Ububu wa AU na ECOWAS baada ya mapinduzi ya Niger waonyesha jinsi akili ya Mwafrika ilivyofumbwa na kuwa tegemezi

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,400
Mapinduzi yameishatokea nchini Niger baada ya jeshi ambayo yameungwa mkono na viongozi wa kijeshi wa Mali, Burkina Faso na hata Algeria.

ECOWAS umoja wa nchi za Afrika Magharibi kwa harakaharaka bila kufikiri wakatangaza kuwa watachukua hatua za kijeshi endapo raisi wa Niger aliepinduliwa Mohamed Bazoum hatorudishwa madarakani.

Baadae Nigeria moja ya wanachama wa ECOWAS wakataka umeme unokwenda nchini Niger ambayo asilimia 70 ya umeme huo yaupata kutoka Nigeria.

Umoja wa nchi za Afrika AU nao umetoa siku 15 kwa uongozi wa kijeshi nchini Niger kuurudisha utawala wa kidemokrasia wa Niger chini ya Bazoum.

Lakini nchini Nigeria kumetokea mapingamizi makubwa kwa serikali na bunge la seneti kupitisha mswada wa dharura wa kuvamia kijeshi Niger ambayo ni majirani zake ili kuwafurahisha nchi za magharibi hususan Ufaransa na Marekani.

Wakti huohuo bado nchini Niger vipo vikosi vya Marekani (1100) na Ufaransa (1500) ambavyo vipo kwa ajili ya kuwafunza majeshi ya Niger "jinsi ya kupambana na magaidi wa Al -Qaeda na ISIS".

Ni wazi kadri ziku zinavyozidi kuyoyoma jeshi la Niger litaendelea kumshikilia Mohamed Bazoum hadi hapo vumbi litapotulia na nchi za magharibi zinapunguza nguvu ya kauli zake za vitisho kwa Niger na kusisitiza mazungumzo ya kidiplomasia.

Hichi kivuli cha kupambana na maghaidi wa ISIL na Al-Qaeda ni kivuli cha nchi za magharibi katika kuficha ejenda yao ya kuwepo sehemu hiyo ya Afrika yenye uwingi wa rasilimali hususan madini ya Uranium ambayo hutumika kutengeneza umeme.

Kwanza, hivi vikundi vya Al-Qaeda na ISIL asili yake ni Afghanstan na Iraq ambapo baadae itikadi yake ilisambaa hadi kufika nchini Libya ambapo baadae vikatokea vita vya wenyewe kwa wenyewe na baadae kuuawa kwa aliekuwa raisi wa Libya Muammar Gaddafi mwaka 2011.

Pili, vikundi hivi ni mpango wa nchi za magharibi hususan NATO na Marekani ambao wamekuwa wakivitumia vikundi hivi kuleta misukosuko katika sehemu mbalimbali duniani hususan Libya, jangwa la Sahara na nchini Syria. Kuwepo wa ISIL kwenye jangwa la Sahara kumesababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe na uvunjwaji wa amani katika nchi nchi katika eneo hilo kama Mali, Burkina Faso, Sahara Magharibi na Niger.

Lakini ikumbukwe kwamba siku zote kunapotokea vita mara nyingi uwepo wa majeshi ya kigeni huwa ni kwa ajili ya kufanya uporaji au "looting" na mauaji (assassinations) kwa baadhi ya watu muhimu kwenye nchi hizo.

Lakini matukio ya mapinduzi yalotokea nchini Mali na Burkina Faso ni mwamko mpya wa fikra za waafrika kuwa TWAIBIWA.

Wizi huu wa maliasili za bara la Afrika umekuwepo miaka nenda rudi huku ukiziacha nchi nyingi za Afrika zikiwa maskini wa kutupwa na wananchi wake wakiishi maisha duni. Serikali za kiraia za Mali, Burkina Faso na Niger zimekuwa zikiwakumbatia nchi za magharibi hususan Ufaransa kwa kutiliana saini mikataba ya hovyo inohusu rasilimali za nchi hizo kwa malipo ya kupewa ulinzi wa majeshi ya kigeni pamoja na mikataba ya kijeshi ambayo mingi ya ya kununua vifaa vya kijeshi ambayo hutumika kuwadidimiza wananchi wenye kuthubutu kuhoji utendaji wa serikali hizo.

Ni kweli Mohamed Bazoum anasemwa kuwa ni raisi aliechaguliwa kidemokrasia lakini kitendo cha nchi za magharibi ziliongozwa na Ufaransa na Marekani kupaza sana sauti kwamba Bazoum aaachiwe kwaleta masuali mengi juu ya nini khasa nchi hizi zinakosa zikiliacha bara la Afrika lijitegemee?

Pia kitendo cha Bazoum kupewa kipande kwenye gazeti la Washington Post kuomba jumuiya ya kimataifa kuingilia ili wasaidie kumrudisha madarakani ni kitendo cha kuonyesha kwamba hata bwana Bazoum mwenyewe haiamini AU kwa kuiona haina maana.

Umoja wa nchi za Afrika na ECOWAS wameonyesha udhaifu mkubwa sana katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi katika nchi za Afrika, pia kuonyesha ufivyu mkubwa wa mawazo walo nayo na pia kutojali kabisa mstakabali wa maendeleo ya bara la Afrika.

Huu ni wakati kwa nchi zinounda AU na jumuiya zingine ndogondogo kama ECOWAS na SADC kuachana na mawazo ya kushikiwa akili na kuamka kuleta mabadiliko kwa kuwa vyombo vya kwanza ambayo kabla ya kutoa kauli yoyote zapaswa kuketi vikao ambayo vitaunda taarifa yenye kuonyesha msimamo.

Bara la Afrika kwa sasa lina shida moja kubwa ambayo huenda ikachukua miaka mingi kuitatua, uhamiaji wa kwenda Ulaya.

Nchi za Morocco, Niger, Mauritania, na Libya zimekuwa wahanga wakubwa wa misafara ya wahamiaji kutoka nchi za Niger, Benin, Nigeria,Ghana, Eritrea, Ethiopia na Libya kutaka kuvuka bahari ya Mediterranean ili kwenda barani Ulaya kutafuta maisha.

Italy imekuwa ni nchi iloathirika ngandingandi kuhusiana na suala la wazamiaji na sasa hivi bara la Ulaya lipo mbioni kutekeleza mikakati ya kupunguza wahamiaji wa kutoka barani Afrika.

Wahamiaji kutoka barani Afrika hivi sasa wamekuwa waathirika wa biashara ya binadamu, soko haramu la ajira na hata kuwa watu wasojielewa barani Ulaya jambo linopelekea hata nchi za Ulaya kuwa na fikra mbaya sana kuhusu waafrika.

Huu ni wakati kwa umoja wa nchi za Afrika AU kuhakikisha inaamka na kuja na mikakati mbalimbali ya kuliweka sawa bara la Afrika ili kupambana na matatizo ya kiuchumi , elimu, umaskini wa akili, gharama kubwa za maisha na utorokaji kwenda nje ya nchi bila kufuata taratibu za uhamiaji.

Huu ni wakati wa AU kuacha ububu na kuwa na sauti kupitia vyombo vya habari vya Afrika vyenye kuonyesha taarifa na programs za kiafrika zenye kuelimisha na kutoa picha halisi kuhusu bara hili.

Huu ni wakati wa AU kuja na mpango wa kuhakikisha moja ya nchi za kiafrika yarusha mtambo wa satelite angani ili kusaidia kupata, njia nzuri za mawasiliano, habari, tafiti na taarifa za kijiografia ambazo zipo katika wakati huohuo yaani Real -Time.

AU iachane na ububu ipate wasemaji makini, iimarishe na kutunza vipaji vilivyopoa Afrika, ivutie vipaji kutoka kwa vijana ambao wamezaliwa barani Ulaya ambao wana ujuzi na elimu ya juu katika masuala mengi ili kusababisha uvutaji vipaji "brain drain" iwe kutoka Ulaya kwenda Afrika na sio Afrika kwenda Ulaya.

Bila hivyo ububu wa AU na kauli za kukurupuka za jumuiya kama ya ECOWAS zitakuja kulitumbukiza bara zima la Afrika katika dhioruba ambayo itakuwa ni vigumu kuilezea.
 
Mapinduzi yameishatokea nchini Niger baada ya jeshi ambayo yameungwa mkono na viongozi wa kijeshi wa Mali, Burkina Faso na hata Algeria.

ECOWAS umoja wa nchi za Afrika Magharibi kwa harakaharaka bila kufikiri wakatangaza kuwa watachukua hatua za kijeshi endapo raisi wa Niger aliepinduliwa Mohamed Bazoum hatorudishwa madarakani.

Baadae Nigeria moja ya wanachama wa ECOWAS wakataka umeme unokwenda nchini Niger ambayo asilimia 70 ya umeme huo yaupata kutoka Nigeria.

Umoja wa nchi za Afrika AU nao umetoa siku 15 kwa uongozi wa kijeshi nchini NIger kuurudisha utawala wa kidemokrasia wa Niger chini ya Bazoum.

Lakini nchini Nigeria kumetokea mapingamizi makubwa kwa serikali na bunge la seneti kupitisha mswada wa dharura wa kuvamia kijeshi Niger ambayo ni majirani zake ili kuwafurahisha nchi za magharibi hususan Ufaransa na Marekani.

Wakti huohuo bado nchini Niger vipo vikosi vya Marekani (1100) na Ufaransa (1500) ambavyo vipo kwa ajili ya kuwafunza majeshi ya Niger "jinsi ya kupambana na magaidi wa Al -Qaeda na ISIS".

Ni wazi kadri ziku zinavyozidi kuyoyoma jeshi la Niger litaendelea kumshikilia Mohamed Bazoum hadi hapo vumbi litapotulia na nchi za magharibi zinapunguza nguvu ya kauli zake za vitisho kwa Niger na kusisitiza mazungumzo ya kidiplomasia.

Hichi kivuli cha kupambana na maghaidi wa ISIL na Al-Qaeda ni kivuli cha nchi za magharibi katika kuficha ejenda yao ya kuwepo sehemu hiyo ya Afrika yenye uwingi wa rasilimali hususan madini ya Uranium ambayo hutumika kutengeneza umeme.

Kwanza, hivi vikundi vya Al-Qaeda na ISIL asili yake ni Afghanstan na Iraq ambapo baadae itikadi yake ilisambaa hadi kufika nchini Libya ambapo baadae vikatokea vita vya wenyewe kwa wenyewe na baadae kuuawa kwa aliekuwa raisi wa Libya Muammar Gaddafi mwaka 2011.

Pili, vikundi hivi ni mpango wa nchi za magharibi hususan NATO na Marekani ambao wamekuwa wakivitumia vikundi hivi kuleta misukosuko katika sehemu mbalimbali duniani hususan Libya, jangwa la Sahara na nchini Syria. Kuwepo wa ISIL kwenye jangwa la Sahara kumesababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe na uvunjwaji wa amani katika nchi nchi katika eneo hilo kama Mali, Burkina Faso, Sahara Magharibi na Niger.

Lakini ikumbukwe kwamba siku zote kunapotokea vita mara nyingi uwepo wa majeshi ya kigeni huwa ni kwa ajili ya kufanya uporaji au "looting" na mauaji (assassinations) kwa baadhi ya watu muhimu kwenye nchi hizo.

Lakini matukio ya mapinduzi yalotokea nchini Mali na Burkina Faso ni mwamko mpya wa fikra za waafrika kuwa TWAIBIWA.

Wizi huu wa maliasili za bara la Afrika umekuwepo miaka nenda rudi huku ukiziacha nchi nyingi za Afrika zikiwa maskini wa kutupwa na wananchi wake wakiishi maisha duni. Serikali za kiraia za Mali, Burkina Faso na Niger zimekuwa zikiwakumbatia nchi za magharibi hususan Ufaransa kwa kutiliana saini mikataba ya hovyo inohusu rasilimali za nchi hizo kwa malipo ya kupewa ulinzi wa majeshi ya kigeni pamoja na mikataba ya kijeshi ambayo mingi ya ya kununua vifaa vya kijeshi ambayo hutumika kuwadidimiza wananchi wenye kuthubutu kuhoji utendaji wa serikali hizo.

Ni kweli Mohamed Bazoum anasemwa kuwa ni raisi aliechaguliwa kidemokrasia lakini kitendo cha nchi za magharibi ziliongozwa na Ufaransa na Marekani kupaza sana sauti kwamba Bazoum aaachiwe kwaleta masuali mengi juu ya nini khasa nchi hizi zinakosa zikiliacha bara la Afrika lijitegemee?

Pia kitendo cha Bazoum kupewa kipande kwenye gazeti la Washington Post kuomba jumuiya ya kimataifa kuingilia ili wasaidie kumrudisha madarakani ni kitendo cha kuonyesha kwamba hata bwana Bazoum mwenyewe haiamini AU kwa kuiona haina maana.

Umoja wa nchi za Afrika na ECOWAS wameonyesha udhaifu mkubwa sana katika kuleta mabadiliko ya kiuchumi katika nchi za Afrika, pia kuonyesha ufivyu mkubwa wa mawazo walo nayo na pia kutojali kabisa mstakabali wa maendeleo ya bara la Afrika.

Huu ni wakati kwa nchi zinounda AU na jumuiya zingine ndogondogo kama ECOWAS na SADC kuachana na mawazo ya kushikiwa akili na kuamka kuleta mabadiliko kwa kuwa vyombo vya kwanza ambayo kabla ya kutoa kauli yoyote zapaswa kuketi vikao ambayo vitaunda taarifa yenye kuonyesha msimamo.

Bara la Afrika kwa sasa lina shida moja kubwa ambayo huenda ikachukua miaka mingi kuitatua, uhamiaji wa kwenda Ulaya.

Nchi za Morocco, Niger, Mauritania, na Libya zimekuwa wahanga wakubwa wa misafara ya wahamiaji kutoka nchi za Niger, Benin, Nigeria,Ghana, Eritrea, Ethiopia na Libya kutaka kuvuka bahari ya Mediterranean ili kwenda barani Ulaya kutafuta maisha.

Italy imekuwa ni nchi iloathirika ngandingandi kuhusiana na suala la wazamiaji na sasa hivi bara la Ulaya lipo mbioni kutekeleza mikakati ya kupunguza wahamiaji wa kutoka barani Afrika.

Wahamiaji kutoka barani Afrika hivi sasa wamekuwa waathirika wa biashara ya binadamu, soko haramu la ajira na hata kuwa watu wasojielewa barani Ulaya jambo linopelekea hata nchi za Ulaya kuwa na fikra mbaya sana kuhusu waafrika.

Huu ni wakati kwa umoja wa nchi za Afrika AU kuhakikisha inaamka na kuja na mikakati mbalimbali ya kuliweka sawa bara la Afrika ili kupambana na matatizo ya kiuchumi , elimu, umaskini wa akili, gharama kubwa za maisha na utorokaji kwenda nje ya nchi bila kufuata taratibu za uhamiaji.

Huu ni wakati wa AU kuacha ububu na kuwa na sauti kupitia vyombo vya habari vya Afrika vyenye kuonyesha taarifa na programs za kiafrika zenye kuelimisha na kutoa picha halisi kuhusu bara hili.

Huu ni wakati wa AU kuja na mpango wa kuhakikisha moja ya nchi za kiafrika yarusha mtambo wa satelite angani ili kusaidia kupata, njia nzuri za mawasiliano, habari, tafiti na taarifa za kijiografia ambazo zipo katika wakati huohuo yaani Real -Time.

AU iachane na ububu ipate wasemaji makini, iimarishe na kutunza vipaji vilivyopoa Afrika, ivutie vipaji kutoka kwa vijana ambao wamezaliwa barani Ulaya ambao wana ujuzi na elimu ya juu katika masuala mengi ili kusababisha uvutaji vipaji "brain drain" iwe kutoka Ulaya kwenda Afrika na sio Afrika kwenda Ulaya.

Bila hivyo ububu wa AU na kauli za kukurupuka za jumuiya kama ya ECOWAS zitakuja kulitumbukiza bara zima la Afrika katika dhioruba ambayo itakuwa ni vigumu kuilezea.
Umechambua vizuri sana
 
Ububu wa nchi za kiafrika unatokana na mengi mno
Mosi
Nikua hata wao hawakuingia madarakani kwa uchaguzi uliokia huru na WA haki.

Pili
Viongozi wengi wa kiafrika wako madarakani kwa muda mrefu usio sahihi nje ya muda wa katiba zao ama walibadiki katiba.

Tatu
Wengi wamejilimbikizia Mali za umma kinyume na sheria na ukwasi mkubwa mno.

Nne
Wengi wao wapo kwa kulinda maslahi ya mabebebru badala ya wananchi.

Tano
Baadhi Yao ama wengi wao pia waliingia madarakani kwa mapinduzi.

Na mengi mengineyo.

Hivyo basi kwa sababu hizo hapo juu na nyingine kama hizo wanakosa uhalali na msimamo wa pamoja kukemea ama kuunga mkono mapinduzi kwa kuogopa ama kuwakera wananchi wao ama mabeberu.
Hli hii inaondoa misismamo ya pamoja.
 
AU wapaswa kuundwa upya.

1. AU ni lazima iwe na jeshi lake la kushughulikia migogoro barani Afrika na kuondokana na majeshi ya kulinda amani ambayo yameundwa na kusambazwa katika nchi nyingi barani Afrika, mbona hatuna majeshi la kulinda amani Ulaya?

2. AU ni lazima iwe na sarafu yake ambayo itatumiwa na mataifa yote ya Afrika.

3. AU iwe na Bunge lake.

4. AU ni lazima iwe na sheria zake ambazo zitakuwa zikilinda maslahi ya bara la Afrika na nchi zake zipatazo 54.

5. AU ni lazima iipe nguvu benki ya maendeleo ya Afrika kufanya biashara na nchi zote za Afrika.

6. AU ni lazima iwe na bajeti yake maalum kwa ajili ya shughuli zake zote pale Addis Ababa.

Huu ni wakati wa AU kuamka na kuanza kutoa kauli za uthubutu na kuionyesha kuwa ni umoja wa Afrika wenye nguvu.
 
umechambua vizuri ila Kuna baadhi ya mambo ngoja nifafanue,
Kuhusu satellite Gadaff alijitolea kujenga matokeo yake wakamuua haraka kwani Africa inalipia pesa nyingi sana ulaya.
Kuhusu wahamiaji haramu Mimi ningeshauri Africa wawasaidie wazidi kuongezeka kwani Hilo tatizo limetengenezwa na ulaya yenyewe.
Namba gani wamelitengeneza1. Wamepotea rasilimali nyingi Afrika na kupeleka kwao hivyo kufanya maisha ya Africa kuwa magumu. watu wengi wanakimbilia Dar kutoka mikoani sababu huduma na fursa nyingi zipo Dar pia pamoja na kuwa Dar es salaam hailimi lakini huwezi kusikia Dar es salaam Kuna njaa. juzijuzi serikali imesaini mkataba was kuchimba madini muhimu lakini madini hayo yanaondoka kama malighafi viwanda vinafunguliwa nje , ajira kwao halafu tinauziwa hivyo lazima waafrika watoke wakatafute ajira nje ya kwao sababu hamna ajira kwetu.
Nchi za ulaya zimeruhusu viongozi wa Africa kuficha pesa kwenye nchi zao ambapo pesa hizo zimepatikana Kwa njia za rushwa badala ya pesa hizo kuzuiwa mfano ni Abacha na viongozi wengine.
Nchi za ulaya zimepora rasilimali watu, waliona watu wenye ujuzi wanawapa mishahara minono na hata uraia, mfano Kuna kipindi Africa Kusini walikuwa wanalalamika wamesomesha manesi ila wakihitimu wanakimbilia ulaya badala ya kutumikia nchi zao. Waliona watu wenye vipaji wamekuwa wakiwapa uraia badala ya kuwaachia warudi nchini kwao na kusaidia, rejea kauli ya Mournho aliyesema nchi za kiafrika kutwaa kombe la Dunia mpaka FIFA itakapozuia wachezaji wa Africa kuchezea timu za taifa ulaya, Ufaransa walichukua kombe la Dunia huku timu Yao ikiundwa na asilimia kubwa ya wachezaji wa asili ya Africa.
 
Mkuu, uko sawa 101%

Afrika tunapaswa kusoma kwa makini haya matukio ya sasa na kujifunza sana.

Ni somo kubwa sana kwa sisi waafrika.
 
Back
Top Bottom