nadhani andiko lako kama limejipinga lenyewe!

Umeandika huoni kama Makamba Jr anaweza kuondolewa uanachama wa CCM halafu hapo hapo ukasema inawezekana kwa sababu Rais Magufuli haeleweki!

Mimi ninakubaliana na wewe kwenye hoja ya Rais Magufuli kutoeleweka.

Rais Magufuli ana tatizo kwenye kufuata taratibu, kanuni na sheria zilizowekwa.

Siwezi kushangaa nikisikia Makamba Jr amefukuzwa ndani ya CCM kama zile sauti zilizofukuliwa zilikuwa kweli niza Makamba Jr.

Inawezekana zile sauti zimetolewa ili kuufahamisha umma kuwa kuna mengi zaidi watoa sauti wanayajua.
Nimeeleza ninachoona kinawezekana, na kuweka mipaka ya uwezo wangu kutabiri kwa uhakika, kwamba, pamoja na maoni yangu haya, usiende ku bet kwa maoni haya, halafu Makamba akafukuzwa uanachama, halafu ukamlaumu Kiranga.

Kwa sababu Magufuli haeleweki anataka nini, na hata sina hakika kama yeye mwenyewe anaelewa anataka nini.

Nimekuwa muangalifu baada ya kusema Bashe atachezea backbench sana bila appointment kwa kuwa ni "team Lowassa" mjuaji, lakini ikawa kama vile Magu kanisoma halafu kataka kunionesha hatabiriki, akamteua Bashe aondoke backbenchers za Bunge aingie serikalini.
 
CCM ni sawa na chemchem isiyokauka maji na iliyo kwenye mbuga ya wanyama. Kila mnyama ataitegemea sana chemchem hiyo kipindi cha kiangazi na kipindi cha masika baadhi ya wanyama wataidharau , wengine watafika hatua ya kutemea mate na kujisaidia pembeni

Nguvu ya ccm iko ndani ya madaraka ya urais ambapo cheo cha mwenyekiti wake huwa na kofia ya amiri jeshi mkuu. Hapo ndio nguvu pekee ya wanaccm wote. Ukimtoa mwana CM yoyote ndani ya ccm ni nadra sana kufanya siasa akafanikiwa hasa hawa waliozaliwa 70s kwenda mbele. Huyo Januari hawezi siasa zozote nje ya siasa za mbeleko ya vyombo vya dola, na anaogopa jela kuliko hata kifo. Leo hii ccm ikitoka madarakani, wanaccm karibia wote watahamia chama kilichoko madarakani ambapo mbeleko ya vyombo vya dola itaendelea kuwa mbele yao.
 
Mkuu umetoa overview nzuri sana. Waandishi wetu wa habari kina Pascal mayala wangekuwa na kazi ya kudadavua kama wenzao wa ulaya kwa kuangalia the Makamba family in totality, I'm sure wangekuja na story tamu sana. I believe is not about January but the Makamba syndrome including Snr, jnr, sister and even mother. There is a story to tell, very touching one.
Mkuu;
Ninakubaliana na angalizo lako.

Nadhani tatizo kuu sio kutoa (supply) bali tatizo ni hitaji (demand).

Watanzania walio wengi hawapendi kusoma makala ndefu au vitabu. Mfano ni hapa Jamiiforums, ukitoa hoja ndefu utaona wengi wa wachangiaji wanaandika, ''ndefu sana'' nimeishia kusoma njiani.

Kama jamii yetu kwa uwingi ingekuwa inapenda kusoma makala ndefu au vitabu, ninaamini wangejitokeza waandishi wa kuandika makala na vitabu kuhusu masuala mbali mbali ikiwa ni pamoja na historia za maisha ya wanasiasa na uchambuzi. Nadhani kwa msingi huu tungekuwa tunajua uwezo na nguvu za Makamba Jr akiwa nje ya siasa.

Kilichobaki kwa sasa ni kupata majibu baada ya tukio kutokea.
 
Back
Top Bottom