Kwa rasimu hii, CCM inakufa

Ndiyo maana tunapiga kelele kuwekewa rasimu online tuisome wenyewe.

Mimi nilifikiri wagombea binafsi itakuwa katika ngazi zote za uongozi kwa maana kuwa madiwani, wabunge na Rais.

Thanks.
 
Unalolisema Mkuu linaweza kabisa kutokea, lakini hii nchi si ya CCM bali ni ya Watanzania hivyo naamini kabisa kama Watanzania tukisimama kidete na kutoruhusu CCM wafanye upumbavu wao wa kuchakachua katiba watakavyo wao basi huo uchakachuaji hautoweza kutokea.


 

Kwenye rasimu ambayo ninayo, Ibara ya 33 (1) inasimeka hivi, "Kila raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ana haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yaom, kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria."
 
Ndiyo maana tunapiga kelele kuwekewa rasimu online tuisome wenyewe.

Mimi nilifikiri wagombea binafsi itakuwa katika ngazi zote za uongozi kwa maana kuwa madiwani, wabunge na Rais.

Thanks.


Amin, ngazi zote kuanzia Kitongoji, Kijiji, Mtaa, udiwani, ubunge hadi urais kunaruhusiwa mgombea binafsi! Mbona hamtaki kuelewa?
 
hivi katiba mpya ni kwaajili ya ccm kwani chadema wanaipenda. Kuwa mtanzania zaidi kuliko ushabiki.
 
Mgombea binafsi itaikoa CCM kwani watakaotoka CCM sio lazima wakimbilie upinzani kama sharti la kuwa mwanasiasa. Hili lina faida hata kwa wale watakaopenda kuachana na vyama vya upinzani na kuwa huru badala ya kwenda CCM.

Hicho kipengele kimoja tu kinaleta u-Taifa mbele ya kila kitu...na haya mambo ya maandamano na siasa za chuki na tamaa za kuchukua dola zitapotea kabisa
 

Umeandika ukweli sana Mkuu , ndiyo maana nilisema kama tutakuwa na Tume huru ya Uchaguzi , hata hiyo rushwa ya Kitanda kwa kitanda inaweza kukomeshwa .
 
hivi katiba mpya ni kwaajili ya ccm kwani chadema wote wanaipenda?. Kuwa mtanzania zaidi kuliko ushabiki.
 
Mkuu manyerere,kwanza nikupongeze kwa thread hii..pili naomba uiweke rasimu ya katiba kwenye uzi wako huu...lakini hata kabla haujaiweka naomba tu unipunguzie mhemko kwa kunithibitishia iwapo mgombea binafsi anaruhusiwa hadi kwenye ngazi ya mbunge na vitongoji... na kama hivyo ndivyo baasi mimi tayari ni mbunge mteule... maana wananchi wameniomba nigombee sema sababu ya kutogombea ni kuwa sio mwanachama wa ccm na sitaki kuwa associated na ccm hata kidogo na sipendi kuwa muumini wa vyama vya siasa....

please say a word...
 
Nasubiri rasimu niisome nione yaliyondani zaidi.
Jamani kwa taarifa yenu bado vyama vitakuwa ni muhimu kuliko kuwa mgombea binafsi.
BINAFSI NINA MPANGO WA KUGOMBEA URAHISI(urais) NGOJA NIONE NAMNA YA KUTUPA KARATA YANGU. LAKINI NASUBIRI RASIMU NIONE KUNA NINI NDANI. NINGEPENDA SANA KUGOMBEA KUPITIA CHAMA KULIKO BINAFSI!
 
Mkuu,
Mgombea huru anaruhusiwa kuanzia kwenye nafasi ya chini kabisa mpaka ya juu kabisa.

Kwahiyo ikipita hiyo basi uchaguzi wa serikali za mitaa utaruhusu wagombea huru. Na mwaka 2015, madiwani, wabunge na rais, wagombea huru wataruhusiwa.

 
Wakati mwingine ni busara tu kukubali kwamba huna uelewa au ufahamu na jambo fulani, mimi sijui yote na hata wewe hujui yote, sasa ngoja nikuelimishe kile usichokijuwa.....

Waislamu wa Tanganyika hawana lolote la kujifunza kwa Waislamu wa Zanzibar kwa sababu mambo ya kadhi Zanzibar hayapo kikatiba, badala yake Waislamu wa Tanganyika wanataka Mahakama ya kadhi itambulike kikatiba na iendeshwe kwa kodi za Watanzania zikiwemo kodi za pombe kutoka TBL.

Huu mkenge CCM waliingizwa na Augustino Lyatonga Mrema ambaye ndiye mwanasiasa wa kwanza kuja na hoja hii na kuahidi akishinda Urais atawapa Waislamu Mahakama ya kadhi.

Ila kwakuwa CCM ni kusanyiko la walevi na walaghai wakaipora hii hoja na kuiingiza rasmi kwenye ilani yao ya uchaguzi mwaka 2005 na ni Alhaj Kikwete aliyetumika kuwalaghai Waislamu wenzake kwa kitu ambacho hakipo na ni hewa tu.

Endelea kuishi kwenye sayari ya peke yako kwamba Mahakama ya kadhi inakuja kwa ambayo siwezi kuamini nakupa pole kwa kujitia upofu kwa hiyari yao, Serikali imeshatoa msimamo wake Bungeni kwamba Waislamu ruksa kuanzisha Mahakama yao ya kadhi ila haitakuwa ndani ya katiba.

Ni Muislamu mpuuzi peke yake ambaye anaweza kuipigia kura CCM mwaka 2015 because what i know is Muslim for CCM but CCM for Christian.
 
Ni nzuri kwa kweli,tunaomba utekelezaji bila zengwe tu
 
Shirikisha ubongo wako, CCM wala hawapaswi kulazimisha Tume, hii ni ahadi ya CCM katika ilani yao ya uchaguzi mwaka 2005 kinachotakiwa ni utelezaji tu au waombwe radhi Waislamu kwa kudanganywa na CCM.

Upeo wako ni finyu sana napata shida kuchangia hoja na low thinkers kama wewe, ila kwenye wajinga ndipo werevu utambulika.
 
Wanzibari na wasubiri kigamboni mkifika pale mnipungie hasa mlioshikara wizara huku nimevaa kapelo ya njano 'chagua cc..'
 
Mzee warioba ...ntaanza kumuheshimu kwa uwezo wangu wote...sikutegemea rasimu nzuri namna ile...kwa zile hints...hiyo katiba itakuwa bora sana.....ni katiba ambayo kama si mzalendo lazima UKAE..naanza kuelewa na msimamo wa prof baregu...
 
Matola hapo ndipo tulikuwa tunatofautiana lakini mimi nimejibu kulingana na jibu alilolitoa Mzee Warioba.

Sasa hawa Waislamu wa bara nao wana matatizo au lao jambo kwa sababu kama zanzibar wana mahakama ya kadhi inayoendesha mambo yake kama wanavyopenda, kwa nini waislamu wa bara wang'ang'anie kuwa na mahakama ya kadhi tofauti naya Zanzibar.

Kung'ang'ania na hoja yao hii ni kutafuta marumbano na serikali yasiyo kuwa na maana. Kama watu wa UAMSHO wanakubaliana na mahakama ya kadhi huko zanzibar, kwa nini masheikh wa bara wasifanye kama Zanzibar?

May be, I'm missing a point!
 
Last edited by a moderator:
Ccm chonda chonde mshaharibu nchi na hii rasimu isichakachuliwe.....mwigulu,nape,kinana,migiro n co..tunawangalia msilete utani kwenye hili....tuipende nchi yetu(tanzania, tanganyika and zanzibar)
 
Mkuu ccm,chadema,waliberali wa tz/cuf watapita lakini tanganyika itabaki,naiona tanganyika ile ikirudi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…