Nakuelewa mkuu,
Lakini ukweli ni kwamba hata kama wameombwa na wapiga kura wa Gambia,
Uvamizi wa kijeshi siyo njia sahihi kwa sasa, wangemuwekea vikwazo vya kiuchumi tu.
Lazima atasalimu amri.
Tukiangalia hili jambo kwenye taswira kubwa,
Afrika yetu haitakiwi iige kila kitu kutoka Ulaya na Marekani,
Kama tukianza kuvamiana kijeshi leo, nakuhakikishia haitaishia hapo tu.
Litakuwa ni Zimwi Jipya kuingia barani Afrika mbali na Umasikini, Maradhi na Ujinga.
Utasikia uchaguzi wa Zimbabwe haukuwa huru na haki,
SADC itume kikosi kazi kwenda kumtoa Robert Mugabe.
Utasikia tena Uchaguzi wa Burundi siyo wa huru na haki,
Rwanda na Uganda wanapendekeza EAC itume kikosi kazi kumtoa Nkhurunzinza.
Mwishowe tutakuja kufika sehemu,
Nchi kubwa zenye nguvu zitatumia huo mwamvuli kuvamia nchi nyingine.
Mwaka 1938 Adolf Hitler alivamia Czechoslovakia akisingizia kwamba anaenda kulinda haki za raia wa Czech na Slovakia.
Lakini ukweli ni kwamba alichokifanya Hitler ulikuwa ni Uhalifu wa kivita.
ECOWAS watakuwa ni watu wa hovyo sana kama wakikubali kufanya huu uamuzi,
Hovyo! Hovyooo kabisaaaaa!!!!
Chaguzi za nyuma akiwa rais ni tume za uchaguzi zilizomtangaza kushinda na hapakuwa na shida.
Mwaka jana mwenyekiti wa tume katangaza Jammey kashindwa, Jammey kakubali, baada ya muda Jammey kageuka. Jiulize, huyo mtu kuna uchaguzi wowote wa baadae atakaopokea matokeo ya kushindwa?
Kwa matukio hayo na sababu ulizotoa, tunatengeneza mazoea mabaya pia, yaani rais ashimeshindwa kwa mujibu wa tume, amekubali baada ya muda anakataa, anatangaza hali ya hatari na hivyo kuzuia kuapishwa kwa aliyetangazwa na tume!
Huo ni mwanya kwa wengine katika nchi hiyo na labda Afrika kufanya hivyo au hali inayofanana na hiyo siku za baadaye.
Umetumia neno kuvamia, lakini tambua pia huyo anayeng'ng'ania pia ni mvamizi wa kutumia majeshi.
Vinginevyo turudi tu kwenye mifumo yetu ya enzi ya uchifu na ufalme tujue moja kinyume cha hapo wakorofi washughulikiwe na washughulikiwe kikwelikweli.