Kwa sasa tutajua weledi na nguvu za January Makamba kwenye siasa nchini!

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
6,808
6,500
Kumekuwa na mjadala mrefu bila hitimisho kuhusu nguvu na uwezo kifikra wa January Makamba kwenye eneo la siasa za Tanzania.

Majadiliano haya yamekuwa marefu kutokana na mazingira ya kimaisha aliyokuwa nayo tokea utotoni mpaka Uwaziri katika Wizara ya nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.

Kuna mwanaJF aliwahi kuandika thread hii;
LINK>>>January Makamba, very intelligent, humble, down to earth! Can make the best President

Makamba Jr ni kati ya watu wachache nchini ambao maisha yao unaweza kuyaeleza kwa lugha ya kiingereza ‘’born with a political silver spoon’’.

Makamba Snr mbali ya kuwa Katibu Mkuu wa CCM pia kwa nyakati tofauti ameshika nyadhifa mbali mbali serikali ikiwa ni pamoja na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Morogoro na Kigoma.

Kwa mantiki hii ni vigumu sana kujua weledi na nguvu za Makamba Jr kwa sababu hata ubunge wa Jimbo la Bumbuli aliupata wakati Baba yake, Makamba Snr akiwa Katibu Mkuu wa CCM wakati yeye akiwa msaidizi wa karibu wa Rais Kikwete. Ni baada ya uchaguzi huo uliolalamikiwa sana ndani ya CCM kwa rushwa na upendeleo ilibidi CCM ifanye mabadiliko na kumuondoa Makamba Snr.

Kazi ya msaidizi wa karibu wa Rais ilimfanya kuwa karibu na vyombo vya habari na wamiliki wa mitandao na amewatumia katika kupitisha ajenda za serikali lakini pia ajenda zake binafsi.

Kwa kifupi ni kwamba, Makamba Jr ameendesha maisha na harakati zake za kisiasa akiwa mtoto wa ‘’watawala’’ huku akisaidiwa na watawala(system).

Tukio la Waraka wa Makamba Snr na Kinana kwa Baraza la Wazee wa CCM huku yeye, Makamba Jnr ikisemekana ndiye mhariri wa waraka huo limechukua sura mpya ya maisha yake ya kisiasa nchini.

CCM chini ya Mwenyekiti Magufuli, kuna uwezekano mkubwa Makamba Jr atafukuzwa uanachama ndani ya CCM na tukio hilo litamfanya aanze maisha ya kisiasa nje ya mfumo uliomsaidia hadi kufikia hatua ya Uwaziri katika Waziri wa nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.

Tukio la yeye kutoonekana katika hafla ya kuapishwa kwa Waziri aliyechukua nafasi yake ni ishara inayoonyesha anajua nini kinachofuata ndani ya CCM lakini kikubwa zaidi ameonyesha bado mchanga/mtoto katika siasa. Hii inaonyesha kuwa kama angekuwa ni Rais halafu akashindwa kwenye Uchaguzi Mkuu basi asingetokea wakati wa kuapishwa Rais Mpya! Typical myopic and tasteless politics.

Maisha haya mapya ndio yatadhihirisha weledi nguvu alizonazo katika uwanja wa siasa za Tanzania mpaka baadhi ya wachangiaji wa mjadala kuhusu weledi na uwezo wake wakasema ana ‘’weledi na nguvu za kisiasa’’ zinazomfanya kuwa Rais wa Tanzania.

Mwaka 2012, Nape Nnauye aliwahi kusema kwenye kipindi cha Jambo Tanzania, TBC kuwa, "Samaki ukimtoa majini hana nguvu, CCM ni taasisi na ina nguvu, ukitaka kuwa na nguvu inabidi uwe ndani ya CCM, bila CCM mwanasiasa huwezi kuwa na nguvu, tutawatoa majini hawa samaki".

Maneno ya Nape Nnauye yalililenga kundi la Edward Lowassa na timu yake (Timu Lowassa) wakati wa vurugu za kisiasa ndani ya CCM. Maneno ya Nape yalidhihirisha ukweli baada ya Lowassa na kundi lake kuondoka CCM na kujikuta hana nguvu mpaka kuamua kurudi tena CCM.

Kwa sasa ni wakati wa kumpima ‘’Samaki’’ January Makamba kama ana nguvu nje ya maji yanayoitwa CCM.
 
Mambo yanabadilika, vizazi vipya vinakuja na mbinu mpya, alikuwa na mazuri yake lakini wapo wengine wenye mikakati tofauti. Licha ya huyu kuwa na nguvu lakini tusisahau nyuma yake yuko mzee wake. Je, nguvu ni ya kwake au ya kuvuviwa kutoka kea baba?
 
Mambo yanabadilika, vizazi vipya vinakuja na mbinu mpya, alikuwa na mazuri yake lakini wapo wengine wenye mikakati tofauti. Licha ya huyu kuwa na nguvu lakini tusisahau nyuma yake yuko mzee wake. Je, nguvu ni ya kwake au ya kuvuviwa kutoka kea baba?
Huyo mzee wake ana nguvu ganj,ana influence kumzidi lowassa?

System ndo zimewalinda miaka yoote hii,wakiwa nje ya system hata Halima mdee/Ester bulaya ni ngangari kuliko hao wazee.
 
Hata hapo Bumbuli ni ngome ya CCM sio Makamba’s , wakiamua kumfanyia fitna hata Ubunge hataupata. Influence ya Makamba ni Twitter tu zaidi ya hapo hakuna kitu. Yupo karibu na baadhi ya wafanyabiashara wakubwa ila hakuna mfanyabiashara atakayetoa pesa kwa Makamba huku anajua anaenda kushindwa.
 
makamba pamoja na baba yake mnawaoverrate sana..mbona weupe sana wale
Mkuu;
Katika hoja yangu nimejaribu kuchambua sehemu kuu mbili. Moja ndio umeiandika lakini pia sehemu ya pili ni wale wanaosema ana nguvu na weledi wa kisiasa.

Muda hutoa jibu sahihi. Tusubiri kwa sasa huo muda kutupa jibu sahihi.
 
CCM ni sawa na chemchem isiyokauka maji na iliyo kwenye mbuga ya wanyama. Kila mnyama ataitegemea sana chemchem hiyo kipindi cha kiangazi na kipindi cha masika baadhi ya wanyama wataidharau , wengine watafika hatua ya kutemea mate na kujisaidia pembeni
Mkuu;
Nakuomba udadavue zaidi hoja yako!

Kumbuka binadamu tunatofautiana uwezo kifikra katika kuchanganua masuala mbali mbali!
 
Back
Top Bottom