Kwa Ramani ya Gambia ilivyo ECOWAS wataipiga ndani ya one week!!

Mkuu vikwazo vitakuwa na matokeo lengwa ikiwa tu wataweza kuzuia mlango bahari (bandari) uliopo banjui usitumike.. Hii inamaanisha vikosi vya majini-Navy wafanye blockade kama Israel wanavyowafanyia Wapalestina wa Gaza.. Hakuna kitu kuingia wala kutoka.. Vinginevyo jamaa ataendelea kufanya biashara hasa kuagiza vitu toka nchi za mbali haswa ulaya na kusini magharibi ya Afrika

Mkuu unachokiongelea kinaitwa PACIFIC BLOCKADE,
Ni moja ya kikwazo kinachofanya kazi vizuri sana.
 
Ujinga wa nchi za Afrika zinakuwa mstari wa mbele kwenye mambo ya kijinga..
Nigeria wameshindwa kuwaondoa waasi wa waliteka watoto wa shule wataweza kumtoa rais???
Wameshindwa kukomesha mauaji. Afrika ya kati wataweza kumtoa rais???
AU bado wanasafari ndefu
ni rahisi kupigana na jeshi la nchi kuliko waasi ambao hata kambi ao hazijulikani na hata sare zao hazijulikani upo.
 
Kuzungukwa siyo kigezo cha kupigwa bali ni faida inayomrahisishia kuwapiga kirahisi wanaomzunguka. Mmoja anawapiga 10 kirahisi kwa vile yeye anachagua ampige wa kulia halafu wa kushoto, mbele ama nyuma wao wanabaki kupigana wao kwa wao.
Dah... Gambia yenyewe ina wanajeshi wasiozidi 1200...magari ya deraya 4.....ndege za kizamani 3.....vifaru 2.... Wapakistan walikuwa wamejaa kuwafundisha wote wamesepa....Hivi mnadhani yule Jenerali wa Gambia aliyesema anawapenda wapiganaji wake na hataki kuwa husisha na upuuzi ni mjinga?
Kama ndiyo hivyo basi Jemmah kabaki na walinzi wasiozidi 50....magari 2 ya deraya...na vijimanowari 2....Kwa ulinzi huu hata askari wa jiji wataweza kumtoa ikulu
 
Sidhani kama unajua jeshi vizuri!kuzungukwa pande zote sio hoja ya ushindi kwenye medani za kijeshi!bali mbinu na uimara wa jeshi husika..mfano mzuri ni rwanda!imezungukwa kila kona na ni ka nchi kadogo lakini kana jeuri kupita maelezo..Hebu tafakari tena!
Tukiongelea medani za kijeshi kwenye uwanja wa kivita position yako na ya adui ni determinant factors kubwa sana. Na ukiangalia nchi hizi mbili zilivyo tu Gambia hawezi kufua dafu kwa Senegal. Kwanza ina wanajeshi wachache due to her population, kutokana na ukubwa wake yaonekana tu haina vifaa vya kutosha kuweza kujilinda ma mashambulizi yatokayo kila upande wa Senegal kumzunguka.
Ushauri; Jamaa angeachia tu madaraka kuepusha kuharibiwa kwa miundombinu ambayo ameihangaikia miaka nenda rudi, kuepusha vifo vya watu wasio na hatia kisa ubongo wake mfinyu kushindwa kufanya maamuzi ya busara mapema
 
Back
Top Bottom