Kwa Ramani ya Gambia ilivyo ECOWAS wataipiga ndani ya one week!!

Eti Rwanda ina jeuri, my foot! Rwanda ina jeuri gani? Kuingia Congo kuiba maliasili? Mbona walishindwa kuwatetea M23; kitengo mahsusi cha jeshi la Rwanda cha wizi wa maliasili za Drc, jeuri ipi?!
Kuingia DRC na kuiba tayari ni jeuri!usitoe povu mama..
 
Jammeh hana mpango wa kuanzisha vita, ila nchi zenye kupenda vita kama Senegal ndizo ambao zinakuwa kimbelembele
 
Sidhani kama unajua jeshi vizuri!kuzungukwa pande zote sio hoja ya ushindi kwenye medani za kijeshi!bali mbinu na uimara wa jeshi husika..mfano mzuri ni rwanda!imezungukwa kila kona na ni ka nchi kadogo lakini kana jeuri kupita maelezo..Hebu tafakari tena!
Rwanda ilipigana na nchi gani ikashinda? M23 ni ya wapi? Ilitwangwa kwa muda gani?
 
Umeuliza swali zuri. Labda humu hatuwezi pata jibu na huenda siyo mahali sahihi. Na ni ukweli pia wasomaji humu ndani tunapata hasira kweli kweli kwa yanayotokea huko, hata mimi nilitamani kuwe na uwezo wa kutuma tu kikosi kazi kwenda kumnyakua jamaa kama tulivyosikia kwa Osama, lakini naamini ECOWAS hawatafanya makosa kwamba wapiga kura wataabike kwa maamuzi yao wakati waliombwa kufanya maamuzi ?
yan Jameh watamfanya kama ilivofanywa Comoro na AU ikiongozwa na Tz
 
Sidhani kama unajua jeshi vizuri!kuzungukwa pande zote sio hoja ya ushindi kwenye medani za kijeshi!bali mbinu na uimara wa jeshi husika..mfano mzuri ni rwanda!imezungukwa kila kona na ni ka nchi kadogo lakini kana jeuri kupita maelezo..Hebu tafakari tena!
Au israel imezungukwa pande zote
 
unaposema akamatwe tu ni nan atakayemkamata na mtu yupo nchin kwake na majesh yake yanamsapoti????????
Majeshi unifomu tu yale, idadi batalioni 2, hawana navy wala airforce, manowari ya Nigeria iko pale nje ya Banjul, mji mkuu wa Gambia tangu jumamosi, hawajui wafanye nini! Kanchi kenyewe upana km 55 urefu km 300; hata FFU yetu au GSU ya Kenya wanakatiza pale kwa masaa machache sana!
 
Nimezungumzia jeuri sio vita!Huu ukanda wetu una utulivu lakini angalia au jikumbushe mikwara ya kagame..Hata hivyo mfano huu unaweza kuufananisha na mataifa ya mashariki ya mbali..Utagundua kitu kwa niliyokueleza..
Sisi tunaongolea vita sio jeuri
 
Hivi hakuna njia nyingine yoyote ya kumfanya Jammeh aachie madaraka zaidi ya kumvamia kijeshi?
Gambia ni nchi ndogo sana na uchumi wake ni wa biskuti, mkiwawekea vikwazo miezi mitatu tu ni lazima uvunjike.
Kimkakati uvamizi wa kijeshi ni njia ya mwisho endapo njia nyingine zimeshindwa.
Wanaweza kuvamia The Gambia na kusababisha majanga makubwa zaidi hata ya Jammeh.
Matatizo ni wazungu. ..msiponunua silaha na kuzitumia atakula wapi? Angalia movie inayoitwa LORD OF WARS. .INASIKITISHA SANA WALAHII
 
Hivi hakuna njia nyingine yoyote ya kumfanya Jammeh aachie madaraka zaidi ya kumvamia kijeshi?
Gambia ni nchi ndogo sana na uchumi wake ni wa biskuti, mkiwawekea vikwazo miezi mitatu tu ni lazima uvunjike.
Kimkakati uvamizi wa kijeshi ni njia ya mwisho endapo njia nyingine zimeshindwa.
Wanaweza kuvamia The Gambia na kusababisha majanga makubwa zaidi hata ya Jammeh.
Naunga mkonyo hojaaa
 
Hakuna njia nyingine mkuu! Na Leo Bunge limemuongezea muda wa kukaa madarakani, Na limepitisha hari ya taadhari aliyoitoa! Binafsi Na support nguvu ya kijeshi dhidi yake, Na lazima apigwe Tu, mpaka Jana Mawaziri 5 wameachia ngazi, more than 20 years Yuko madarakani, anataka nini zaidi!???
 
Umeuliza swali zuri. Labda humu hatuwezi pata jibu na huenda siyo mahali sahihi. Na ni ukweli pia wasomaji humu ndani tunapata hasira kweli kweli kwa yanayotokea huko, hata mimi nilitamani kuwe na uwezo wa kutuma tu kikosi kazi kwenda kumnyakua jamaa kama tulivyosikia kwa Osama, lakini naamini ECOWAS hawatafanya makosa kwamba wapiga kura wataabike kwa maamuzi yao wakati waliombwa kufanya maamuzi ?

Nakuelewa mkuu,
Lakini ukweli ni kwamba hata kama wameombwa na wapiga kura wa Gambia,
Uvamizi wa kijeshi siyo njia sahihi kwa sasa, wangemuwekea vikwazo vya kiuchumi tu.
Lazima atasalimu amri.

Tukiangalia hili jambo kwenye taswira kubwa,
Afrika yetu haitakiwi iige kila kitu kutoka Ulaya na Marekani,
Kama tukianza kuvamiana kijeshi leo, nakuhakikishia haitaishia hapo tu.
Litakuwa ni Zimwi Jipya kuingia barani Afrika mbali na Umasikini, Maradhi na Ujinga.

Utasikia uchaguzi wa Zimbabwe haukuwa huru na haki,
SADC itume kikosi kazi kwenda kumtoa Robert Mugabe.
Utasikia tena Uchaguzi wa Burundi siyo wa huru na haki,
Rwanda na Uganda wanapendekeza EAC itume kikosi kazi kumtoa Nkhurunzinza.

Mwishowe tutakuja kufika sehemu,
Nchi kubwa zenye nguvu zitatumia huo mwamvuli kuvamia nchi nyingine.
Mwaka 1938 Adolf Hitler alivamia Czechoslovakia akisingizia kwamba anaenda kulinda haki za raia wa Czech na Slovakia.
Lakini ukweli ni kwamba alichokifanya Hitler ulikuwa ni Uhalifu wa kivita.

ECOWAS watakuwa ni watu wa hovyo sana kama wakikubali kufanya huu uamuzi,
Hovyo! Hovyooo kabisaaaaa!!!!
 
Majeshi unifomu tu yale, idadi batalioni 2, hawana navy wala airforce, manowari ya Nigeria iko pale nje ya Banjul, mji mkuu wa Gambia tangu jumamosi, hawajui wafanye nini! Kanchi kenyewe upana km 55 urefu km 300; hata FFU yetu au GSU ya Kenya wanakatiza pale kwa masaa machache sana!
Hawa FFU mtaani tunawaita fuka fuka wakuu huwa wabishi, wajeuri na wanapenda sana sifa wakipewa hilo jukumu wanaweza kukubali na kwenda kumchallenge huyo Rais wa Gambia kwa kumng'oa bila hata kuhoji uimara wa adui.
 
Hakuna njia nyingine mkuu! Na Leo Bunge limemuongezea muda wa kukaa madarakani, Na limepitisha hari ya taadhari aliyoitoa! Binafsi Na support nguvu ya kijeshi dhidi yake, Na lazima apigwe Tu, mpaka Jana Mawaziri 5 wameachia ngazi, more than 20 years Yuko madarakani, anataka nini zaidi!???

Kwa hiyo Mkuu wangu,
Kukaa madarakani miaka 20: Bunge kumuongezea muda wa kukaa madarakani :Na Mawaziri 5 kuachia ngazi unadhani ndiyo sababu tosha za kuidhinisha uvamizi wa kijeshi nchini Gambia?
 
Back
Top Bottom